Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Umenena vyema sana!!!! Nakuongezea wengine, na W/nzi wa shule za secondari nao walikuwapo [Read between lines].

Jenga hoja zenye mshiko.Acha kudhihaki watu.Umewaona Udom tu?,mipango;St John na CBE nao walienda kumshawishi EL kama Jk alivyoagiza akiwa Songea.
 
Tatizo la Watu ambao wanamamlaka CCM a.k Chama Cha Majungu, wanazani CCM ni mali yao na wanahati miliki ya CCM. Endeleeni na majungu tu, ndiyo mwisho wa CCM huo! Lowassa mnacheza naye tu; Mtakuja jutia kwann mlimnyanyasa kiasi hiki? Lowassa ni mpango mzima, CCM, inakwenda kukatika vipande viwili na ndiyo hapo yatakapo timia maneno ya Mwalimu J.k.Nyerere" Upinzani wa kweli utatokea pale CCM, itakapo katika vipande viwili!".
 
Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Kinavhofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anawezakuondolewa," alisema Nape.

CCM wakimteua mtu mwenye tamaa na mlafi wa aina hii itakuwa ni aibu sana. Bora wamfukeze ...ngoja tuone kama CCM wana guts kama waliyokuwanayo CDM kwa Zitto!
 
Mkuu tpaul unadhani laigwanan atatinga Magogoni? Asilani! Kila kukicha anafurunda kwa kampeni zake.
 
Kuna wakati Mrema alijiona atakuwa raisi baada ya Mzee Mwinyi kumaliza muda wake,na hata alipohamia chama kipya NCCR Mageuzi alibebwa na hata gari lake lilisukumwa kila sehemu aliyokuwa naenda kuhutubia,mikutano ikajaa nyomi na Mrema akajidanganya kuwa atauchukua uraisi,na sote tunajua yaliyotokea .Tusubiri tsunami itakavyowapata wale wanaojiona wana miliki ya kuwa raisi hadi wanajidanganya wenyewe.Hayo mabilioni ya watu sijui yatafidiwa na nini.
 
Nape ni mpuuzi mwezi jana alisema CCM haiwezi kumpitisha mgombea wa kuosha na dodoki,leo anasema Lowasa yuko hatarini kuwnguliwa kwa kuanza kampeni mapema sasa unajiuliza kumbe sababu yenu na akina membe yakutaka lowassa akatwe jina ni nini

1 Ni msihangaike na madodoki?
2 au Ameanza kampeni mapema

fuuuuuumbafu hatudanganyiki mziki huu hamtaweza kuucheZa Lowasa ni chaguo la watanzania na bidhaa inayouzika sokoni
 
Kuna wakati Mrema alijiona atakuwa raisi baada ya Mzee Mwinyi kumaliza muda wake,na hata alipohamia chama kipya NCCR Mageuzi alibebwa na hata gari lake lilisukumwa kila sehemu aliyokuwa naenda kuhutubia,mikutano ikajaa nyomi na Mrema akajidanganya kuwa atauchukua uraisi,na sote tunajua yaliyotokea .Tusubiri tsunami itakavyowapata wale wanaojiona wana miliki ya kuwa raisi hadi wanajidanganya wenyewe.Hayo mabilioni ya watu sijui yatafidiwa na nini.
We jidanganye hujui ya ndani mrema hakua chochote kumlilinganisha na Lowassa huyu amepenya kwenye system zote ambazo ccm wakichemsha kumkata jina wamekwenda na maji unajua hella mrema ambaye hata jeshini walikua hawamjui
 
Mbona mnatishia chama kikongwe barani Africa na chenye azina kubwa ya wagombea? Mtu nmoja anaweza kuua taasisi kama ccm?
 
Attachments

  • 1427234115200.jpg
    1427234115200.jpg
    38.4 KB · Views: 224
Maneno yako yanaukweli lakini Lowassa hatalipa kisasi amekomaa Mungu akimjalia atawapuuza tuu

EL n MTU Wa visasi Sana na ndiye aliyhakikisha wote ambao hawakuunga mkono mtandao wao 2005 wanatupiliwa mbali....

Namwonea huruma Nappe anapotumia dhamana aliyonayo kupigania mambo binafsi.....
 
Hivi Nape anadhani Lowassa ni Juliana Shonza? Kashindwa kumvua gamba atamuweza sasa hivi wakati "Ameshawishiwa naye kashawishika?" Lowassa ndio kete kuu ya upinzani katika kukivuruga chama chao ili wapenye kwa urahisi.
Wahenga walisema adui mwombee njaa, na njaa ya upinzani ni kuona hili dude komavu linaloitwa ccm linajikata lenyewe miguu,kichwa na nyonga kabla ya kupambana nalo October
 
Last edited by a moderator:
Jamii forums na nyie mnaenda lini kumshawishi?

Mzee wa mamvi alete tuu mshiko kama 10M za kumchangia yeye mwenyewe tutampelekea kwa maandamano. Ila mimi ndio niwe mweka hazina. Hawa wakina Invisible wao wabaki ofisini kuendeleza majukumu ya JF mie nitawatoa baadae.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom