Nape, Lusinde walichokuta Mwanza kimewatosha

Eraldius

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
1,120
906
Timu ya CCM iliyotumwa Mwanza Nape, Lusinde wamechemsha na wameishia kutukana.

Lusinde kasema atatupiga mimba, Nape kasema atatupandisha ukuta. Kweli hawa ndio viongozi wa kitaifa?.

Cha kushangaza Mwanza hadi watoto hawataki habari za CCM.

Kutoka gazeti la Mwananchi:
Frederick Katulanda, Mwanza

MKUTANO wa hadhara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magoneni, Kirumba jijini hapa, uliingia dosari baada ya kundi la vijana kuwazomea viongozi karibu wote wa chama hicho waliopanda jukwaani na kukifanya kikundi cha ulinzi cha CCM, Green Guard kutembeza kipigo hadharani.Katika mkutano huo, Nape alikuwa amefuatana na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangalla.

Baada ya kuanza saa 9: 55, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Shaibu Akwilombe ambaye pia ni Katibu wa Wilaya ya Ilemela alipanda jukwaani kuwatambulisha makada wa chama hicho waliokuwa katika msafara wa Nape kisha kumkaribisha Dk Kigwangalla kuzungumza.

Akizungumza katika eneo hilo ambalo ni moja ya ngome maarufu za Chadema, Dk Kigwangalla alisema katika zama za sasa hakuna chama kinachoweza kuwafikisha wananchi katika uchumi mwema zaidi ya CCM. Kauli hiyo ilionekana kuwakera baadhi ya wananchi hasa vijana walikuwapo katika mkutano huo ambao walianza kuzomea huku wengine wakiguna.

Kuona hivyo, Dk Kigwangalla alikatisha hotuba yake akisema yeye siyo msemaji wa mkutano huo. Akwilombe alirejea jukwaani, safari hii akionekana kujawa na hasira na kusema hatakubali kuona watu wakileta vurugu na kusema wanaofanya hivyo wanapima kina cha maji kwa kuweka mguu.

"Hata bila ya polisi hatuwezi kukubali fujo zitokee katika mkutano wetu… na sasa namkaribisha Lusinde kuwasha moto na wanaotaka kupima kina cha maji kwa mguu waone..," alisema Akwilombe.

Lusinde aliposimama alisema kelele za kuzomea amezizoea na amejifunzia Tarime ambako alikuwa Katibu wa CCM hivyo hazimpi shinda.

"Hawa wanajifunza kutoka Tarime, wanaiga mambo ya utoto, huu mkutano siyo wako ni mkutano wa CCM wewe unakuwasha nini? Kama unaona huwezi kuvumilia mwana CCM usiende kwenye mkutano wa Chadema na kama mwana Chadema huwezi kuvumilia mkutano wa CCM usiende! Wanachofanya ni kwamba uvumilivu kwa vijana wa CCM unafika mwisho," alisema.

Kauli hiyo ilikuwa kama kutia petroli kwenye nyasi zinazowaka kwani ilizidisha vurugu huku zomeazomea ikiongezeka baada ya hali hiyo kuendelea, Lusinde alisema: "Hii ni nchi yetu wote kilichotokea hapa (Kata ya Kirumba kuongozwa na upinzani), wanakijua, lakini lazima wajue hakuna watu wenye haki ya kuzunguka nchi nzima na wengine wakakosa."

Ilipofika zamu ya Nchemba ambaye alikuwa Mratibu wa uchaguzi mdogo wa CCM, Igunga alisema Chadema kimeshindwa Igunga kihalali na kwamba anashangaa kusikia kikilalamika kuibiwa kura.

Alisema katika uchaguzi huo hakuna masanduku ya kura yaliyopotea wala kituo ambacho kura zake hazikuhesabiwa. Alidai kwamba kama Chadema kisingefanya hujuma, kisingepata kura zaidi ya 1,000.

Baada ya Nchemba iliwadia zamu ya Nape. Vurugu zilitokea mara mbili wakati kiongozi huyo machachari wa CCM alipokuwa akihutubia.

Nape alianza kwa kuwapongeza Nchemba na Lusinde akisema walipokuwa wakizungumza walikuwa wakikamata pua za wagonjwa wakorofi ili yeye aweze kuwanywesha dawa.

Wakati akihutubia, vijana wa Green Guard walianza kufanya doria kuwasaka wazomeaji na kijana wa kwanza alikamatwa na kushambuliwa na vijana zaidi ya saba kiasi cha kumfanya Nape kukatisha hotuba yake kumuokoa.

Hali ilichafuka tena pale aliposema viongozi wa upinzani hawana uchungu na nchi na kwamba CCM ni waungwana na ndiyo maana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wake Mkuu, Dk Wilibroad Slaa hawajawahi kuguswa kwa risasi huku akiwahoji kuwa tangu siasa za vyama vingi zianze ni wapi ambako viongozi hao walifanyiwa hivyo? Hata hivyo, alijibiwa kwa nguvu na kundi la watu ... "Arusha."

Majibu hayo yalisababisha vurugu nyingine kwani kijana mwingine alikamatwa na kuanza kupigwa na vijana hao wa CCM kabla ya gari la Polisi kuwasili na kuanza kuzunguka katika uwanja huo kulinda amani.

Mkutano huo unadaiwa kuwa ni wa maandalizi ya kampeni za kuwania kiti cha udiwani wa Kata ya Kirumba ambacho kipo wazi baada ya diwani wake, Novatus Manoko (Chadema) kufariki dunia
 
we mleta habari haueleweki... ulileta nyingine ya kikao hichohicho ukaulizwa maswali ukakimbia sasa umekuja na hii

kuwa muwazi au omba watu wakusaidie kuandika
 
Cha kushangaza wamekuja na ajenda za Igunga na ajenda ya matusi.

Lusinde anatakiwa akapimwe yeye akili manake hii hoja aliitoa bungeni kwamba kuna haja ya baadhi ya wabunge kupimwa akili..

Ila nasema kama CCM inawategemea hawa watu, imeishiwa.
 
Timu ya CCM iliyotumwa Mwanza Nape, Lusinde wamechemsha na wameishia kutukana.

Lusinde kasema atatupiga mimba, Nape asema atatupandisha ukuta. Kweli hawa ndio viongozi wa kitaifa?.

Cha kushangaza Mwanza hadi watoto hawataki habari za CCM.

Mkuu wamesema hayo kwenye Jukwaa by the way au walikuwa wanaongea na wewe binafsi...? na walikuwa wanamtukana nani hasa..?

Sababu sidhani kama kuna mtu mwenye ubavu wa kuweza kutukana kadamnasi inayomsikiliza alafu wakatoka wazima.
 
Wakazi kiduuchu waliohudhuria mkutano wa hadhara katika viwanja vya MAGOMENI jijini Mwanza ulio andaliwa na CCM chini ya katibu mwenezi NAPE akiwa na lengo la kueleza sera ya chama hicho juu ya kujivua GAMBA,,WAMESHUHUDIA RUNDO LA MATUSI YA NGUONI KUTOKA KWA MAKADA HAO.

Ushauri wa bure kwa ccm,NAPE hawezi siasa bora wampost kwenye bendi yao ya TOT akawape burudani ya Taarabu,,ilibidi baadhi ya watu waanze kujisogeza na kuondoka,wengine waanze kunong"ona wakimshangaa baba huyu.kama vile haitoshi ilibidi baadhi ya vijana kwa kuchoshwa na upuuzi huo waanze kumjibu poale alipouliza maswali ya kipuuzi mfano;Nani alishawahi kuwaona viongozi wa CDM wakidhurika ktk

maandamano?JIBU Likapatikana wadau wakijibu...arushaaaaaaaaa,DK.SLAAAAAAA....AKAUDHIKA AKAANZA KUYAPOROMOSHA
1.WANAUME LAKINI OVYOOOOO
2.YAONE YANAWASHWAAAAAA
3.ANAE WASHWA ASHIKE UKUTA AONE VIDUME....
Namengine mengi ya aibu,,USHAURI....CCM mkiendelea kumtumia NAPE asie na SOCIOL ETHICS mtazidi kujiaribia ila kwa MWANZA LEO MMECHEMKA NA BWANA HUYO SIDHANI KAMA ATARUDI TENA MWANZA,,,,,
THANKS,NAWASILISHA
 
Jana nili-post hapa nikasema wanaenda kuvuna aibu hatimaye yametimia.Kwa wale walioko Mwanza watakubaliana na mimi Mwanza mjini yote karibia kila mtu ni CHADEMA
 
Timu ya CCM iliyotumwa Mwanza Nape, Lusinde wamechemsha na wameishia kutukana.

Lusinde kasema atatupiga mimba, Nape asema atatupandisha ukuta. Kweli hawa ndio viongozi wa kitaifa?.

Cha kushangaza Mwanza hadi watoto hawataki habari za CCM.

Mza mnatupa wakati mgumu sana kuielewa akili yenu!

Inakuwaje wote mnatukanwa na nyie mnakubali tu? Na pengine mnashangilia! Ajabu na kweli!
 
Wakazi kiduuchu waliohudhuria mkutano wa hadhara katika viwanja vya MAGOMENI jijini Mwanza ulio andaliwa na CCM chini ya katibu mwenezi NAPE akiwa na lengo la kueleza sera ya chama hicho juu ya kujivua GAMBA,,WAMESHUHUDIA RUNDO LA MATUSI YA NGUONI KUTOKA KWA MAKADA HAO.

Ushauri wa bure kwa ccm,NAPE hawezi siasa bora wampost kwenye bendi yao ya TOT akawape burudani ya Taarabu,,ilibidi baadhi ya watu waanze kujisogeza na kuondoka,wengine waanze kunong"ona wakimshangaa baba huyu.kama vile haitoshi ilibidi baadhi ya vijana kwa kuchoshwa na upuuzi huo waanze kumjibu poale alipouliza maswali ya kipuuzi mfano;Nani alishawahi kuwaona viongozi wa CDM wakidhurika ktk

maandamano?JIBU Likapatikana wadau wakijibu...arushaaaaaaaaa,DK.SLAAAAAAA....AKAUDHIKA AKAANZA KUYAPOROMOSHA
1.WANAUME LAKINI OVYOOOOO
2.YAONE YANAWASHWAAAAAA
3.ANAE WASHWA ASHIKE UKUTA AONE VIDUME....
Namengine mengi ya aibu,,USHAURI....CCM mkiendelea kumtumia NAPE asie na SOCIOL ETHICS mtazidi kujiaribia ila kwa MWANZA LEO MMECHEMKA NA BWANA HUYO SIDHANI KAMA ATARUDI TENA MWANZA,,,,,
THANKS,NAWASILISHA
Anadhani kila mtu anashikishwa ukuta kama february na dada yake!
 
Back
Top Bottom