Nape: Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM!

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
331
Wakati wa hafla ya kumpokea Mbunge wa Igunga Katibu wa uenezi na itikadi wa CCM, NAPE NNAUYE, ametamka kuwa kuna watu wanataka kuleta vurugu. Na kwamba hawajui kuwa nchi ina wenyewe, na wenyewe ni CCM.

Je ni kweli kwamba nchi ni ya CCM? Na kama nchi ni ya CCM kuna wakati wowote watakubali kumpa mtu au chama kingine?.
 

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,711
1,365
Wana JF leo nimepata mshtuko wa ajabu baada ya kumsikia Nape akihutubia wana CCM pale Manzese na pamoja na mengi aliyozungumza amesema "Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM".

Je huu ndio uzalendo kweli? Nchi hii ni ya CCM? Na sisi ina maana nchi yetu ni ipi?

Kwa maoni yangu serikali ya CCM imekuwa kama serikali ya mkoloni mzungu, aliyeamini kuwa Africa ni ya kwao na sisi wananchi ni watu wa kutawaliwa. Mashujaa wetu wakawafurusha wakaondoka.

Mawazo yangu ni kuwa wakati umefika wa kuifurusha CCM kwa nguvu ili wajue kuwa nchi hii wenyewe si wao wasio na uchungu na nchi hii kwa kuwafuga mafisadi bali wenye nchi ni wale wenye uchungu wa nchi hii.

Saa ya ukombozi ni sasa.
 

Stigliz

Member
Aug 9, 2011
44
13
Hawa wanajichimbia kaburi,mazuzu ccm ni wengi,tunapoelekea wananchi mpaka vijijini wanajua kutenga mbivu na mbovu.Tusubiri mwakani uone jinsi ccm itakavyo paranganyika.
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni sisi Watanzania, sio CCM, CDM wala CUF wala CCK.

Viongozi wa CCM huwa wananishangaza sana wanapodai wenye nchi ni CCM pekee. Kwa CCM kujimilikisha hakimiliki ya nchi yetu ni wazi hawatutakii mema.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Akasisitiza wao wapo tayari kusema tuandamane hadi ikulu kuindoa serikali na hawaoni aibu amani endapo itapotea!

Akasema serikali haiwezi kulikubali hilo, naye Nchemba akasema walimu wanaposimamia
uchaguzi wakumbuke kuwa wao ni watumishi wa serikali na endapo CDM isingesaidiwa na walimu basi CDM ingepata kura 1000!
 

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kaka umeniwahi kupost mada hii.

Mimi mwenyewe nimemsikia Nape kupitia habari ya ITV. Nimeguswa sana ukizingatia mimi sio mwanachama wa ccm na wala sitegemei kuwa mwanachama wa chama hicho.

Kwa kauli hiyo ya Nape anamaanisha wale wote wasio wana ccm nchi hii si yao na hivyo wanapaswa kutafuta mahali pengine pa kuishi. Nape amechoka mapema sana wakati umri wake bado mdogo.

Nape atwambie tusio wanachama wa CCM twende wapi kama nchi hii ni ya CCM! Vinginevyo ajitokeze hadharani nakufuta kauli yake na akiri kwamba ulimi uliteleza.
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,606
20,998
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi! Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

hata mimi nimeshndwa kumuelewa bt i came with conclusion kwamba jamaa ni left hand(co mzma atakuwa ni mlemavu wa kufkr)
 

Makamuzi

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,155
263
hapa ndo nawashangaa viongozi wa ccm wanaosema nchi hii ni yao,lakini simshangai nape kwani uwezo wake wa kufikiri ni mdogo tangu akiwa anasoma Nsumba,anabwabwaja tu.
 

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni sisi Watanzania, sio CCM, CDM wala CUF wala CCK.

Viongozi wa CCM huwa wananishangaza sana wanapodai wenye nchi ni CCM pekee. Kwa CCM kujimilikisha hakimiliki ya nchi yetu ni wazi hawatutakii mema.

Nimemfananisha Nape na mtoto wa gadhaffi juu ya kauli zake kwa wa libya,lakini sasa anaishi mafichoni na cockroach wako tripol.
Jaji Warioba alisema haioni serikali ya Tanzania iliyopo ni serikali ya CCM.
 
  • Thanks
Reactions: mku

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi! Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

kauli zenye utata kama hizi huko majuu, kibarua cha nape kingeota nyasi leo na mapema.

wanapinga ubaguzi huku wanahubiri ubaguzi.
 

nzitunga

Senior Member
Oct 31, 2010
193
52
Kwa imani kama hizo, kujifanya wao ndo wenye nchi, ndo maana wanafanya lolote wawezalo hata kuvunja sheria, hata kuwachonganisha watu kwa imani zao, hata kuleta vita ili mradi tu wabakie madarakani.
Tumekwisha gundua janja yao, hii nchi ni ya kwetu, watanzania! kama walishauza walionunua wametapeliwa kwani 2015 everything will come back to Tanzanians.
Pole Nape na magamba yako!
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni sisi Watanzania, sio CCM, CDM wala CUF wala CCK.

Viongozi wa CCM huwa wananishangaza sana wanapodai wenye nchi ni CCM pekee. Kwa CCM kujimilikisha hakimiliki ya nchi yetu ni wazi hawatutakii mema.

Katika mazingira kama haya mtu huwezi kuwa na shaka na uwezo na uelewa wa nape kwamba uko chini sana tena below minimum.

Kama ccm inakadiriwa kuwa na wanachama milioni tano miongoni mwa watanzania wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni arobaini, mtu mwenye uelewa wa kawaida hawezi kusema 12% ya watanzania ndio wenye nchi, huo utakuwa ni upuuzi mkubwa.
 

SILENT ACtOR

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
628
181
Bado tu anayoongea Nape yanakuumiza ubongo? Yule profession yake ni "MC" .Husema chochote ili kuwafurahisha bwana wakubwa ccm. We mwache aongee, kwani 40 za mwizi zi karibu, ni suala la muda tu.
 

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Katika mazingira kama haya mtu huwezi kuwa na shaka na uwezo na uelewa wa nape kwamba kiko chini sana tena below minimum.

Kama ccm inakadiriwa kuwa na wanachama milioni tano miongoni mwa watanzania wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni arobaini, mtu mwenye uelewa wa kawaida hawezi kusema 12% ya watanzania ndio wenye nchi, huo utakuwa ni upuuzi mkubwa.

hapo ndo ujue kuwa kuna baadhi ya watu ccm wanawaza kwa kutumia 'masaburi'
 

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,489
907
Ila Mie namkubali nape.. ametusaidia kujua kumbe CCM yote ni Bongokufa sio bongolala tena.. Kama mropokaji. msemahovyo, chapombe, mtukanaji kwenye threads humu jamvini, mtu asiyeshaurika Nape ndo kiongozi wa wengine humo CCM, sasa unadhani hao wenzake wakoje? -MISUKULE WATUPU
 

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Nape hazimtoshi atwambie sisi tusio wana ccm tuende wapi au anataka tuingie msituni kama waasi wa Libya, uganda na kwingineko? Atutake radhi watanzania wote.
 

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi! Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

Ni Nape yupi mkuu? Kama ni yule katibu mwenezi wa CCM nadhani ni hoja iliyondani ya uwezo wa akili yake...wala haina aja kumlaumu,kwanza naona ameenza ku-iprove maana hata kuongea mbele za watu ilikuwa ishu,kama kaweza kaa mbele ya kamera ni big improvement kwake...!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom