Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Muhamie mara ngapi tena ? Labda muuthibitishie umma tuu
chagas+ roman catholic= chadema
 
pole sana Nape kwa kazi ya uchonganishi na kutuletea ukabila nchini,kwamba CDM ni ya wachaga,
Hivi Iringa ni ya wachaga?
Mbeya je nayo ni ya wachaga?
Mwanza nayo ni ya wachaga?
Musoma ni ya wachaga?
Kigoma nayo ni ya wachaga?
Basi sisi wote tuondoke Tanzania kwa kuwa ni ya wachaga,kwa taarifa yako CDM ni chama cha UMMA haina kabila wala dini,
we dont need bla bla all we need is changes.
 
siasa za ukabila ni mbaya na mbovu sana kwa jamii ya kitanzania hasa kama mtu anayehubiri siasa hizo ni kijana...still we have a long ay to go kuhakikisha nchi yetu inajikomboa kutoka katika HUU UKOLONI MWEUSI...msitugawe kwa dini zetu, kabila zetu wala jinsia zetu.

Mchange na Wana JF wote,

Swala la uchagga ni conspiracy ndani ya ccm na wanaongea sana na kuwapiga vita wachaga hiyo siyo siri mimi nimekwisha penyezewa mambo kibao na watu wenye heshima zao ndani ya chama cha mapinduzi jinsi ya kuwaogopa wachaga na imekuwa kama buzz word ya makada wa ccm,

Na haijawahi tokea ndani ya ccm mchagga akateuliwa nafasi kubwa za nchi kama kugombea Uraisi, uwaziri mkuu, au uspika wa bunge, hilo sio siri na lazima tuwe wazi kabisa bila kuficha, hili swala lipo na ccm ni chama cha kibaguzi ijapokuwa wanahubiri umoja na mshikamano wa kitaifa majukwaani lakini yanayofanyika behind the curtain ni aibu kubwa. hivyo tusishangae kijana kama Nape anaongea kwa ujasiri mkubwa such an offensive statement na kauli ya kibaguzi kwa sababu ndo conspiracy zinazoendelea ndani ya ccm for decades now. Ushahidi tunao na hata humu wana JF nadhani baadhi yetu tumekwisha umwa masikio juu ya kujiunga na chadema kwa sababu ya hofu ya wachaga.


Na hili sio kwa wachagga tu bali kulikuwa na kama myth ndani ya ccm zidi ya makabila yote makubwa kupewa nafasi za juu za uongozi wa nchi hata kama mtu anasifa gani, huo ndo ulikuwa msimamo wa decision makers wa ccm.


Hivi sasa watu wazima ndani ya chama cha mapinduzi baada ya kuona muungano umepoteza mvuto kwa wazanzibari nimeanza kupenyezewa propaganda ya kuwa hata wazanzibari wafanye nini haiwezekani kuvunja muungano, kwani lazima tuwalinde waunguja dhidi ya wapemba kwani SULTANI bado yupo uingereza anasubiri muungano uvunjike arejee, ukiwauliza sultani atarejea kwa style ipi? hawana jibu.

mimi nadhani ccm sasa hivi wamekuwa so desperate sana kiasi kwamba wanatuchafulia nchi kwa kasi ya ajabu na kukumbatia politics of everything goes.... ("SHENANIGANS"), Kitu cha ajabu vijana kama Nape wanapokubali kuingia kwenye mtego wa siasa za kibaguzi zilizokuwepo kwa kiasi kidogo zamani, na zilianza kupotea lakini sasa ccm wanazirudisha kwa kasi ya ajabu.


Hizi siasa za udini na ukabila ndio zinaweza kuitokomeza CHADEMA kwenye ulimwengu wa siasa za nchi hii kama mlivyodhamiria kupotosha umma! na ccm ikaendelea kutawala lakini kwa gharama kubwa sana ya umoja na mshikamano wetu kama taifa! na kumbe tukaingia kwenye machafuko makubwa sana kwa kuendekeza propaganda chafu, Nape umeingia kwenye ukurasa mbaya wa siasa za nchi kwa kutosimama na kukataa siasa za kibaguzi. Hata raisi kikwete alifanya kosa kubwa sana kulitangazia taifa kwamba kuna udini, hiyo ni maswala sensitive sana yanapaswa kutatuliwa kwa kutumia busara, kwani mitaani hakuna udini, udini unajitokeze kwenye maslahi ya wana siasa tu na si vinginevyo.


Nape, kama chadema ni chama cha kikabila na cha kidini nadhani sheria za nchi hii haziruhusu chama cha siasa cha kikabila na kidini kupata usajiri, je kwa nini serikari ya chama cha mapinduzi isikifute? kwa mujibu wa sheria? kwa nini mnaendekeza hizi propaganda chafu?

Nasikitika sana kwa kijana mdogo kama wewe kuingia kwenye mtego huu kirahisi hivyo.
 
CDM IS MY RELIGION. Who is Nape anyway! Pro ccj, mropokaji, myopic, GOD KNOWS
 
Nape nafikiri hiki kitengop cha propaganda kinwafanya watu wanakuwa wendawazimu nini mh hii kali
 
happo kwenye mstari ni maneno tu but in reality i cant buy this kuwa Nape ni adui namba moja wa wachaga . kwa sababu kila siku yupo nao , na hata huko shule aliposoma lazima alikuwa na wachaga na wengi lazima watakuwa wamemsaidia hata hesabu au fiziks au biology ,we can say may be ulimi ulimtelleza na kungekuwa na uwezekano angeomba msamaha ila anaogopa
sidhani kama alisoma fisikia na hesabu vinginevyo asingeweza kutoa matashi hatarishi kiasi hiki
 
Eneza siasa na sera za chama chako Nape,..
mbona umekimbia sasa?
huwezi kujibu hoja eh?

Alikuwa anatikisa kiberiti, naona kaona njiti ziko kibao..tena imara...kakimbia. Akale kozi tena ndio arudi humu kujibu hoja. Kuomba radhi ni ngumu eeh!
 
haya jamani...yeyote mwenye clip ya Nnape akisema 'siendi chadema kwani mi mchaga??" ailete humu aseee.ili mada iishe fasta..
 
huyu Jamaa analeta Siasa za Maji taka. we don't need cheap politics in Tanzania. bwana Nape unataka kuleta Ukabila Tanzania amakweli umefilisika kimawazo, hivi unafurahia nchi jirani wanavyo chinjana kwa Upuuzi wa UKABILA. Ndugu Watch out, neno tu linatosha kuchafua hali ya hewa.
 
CCM tumechoka, tukubali yaishe, pia nipo CCM ila tukubali ukweli kwamba hatua budi kujianda kuwa chama cha Upnzani. Tukubal tusikubali tuelekeako ni kugumu kuliko tutokapo. Watanzana wote wamekua wajanja na wanatusanifu tu

Angalieni wenzetu CHADEMA walivyo na mass suport, Elimu ya Uraia ni nzuri kwa sasa na hatuna la kufisha

Sie si wawajibkaji tena na kioo chetu chote ni kichafu,tuanzgalie njia mpya hata kama ni kuwahaa daa watanzania, isiwe hizi siasa za Nape anazoanzisha za Udini na Ukabila.

Kama ndiyo inamaana Mh. Mkapa kwa Wakati huo alikua anawawaklisha Wakristu wa thehebu la Kikatoliki, au kwa kua alikua CCM, basi hakuna Udini, naye Kikwete anawakilisha akina nani kwa sasa?.

Mawazri na wabunge wote wenye asili ya Uchagga huko CCM wanajipendekeza ua?

Ukweli CHADEMA wanaongea mambo ya uhalisia na si poropaganda za kijinga kama CCM,na ndo maana Wasom kwa ngazi tofaut kwa pamoja na waso wa som wanakubaliana na hoja za CHADEMA.

Just try to conduct a very simple evalution during our compsign and that of CHADEMA to find out which party gets our more Fun

Tufikirie mbele na sio kuzozana kana kwamba sie wanaCCM n chama cha Upinzani
 
huyu angekuwa nchi za watu angekuwa ameshajiuzulu maana anahimiza hate...! ndo wana siasa tulionao Tanzania nathani ana uhakika kwamba yeye ni Mmakonde kama mama yake alivyomuaminisha na si Mchagga au kabila lingine maana alifanya DNA test

nape amekaa kichaga
 
Nape, wewe bado ni kijana mdogo katika siasa. Una future kubwa sana katika siasa kama utachunga kauli zako. CCM inaweza kuanguka kesho lakini wewe bado ukabaki mwanasiasa. Zungumza kama vila vile CCM sio mwisho wa kila kitu. Kumbuka siasa 'is all about public opinion' Watu wanadhani umekosea ulivyodai CDM ni ya wachaga, omba msamaha tusonge mbele. Kuna kesho!
 
jeykey,acha kujivisha uhusika usio kufaa,angalia michango yako mara jenga chama chenu,mara jenga chama chetu,sasa w
w uko wapi? Nape alikuwa na kila sababu ya kusema cdm ni chama cha kichaga kwan uongo? Watanzania weng wanajua hivyo toka mlipomzuia Zitto kugombea uenyekiti kwa sababu zisizojulikana,sasa unamtisha nan eti wachaga mmezaa na kabila nying,ni kabila gan ambalo halijazaa na kabila nying? Chadema achen ubabaishaji ktk mising ya ukweli,Unaleta uongo usio na msing et Nape kapanda jukwaan,jukwaa gan? Na wap? Tuwe wakweli sio kuponda tu
 
08_10_zbraec.jpgSiasa ni Mchezo Mchafu.. Tunataka Maisha Bora Ya Nini Marumbano Sababu Ni Mateso Lakini Pembeni Sijiweki
 
Nape hajui maana ya ukabila. Je wabunge wote ni kabila moja? Je viongozi wa juu ni kabila moja? Nape acha ujinga.
 
Acha upuuzi, tumi bongo lako kufikiri na sio kututolea ushuzi hapa. Hata updates za nchi hauna, unongea tu yanayokutoka.

wahame serikalini....labda wengine tutapata kazi huko....waache kazi serikalini(TRA) labda tutapata kazi na sisi......n amadili yatapungua ...kwanza huomba rushwa bila aibu....tokeni mchana kweupe tokeni tutanufaika....!
 
Sikupendezwa na kauli za nape kusimama majukwaani na kuubili ukabila, hii ni mbaya kwa Tanzania nahisi viongozi wakuu watakuwa wamamuonya. Propaganda hazifanywi kwa kushutumu hisia za watu, Mimi ni mchaga ina maana kwa kauli yao niame kwenye chama chetu??

Sisi wachaga tumezaa na makabila mengi hapa tanzania ina maana na wenyewe waame? Nape hacha utoto huu katika siasa, Jenga chama na sio kutuaribia chama


Ukichezea hisia za mtu anaweza kukujeruhi au kukuuwa, wewe unajisikiaje ukitembelea sehemu ambazo ziko wachaga wa ccm? unajirinje?

Nakupa ushauri
Tujengee chama chetu 2015 tushike dola

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Bariki Makabila yote
Mungu mbariki Raisi wetu

Umesema Mungu mbariki Raisi wetu. Je ni raisi yupi unayemzungumzia ? Ni yule dr wa uongo na aliyechakachua matokeo au ni yule Dr. wa ukweli na aliyeshinda matokeo na anayeendelea kuishi mioyoni mwetu ? Kama ni huyu wa mwisho, nakubaliana nawe. lakini kama ni huyo wa kwanza, mmmmh, huyu siye raisi wangu
 
Umesema Mungu mbariki Raisi wetu. Je ni raisi yupi unayemzungumzia ? Ni yule dr wa uongo na aliyechakachua matokeo au ni yule Dr. wa ukweli na aliyeshinda matokeo na anayeendelea kuishi mioyoni mwetu ? Kama ni huyu wa mwisho, nakubaliana nawe. lakini kama ni huyo wa kwanza, mmmmh, huyu siye raisi wangu

Rais kikwete
 
Back
Top Bottom