Uongo mtupu...angalieni marudio ya Taarifa ya habari ya Star TV kesho asubuhi mtaona...anasingizia eti mimi nilikatisha hotuba yangu wakati niliongea dakika zote nilizokuwa nimepangiwa!
Vijana wa CDM waliokuwepo pale ni wachache sana, kama 15 hivi ukilinganisha na wengi wenye hekima na busara waliokuwa wametulia na kufuatilia hotuba zetu.
WanaJF hebu jiulizeni kitu hapa, kama watu wa CDM walikuwa wengi kushinda wa CCM na walikuwa wanazomea na greenguards wakaenda wakamkamata mfanya fujo mmoja, CDM si wangeleta vurugu mbaya kabisa, pengine hata mauaji? Iliwezekana vipi CCM kuendesha mkutano wake vizuri na kwa amani na utulivu kabisa mpaka mwisho kama kweli kulikuwa na fujo za kiasi kilichoelezewa namna hii?
Waandishi ni mhimili wa nne wa dola, fanyeni kazi yenu kwa ufanisi na kimaadili. Nchi yetu sote basi tuilinde!
kaka nina mambo machache naomba unijibu kuhusiana na hiyo sehemu niliyo weka nyekundu
1. Vipi ni halali kwa kila chama kuwa najeshi lake kama hivi mnavyofanya na kuwapeleka makambini kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi au ni ruksa kwa ccm tu?
2. Je vijana hawa hulipwa kiasi gani na nani na kwa kufungu lipi au wanajitolea tu kwa mapenzi waliyonayo katika chama chao?
3. Vipi mkuu vijana hawa khali yao kimaisha ikoje wapo angalau wanaomiliki walau nyumba moja ya kisasa au hapana?
4. Mkuu nijuze kuhusu elimu ya vijana wetu hawa kwa wastani elimu yao ni ya kiwango gani ?naomba unijibu hili niweze kuwafahamu kwa kina hawa vijana
mkuu ukiwa kiongozi na ukategemea walinzi na bastola pale unapoenda kuonana na wale unaowaongoza wewe si kiongozi .
Sehemu pekee ambapo unaweza kuupata ukweli kama ulivyo ni JF....gazeti sitegemei kama wataandika matusi hayo ya NapeSource yako ambayo ni gazeti la Mwananchi haina matusi ambayo umeandika ktk thread hii sasa tukuaminije au umewalisha maneno?
Hawa jamaa wamechanga nyikiwa huyu anasema hivi huku mwingine anasema kinyume chake...Nape alisema nchii hii ina wenyewe Kimwangalla ana sema nchii ni yetu sote sasa sijui wana amini lipi............Nape anaamini hivi pia?
Frederick Katulanda, Mwanza-Mwananchi
MKUTANO wa hadhara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magoneni, Kirumba jijini hapa,
Nape alianza kwa kuwapongeza Nchemba na Lusinde akisema walipokuwa wakizungumza walikuwa wakikamata pua za wagonjwa wakorofi ili yeye aweze kuwanywesha dawa.
Wakati akihutubia, vijana wa Green Guard walianza kufanya doria kuwasaka wazomeaji na kijana wa kwanza alikamatwa na kushambuliwa na vijana zaidi ya saba kiasi cha kumfanya Nape kukatisha hotuba yake kumuokoa.
Hali ilichafuka tena pale aliposema viongozi wa upinzani hawana uchungu na nchi na kwamba CCM ni waungwana na ndiyo maana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wake Mkuu, Dk Wilibroad Slaa hawajawahi kuguswa kwa risasi huku akiwahoji kuwa tangu siasa za vyama vingi zianze ni wapi ambako viongozi hao walifanyiwa hivyo? Hata hivyo, alijibiwa kwa nguvu na kundi la watu ... "Arusha."
Majibu hayo yalisababisha vurugu nyingine kwani kijana mwingine alikamatwa na kuanza kupigwa na vijana hao wa CCM kabla ya gari la Polisi kuwasili na kuanza kuzunguka katika uwanja huo kulinda amani.
Hivi ni kwanini Nape siku hizi ananyoa nyusi? Au nayeye ananunuliwaga suti 5 siku hizi?Anadhani kila mtu anashikishwa ukuta kama february na dada yake!
Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara jijini Mwanza jana kwenye viwanja vya Magomeni, Kirumba, Bw. Nnauye alisema mageuzi hayo ni ukombozi kwa wanyonge kwa kuwa yamelenga kuimarisha misingi ya uadilifu na kuwajibika kwa viongozi waliopewa dhamana.
"Ni rahisi leo kumkuta kiongozi anamiliki utajiri wa kutisha na kufuru kuliko hata kipato chake halali, tukisema tukae kimya nchi hii haitatawalika. Dawa ni kufanya mageuzi haya leo kabla hali haijachafuka sana," alisema na kuongeza.
"Tusisahau ndugu zangu, nguvu ya chama hiki na heshima yake imekuwa ni kutetea wanyonge nchini, Afrika na duniani kwa ujumla. Kutetea wanyonge lazima uhakikishe rasilimali za nchi zinanufaisha wanyonge, bila uadilifu na kuwajibika haitawezekana, ndio malengo ya mageuzi tuyafanyayo," alisema Bw. Nnauye.
Akitoa ufafanuzi zaidi Bw. Nnauye alionya kuwa kama tofauti ya kipato isiposhughulikiwa mapema na hasa kuwadhibiti wale wanaojilimbikizia mali kwa njia haramu wakiwemo viongozi na kugeuza chama kichaka chao, nchi itavurugika kwa kuwa wanyonge ni wengi na watatumia nguvu kudhibiti rasilimali zao na kudai usawa.
Siasa za Kuzomeana ni uhuni ambao wanasiasa pande zote lazima wazikemee! Hatuwezi kujenga na Kukuza Taifa la Wazomeaji! Tubishane kwa hoja na kumsikiliza kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake hapo ndipo tupime kama ni porojo au pointi!
Nape anachama chake anataka kuuiua CCM ili aibukie chama chake cha CCJ......Nape umeishiwa na busara wewe hufai kuwa kiongozi na hufai kuigwa na jamii. kama kweli umesema maneno hayo shame be upon you!!!!!!!
Ukiona unachangiliwa kumbuka IKO SIKU UTAKUWA UNAZOMEWA SASA KIPINDI CHA KUSHANGILIWA KWA ccm KIMEISHA NA SASA NI KUZOMEWA NDIYO MPANGO MZIMA...ccM WASHANGILIWE KWA LIPI SASA HIVI HAWANA JIPYA ACHA WAZOMEWE KWANZA WAKAZI WA MWANZA WAMEONYESHA UVUMILIVU KAMA WALITUKANWA MATUSI YOTE HAYO HAWAKUWAPOPOA MAWE....Siasa za Kuzomeana ni uhuni ambao wanasiasa pande zote lazima wazikemee! Hatuwezi kujenga na Kukuza Taifa la Wazomeaji! Tubishane kwa hoja na kumsikiliza kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake hapo ndipo tupime kama ni porojo au pointi!