Nape, Lusinde walichokuta Mwanza kimewatosha

Hivi huyo Lusinde si alikuwa CDM imekuaje leo anaongea hayo matapishi? Ama kweli njaa mbaya sana. Asidhani huo ni U MC wa harusi akajisahau.
 
Frederick Katulanda, Mwanza-Mwananchi

MKUTANO wa hadhara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magoneni, Kirumba jijini hapa, uliingia dosari baada ya kundi la vijana kuwazomea viongozi karibu wote wa chama hicho waliopanda jukwaani na kukifanya kikundi cha ulinzi cha CCM, Green Guard kutembeza kipigo hadharani.Katika mkutano huo, Nape alikuwa amefuatana na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangalla.

Baada ya kuanza saa 9: 55, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Shaibu Akwilombe ambaye pia ni Katibu wa Wilaya ya Ilemela alipanda jukwaani kuwatambulisha makada wa chama hicho waliokuwa katika msafara wa Nape kisha kumkaribisha Dk Kigwangalla kuzungumza.

Akizungumza katika eneo hilo ambalo ni moja ya ngome maarufu za Chadema, Dk Kigwangalla alisema katika zama za sasa hakuna chama kinachoweza kuwafikisha wananchi katika uchumi mwema zaidi ya CCM. Kauli hiyo ilionekana kuwakera baadhi ya wananchi hasa vijana walikuwapo katika mkutano huo ambao walianza kuzomea huku wengine wakiguna.

Kuona hivyo, Dk Kigwangalla alikatisha hotuba yake akisema yeye siyo msemaji wa mkutano huo. Akwilombe alirejea jukwaani, safari hii akionekana kujawa na hasira na kusema hatakubali kuona watu wakileta vurugu na kusema wanaofanya hivyo wanapima kina cha maji kwa kuweka mguu.

“Hata bila ya polisi hatuwezi kukubali fujo zitokee katika mkutano wetu… na sasa namkaribisha Lusinde kuwasha moto na wanaotaka kupima kina cha maji kwa mguu waone..,” alisema Akwilombe.

Lusinde aliposimama alisema kelele za kuzomea amezizoea na amejifunzia Tarime ambako alikuwa Katibu wa CCM hivyo hazimpi shinda.

“Hawa wanajifunza kutoka Tarime, wanaiga mambo ya utoto, huu mkutano siyo wako ni mkutano wa CCM wewe unakuwasha nini? Kama unaona huwezi kuvumilia mwana CCM usiende kwenye mkutano wa Chadema na kama mwana Chadema huwezi kuvumilia mkutano wa CCM usiende! Wanachofanya ni kwamba uvumilivu kwa vijana wa CCM unafika mwisho,” alisema.

Kauli hiyo ilikuwa kama kutia petroli kwenye nyasi zinazowaka kwani ilizidisha vurugu huku zomeazomea ikiongezeka baada ya hali hiyo kuendelea, Lusinde alisema: “Hii ni nchi yetu wote kilichotokea hapa (Kata ya Kirumba kuongozwa na upinzani), wanakijua, lakini lazima wajue hakuna watu wenye haki ya kuzunguka nchi nzima na wengine wakakosa.”

Ilipofika zamu ya Nchemba ambaye alikuwa Mratibu wa uchaguzi mdogo wa CCM, Igunga alisema Chadema kimeshindwa Igunga kihalali na kwamba anashangaa kusikia kikilalamika kuibiwa kura.

Alisema katika uchaguzi huo hakuna masanduku ya kura yaliyopotea wala kituo ambacho kura zake hazikuhesabiwa. Alidai kwamba kama Chadema kisingefanya hujuma, kisingepata kura zaidi ya 1,000.

Baada ya Nchemba iliwadia zamu ya Nape. Vurugu zilitokea mara mbili wakati kiongozi huyo machachari wa CCM alipokuwa akihutubia.

Nape alianza kwa kuwapongeza Nchemba na Lusinde akisema walipokuwa wakizungumza walikuwa wakikamata pua za wagonjwa wakorofi ili yeye aweze kuwanywesha dawa.

Wakati akihutubia, vijana wa Green Guard walianza kufanya doria kuwasaka wazomeaji na kijana wa kwanza alikamatwa na kushambuliwa na vijana zaidi ya saba kiasi cha kumfanya Nape kukatisha hotuba yake kumuokoa.

Hali ilichafuka tena pale aliposema viongozi wa upinzani hawana uchungu na nchi na kwamba CCM ni waungwana na ndiyo maana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wake Mkuu, Dk Wilibroad Slaa hawajawahi kuguswa kwa risasi huku akiwahoji kuwa tangu siasa za vyama vingi zianze ni wapi ambako viongozi hao walifanyiwa hivyo? Hata hivyo, alijibiwa kwa nguvu na kundi la watu ... “Arusha.”

Majibu hayo yalisababisha vurugu nyingine kwani kijana mwingine alikamatwa na kuanza kupigwa na vijana hao wa CCM kabla ya gari la Polisi kuwasili na kuanza kuzunguka katika uwanja huo kulinda amani.

Mkutano huo unadaiwa kuwa ni wa maandalizi ya kampeni za kuwania kiti cha udiwani wa Kata ya Kirumba ambacho kipo wazi baada ya diwani wake, Novatus Manoko (Chadema) kufariki dunia
 
Udiwani waache tu. Hilo jiji ni la CDM. Hata waweke jiwe na Gamba, jiwe litashinda tu
 
Nape na magamba menzake yanazidi kuwaongyesha watz ni kwa namna gani siasa zimewashinda na sasa wanasambaza vurugu. Kama chama tawala kinafanya hivi ni dalili tosha kwamba kimeishiwa sera na inabidi kikae pembeni.
Hongera wanachi wa Mwanza! Hiyo ilikuwa salamu tu kwa CCM kwamba hawatakiwi katika nchi hii.
Bye-bye CCM, mjiandae kuwa chama pinzani!
 
Uongo mtupu...angalieni marudio ya Taarifa ya habari ya Star TV kesho asubuhi mtaona...anasingizia eti mimi nilikatisha hotuba yangu wakati niliongea dakika zote nilizokuwa nimepangiwa!

Vijana wa CDM waliokuwepo pale ni wachache sana, kama 15 hivi ukilinganisha na wengi wenye hekima na busara waliokuwa wametulia na kufuatilia hotuba zetu.

WanaJF hebu jiulizeni kitu hapa, kama watu wa CDM walikuwa wengi kushinda wa CCM na walikuwa wanazomea na greenguards wakaenda wakamkamata mfanya fujo mmoja, CDM si wangeleta vurugu mbaya kabisa, pengine hata mauaji? Iliwezekana vipi CCM kuendesha mkutano wake vizuri na kwa amani na utulivu kabisa mpaka mwisho kama kweli kulikuwa na fujo za kiasi kilichoelezewa namna hii?

Waandishi ni mhimili wa nne wa dola, fanyeni kazi yenu kwa ufanisi na kimaadili. Nchi yetu sote basi tuilinde!
 
Kwahiyo mkuu mikutano yenu inalindwa siku hizi na kila anayebisha au kutokukubaliana na nyie anapata kipigo toka kwa greenguards au hata watu wakishangilia pia wanakamatwa...

Enzi za nguvu ya hoja zimekwenda wapi mkuu...?, au hiki ni kipindi cha Yes Sir, Ndio Mzee na Kutumia Mabavu..?, kama kweli mnakubalika greenguards wa nini si wananchi wenyewe wangemyamazisha mfanya fujo ili wasikie points ?

Acheni hizo Bana..!!!
 
Mhhhh! Magamba wameamua kuwatisha Watanzania, Arusha na Tarime kulikuwa na vipigo na risasi za moto na baadhi kupoteza maisha yao, Dar vipigo vilitembezwa na manjagu waliovaa kiraia walionekana wakiwa na bunduki tayari kufanya vitu vyao na sasa yametokea tena Mwanza.

Huko tunakoelekea si kwema kabisa.
 
Uongo mtupu...angalieni marudio ya Taarifa ya habari ya Star TV kesho asubuhi mtaona...anasingizia eti mimi nilikatisha hotuba yangu wakati niliongea dakika zote nilizokuwa nimepangiwa!

Vijana wa CDM waliokuwepo pale ni wachache sana, kama 15 hivi ukilinganisha na wengi wenye hekima na busara waliokuwa wametulia na kufuatilia hotuba zetu.

WanaJF hebu jiulizeni kitu hapa, kama watu wa CDM walikuwa wengi kushinda wa CCM na walikuwa wanazomea na greenguards wakaenda wakamkamata mfanya fujo mmoja, CDM si wangeleta vurugu mbaya kabisa, pengine hata mauaji? Iliwezekana vipi CCM kuendesha mkutano wake vizuri na kwa amani na utulivu kabisa mpaka mwisho kama kweli kulikuwa na fujo za kiasi kilichoelezewa namna hii?

Waandishi ni mhimili wa nne wa dola, fanyeni kazi yenu kwa ufanisi na kimaadili. Nchi yetu sote basi tuilinde!
Nyinyi CCM mchezo wenu ni mauti yenu. Hawa wahuni mnaowatumia mnawaita Green Guard, watatupeleka kusiko, so far ninyi ndo mnaopambana kuipeleka nchi kwenye uvunjifu wa amani ingawa mnajifanya mahodari wa kuhubiri amani. Mmeona siasa za hoja zimewashinda,sasa mneamua kutumia mabavu, hamuwezi kushindana na nguvu ya umma, kama kashindwa Gadaffi nani Africa hii ataweza kudhibiti nguvu ya umma??hamjui moto mnaouwasha. Mtakao pata hasara katika tafrani mnalolianzisha ni nyinyi wenzetu wenye mali, sisi nyumba zetu za nyasi na vumbi hata mkizichoma mvua itanyesha nyasi zitaota, tutakata tutaezeka mwendo mdundo. nyie tuchokoeni tu, hamjui ni chuki kiasi gani mmetujengea na hilo chama lenu la mafisadi.
 
uongo mtupu...angalieni marudio ya taarifa ya habari ya star tv kesho asubuhi mtaona...anasingizia eti mimi nilikatisha hotuba yangu wakati niliongea dakika zote nilizokuwa nimepangiwa!

Vijana wa cdm waliokuwepo pale ni wachache sana, kama 15 hivi ukilinganisha na wengi wenye hekima na busara waliokuwa wametulia na kufuatilia hotuba zetu.

Wanajf hebu jiulizeni kitu hapa, kama watu wa cdm walikuwa wengi kushinda wa ccm na walikuwa wanazomea na greenguards wakaenda wakamkamata mfanya fujo mmoja, cdm si wangeleta vurugu mbaya kabisa, pengine hata mauaji? Iliwezekana vipi ccm kuendesha mkutano wake vizuri na kwa amani na utulivu kabisa mpaka mwisho kama kweli kulikuwa na fujo za kiasi kilichoelezewa namna hii?

Waandishi ni mhimili wa nne wa dola, fanyeni kazi yenu kwa ufanisi na kimaadili. Nchi yetu sote basi tuilinde!
kaka nina mambo machache naomba unijibu kuhusiana na hiyo sehemu niliyo weka nyekundu

1. Vipi ni halali kwa kila chama kuwa najeshi lake kama hivi mnavyofanya na kuwapeleka makambini kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi au ni ruksa kwa ccm tu?

2. Je vijana hawa hulipwa kiasi gani na nani na kwa kufungu lipi au wanajitolea tu kwa mapenzi waliyonayo katika chama chao?

3. Vipi mkuu vijana hawa khali yao kimaisha ikoje wapo angalau wanaomiliki walau nyumba moja ya kisasa au hapana?

4. Mkuu nijuze kuhusu elimu ya vijana wetu hawa kwa wastani elimu yao ni ya kiwango gani ?naomba unijibu hili niweze kuwafahamu kwa kina hawa vijana

mkuu ukiwa kiongozi na ukategemea walinzi na bastola pale unapoenda kuonana na wale unaowaongoza wewe si kiongozi .
 
Kwahiyo mkuu mikutano yenu inalindwa siku hizi na kila anayebisha au kutokukubaliana na nyie anapata kipigo toka kwa greenguards au hata watu wakishangilia pia wanakamatwa...

Enzi za nguvu ya hoja zimekwenda wapi mkuu...?, au hiki ni kipindi cha Yes Sir, Ndio Mzee na Kutumia Mabavu..?, kama kweli mnakubalika greenguards wa nini si wananchi wenyewe wangemyamazisha mfanya fujo ili wasikie points ?

Acheni hizo Bana..!!!

Siyo kuwapa mkong'oto tu , bali ni pamoja na kuwaua na kuwapoteza mtawaona baada ya week mbili wakiwa vichakani!!! hicho ndicho chama cha majambazi orijino
 
Haya maswali yanapaswa kujibiwa tafadhali,
kaka nina mambo machache naomba unijibu kuhusiana na hiyo sehemu niliyo weka nyekundu

1. Vipi ni halali kwa kila chama kuwa najeshi lake kama hivi mnavyofanya na kuwapeleka makambini kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi au ni ruksa kwa ccm tu?

2. Je vijana hawa hulipwa kiasi gani na nani na kwa kufungu lipi au wanajitolea tu kwa mapenzi waliyonayo katika chama chao?

3. Vipi mkuu vijana hawa khali yao kimaisha ikoje wapo angalau wanaomiliki walau nyumba moja ya kisasa au hapana?

4. Mkuu nijuze kuhusu elimu ya vijana wetu hawa kwa wastani elimu yao ni ya kiwango gani ?naomba unijibu hili niweze kuwafahamu kwa kina hawa vijana

mkuu ukiwa kiongozi na ukategemea walinzi na bastola pale unapoenda kuonana na wale unaowaongoza wewe si kiongozi .
 
mimi pia nina maswali

Je green guards wana 'guard' nini?
wanatumia strategies zipi kufanya hiyo kazi ya ku guard?
Je wana mamlaka au haki yoyote kisheria ya matumizi ya nguvu katika kutuliza vurugu kwenye mikutano?
 
Wakazi kiduuchu waliohudhuria mkutano wa hadhara katika viwanja vya MAGOMENI jijini Mwanza ulio andaliwa na CCM chini ya katibu mwenezi NAPE akiwa na lengo la kueleza sera ya chama hicho juu ya kujivua GAMBA,,WAMESHUHUDIA RUNDO LA MATUSI YA NGUONI KUTOKA KWA MAKADA HAO.

Ushauri wa bure kwa ccm,NAPE hawezi siasa bora wampost kwenye bendi yao ya TOT akawape burudani ya Taarabu,,ilibidi baadhi ya watu waanze kujisogeza na kuondoka,wengine waanze kunong"ona wakimshangaa baba huyu.kama vile haitoshi ilibidi baadhi ya vijana kwa kuchoshwa na upuuzi huo waanze kumjibu poale alipouliza maswali ya kipuuzi mfano;Nani alishawahi kuwaona viongozi wa CDM wakidhurika ktk

maandamano?JIBU Likapatikana wadau wakijibu...arushaaaaaaaaa,DK.SLAAAAAAA....AKAUDHIKA AKAANZA KUYAPOROMOSHA
1.WANAUME LAKINI OVYOOOOO
2.YAONE YANAWASHWAAAAAA
3.ANAE WASHWA ASHIKE UKUTA AONE VIDUME....
Namengine mengi ya aibu,,
USHAURI....CCM mkiendelea kumtumia NAPE asie na SOCIOL ETHICS mtazidi kujiaribia ila kwa MWANZA LEO MMECHEMKA NA BWANA HUYO SIDHANI KAMA ATARUDI TENA MWANZA,,,,,
THANKS,NAWASILISHA
mama yangu wee! walahi siamini kama macho yangu yanaona vema kilichoandikwa hapo kwenye nyekundu.
 
Hii ni aina (style) mpya ya siasa za Tanzania? Mtu unaweza kuona JF na social networks nyingine ukachukulia kuwa ni utani vile, kumbe ndicho kinachoendelea on ground?

Basi tunakoelekea kufikia 2015 iko kazi, tutarajie vituko zaidi ya sasa.
 
Ukisikiliza hawa viongozi wetu (baadhi) unaona bora uendelee kupigana pembeni kwa nguvu ili kuwapumzisha, sijui ndo kulewa pesa zetu za kodi au ndo kujiona wako juu ya jamii. Maana halisi ya uongozi siku hizi haipo tena kwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM.
 
hivi kwa nini Nape anachukuiwa hapa JF sijwahi ona any positive post yake.kulikoni?

mimi sijasoma post zote zinazo muhusu huyu kiongozi
yupo humu labda um pm umuulize kwa nini hana positive post
ila kama unamaanisha hujawahi kuona any positive post iliiyoelekezwa kwake basi hiyo hatari maana humu mashabiki wa CCM pia wapo, ningetegemea kuona angalau mmoja wao anamsapoti

vinginevyo, kiongozi wa CCM kuchukiwa mi naona ni jambo la kawaida kabisa, mtu wa kawaida anayekufa kwenye lindi la umaskini yeye na wanawe, hawezi kumpenda "kiongozi" wake aliyemwacha mbali sana kimaisha.
 
CCM; from the towers of grace and Tanzanians' absolute loyalty to grass and a chorus of condemnation from all directions. What is it that may have significantly gone wrong somewhere in-between anyway??????
 
Back
Top Bottom