Nape: Mapendekezo ya wabunge kuhusu muswada wa Sheria ya Taarifa Binafsi yatazingatiwa kwenye uundaji wa Kanuni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Leo Novemba 1, bunge la Tanzania limesoma kwa mara ya ili muswada wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ikiwa ni baada ya kuokea maendekezo kutoka kwa wadau mbali mbali ikiwemo Jamii Forums.

Waziri Nape Nnauye ambaye ni waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akihitimisha baada ya mapendekezo ya wabunge amesema mapendekezo hayo yatatekelezwa kwenye uundaji wa kanuni.

Hata, hivyo amesema kwa mapendekezo ya ulinzi wa taarifa za marehemu na watu wasio na uwezo wa maamuzi kama watoto, wagonjwa na wenye ulemavu Muswada unaopendekezwa umezingatia hilo.

Muswada wa sheria binafsi umetajwa kuwa utaongeza kwa kiasi kikubwa wawekezaji ambao huangalia sana uwepo wa Sheria ya Taarifa binafsi.

Sheria hii ikisainiwa Tanzania itaingia katika nchi nyingine zenye sheria ya ulinzi wa Taarifa binafsi zikiwemo nchi za Afrika Mashariki na SADC.
 
Udukuaji wote sio mbaya na hautakwisha maana ni njia moja kubwa ya kulinda usalama wa nchi na ni njia rahisi ya kudhibiti rushwa kwa watu hasa watumishi wa umma
 
Back
Top Bottom