Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

- Sawa sawa wala haina majadiliano, Bravo Nape!

Willie @ NYC, USA.
Baba yako John na Mama yako Anne wameshindwa kuzuia mgao wa umeme na wala kuleta mawazo mbadala kumaliza mgao. The Losers Family... Umeishajichagulia upande unaoona utakufaa kuja kutafuta madaraka ya bwelele ili uendeleze imani mbovu ya nyie watoto wa wakoloni weusi kuwa bila uongozi huwezi kuishi. Mitaji mnayo kwa nini msianzishe biashara tu angalau mtatoa ajira. Mbona Fisadi Lowasa watoto wake wanapiga biashara na wameajiri wabongo kibao, nyie mnataka kuja kuendeleza ukoloni... Nyambafu...
 
Kama Nape ndio tegemeo la CCM basi muda sio mrefu tutapata habari nzito. Wapo watakaofurahia ila wengi watahuzunika!
 
- Sawa sawa wala haina majadiliano, Bravo Nape!Willie @ NYC, USA.
Nimeshakusoma mkuu kwamba uko kinyume na EL.Kwa sababu nape yupo kambi ya upinzani kwa EL so ni haki yako kumpongeza mwenzako.Siku za ccm kutawala si nyingi,kumbekeni vyama vilivyopigania uhuru katka nchi kadhaa za africa leo ni vyama pinzani.Nyie sijui mmebatizwa kwa jina la magamba? why dont u be realistic n honest like madaraka nyerere.Yule jamaa nampenda kwa sababu huwa anatetea ukweli pasipo kujali kuwa baba yake alikuwa mwanzilishi wa ccm.Mi nakuchoka sana mkuu kwa sababu umeshawahi kuandika kwamba ukitaka kupata habari kwa mtu lazma uwe kinyume chake.Sijui labda hata sasa una2enjoy tu
 
We have to give him more time to demonstrate his tallent and political power
 
- Sawa sawa wala haina majadiliano, Bravo Nape!

Willie @ NYC, USA.

Kaka Willlie,
Jana nilimsikiliza Nape mwanzo mwisho, nimegunda CCM imechoka sana, ni kwanini wasijitokeze watu wanaoweza kujenga hoja ya karne hii, kwanini CCM inategemea watu wa kaliba ya Nape, Makamba babu, Hiza Tabwe, sofia Simba, ? Hawa sehemu yao nzuri ni kikundi cha taarabu. Mifano mingi aliyoyatoa jana ni ya ngono tu kuhusu CCM,

Nafikiri CCM wanashindwa kutambua nyakati, angalia bunge wabunge toka CCM ni usingizi tu, leo Chibulunje kawekwa page ya kwanza ya gazeti la mwananchi kapiga usingizi mzito.
 
anakula per diem za chama tu. Ni sawa na kujjaza maji kwenye ndoo inayovuja. Wananchi hawakichukii ccm bali wanachukia matokeo mabaya katika taifa yaletwayo na ccm. Ziara za nape zitakuwa na positive impact once government perfomace meet citizens expectations. Otherwisw narudia tena, nape anakula posho za safari tu

- Kazi yake ni uenezi wa Itikadi ya chama, ndio maana ni lazima asafiri sana ni fact of life zaidi kuliko siasa!

Willie @ NYC, USA.
 
Malecela,umewah kuona nape akihutubia????huwa anawahutubia wanafunz tena wa shule za msingi,sasa hawa watoto kwanini watolewe shule wamsikilize NNAUYE????,

- JF huwa tuna tabia moja kuwajadili viongozi tunaowapenda tu, regardless ya kazi zao kwa taifa so! Nape is great, jamani give the guy a credit I mean CCM sasa imasimama tena baada ya almost kufa kwa muda mrefu sana!

Willie @ NYC, USA.
 
Baba yako John na Mama yako Anne wameshindwa kuzuia mgao wa umeme na wala kuleta mawazo mbadala kumaliza mgao. The Losers Family... Umeishajichagulia upande unaoona utakufaa kuja kutafuta madaraka ya bwelele ili uendeleze imani mbovu ya nyie watoto wa wakoloni weusi kuwa bila uongozi huwezi kuishi. Mitaji mnayo kwa nini msianzishe biashara tu angalau mtatoa ajira. Mbona Fisadi Lowasa watoto wake wanapiga biashara na wameajiri wabongo kibao, nyie mnataka kuja kuendeleza ukoloni... Nyambafu...

- Hii imenivunja sana mbaavu! ha! ha! ha! ha! ha! ha! ha!

Willie @ NYc, USA.
 
Siku nyingi sijamsikikia kada wa CCM Hiza Tambwe. Anayesikika sasa ni Nape Nauye. Hiza yuko wapi ? Kachukia Nape kupewa nafasi ya kuwa msemaji wa chama? Mara nyingi najiuliza kama kuna tofauti kati ya Nape na Hiza. Tofauti zao ni katika umri, wasilishaji wao wa hoja, Nape huwa hupayuka sana wakati Hiza ni mtaratibu asiyejali hoja toka upinzani. Nape anapambana na wanaccm wenzake wakati Hiza anatetea ccm kwa gharama zote hata za propaganda. Wanalenga zaidi kwenye maslahi binafsi huko ndiko kufanana kwao.
 
Kabla ya Nape sijawahi kukisikia sana cheo chake hiki, wakati huo mtu maarufu kwenye chama ukiacha JK alikuwa ni Makamba, Lakini kwa sasa ni kama vile Mukama hayupo na Nguzo na tegemeo kubwa la CCM sasa limebaki kwa Nape, ndiye mwenye uthubutu wa kwenda kilimanjaro, Arusha na Mbeya. Kijana atakumbukwa sana huyu

Nepi anasikika na watu wa magamba tu.

sisi wengine tunaendelea kusikia harufu ileile ya ccm ambayo haina tofauti na harufu ya choo cha passport-size kipindi cha mvua za masika.
 
Jana alipokuwa ana hutubia watu maeneo ya stendi hapa Moshi mjini alitoa kauli zenye maudhi ndani yake na labda bila kujua kuwa kauli zake zina ukakasi alizidi kukandamiza lawama kwa vyama vipinzani huku akishindwa kuona ukweli na uhalisia wa mambo.

Nape alisema Tanzania kuna zaidi ya vyama 17 vya siasa lakini kuna chama kimoja tu kilicho beba matumaini ya watanzania. Chama hicho ni CCM na vyama vingine ni vyama vya WALALAMIKAJI, lakini akiwa anasema hayo mji wa Moshi hasa karibu na eneo alilo kuwa anahutubia palikuwa pametawalia na kelele za majenerata, hapa ndio nashindwa kumuelewa Nape! Hivi wana JF wanao lalamikia umeme nao ni wa vyama pinzani tu! Mbona wabunge wa CCM Wameungana na upinzani kukwamisha bajeti ya Ngeleja? Na wabunge wale nao atawaitaje maana nao walilalamika.

Wizi ulio ibuliwa na vyama pinzani hasa CDM nao ulikuwa ni aina ya malalamiko ambayo Nape anataka kuaminisha kuwa Cdm ni chama cha walalamikaji? Mbona Kina Sita nao ndani ya CCM wanalalamika kuwa kuna watu wanaifilisi nchi kwa biashara zao za kitapeli, je nao ni aina ya walalamikaji wa CCJ na sio CCM?!
Mbona JK nae alisha wahi kulalamika kuwa CDM wanataka kumng'oa madarakani kwa maandamano, vipi nae ni aina ya viongozi wa vyama vya ulalamikaji?!

Una mapungufu ya kimantiki Nape. Rudi darasani ukaketi upya.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hivi nape bado anatumia hela ya wizi ya EPA aliyopewa na jeetu patel agombee uenyekiti uvccm??kumbe NAPE NI FISADI....
 
<strong><font size="4"><span style="color:#0000ff;">tatizo lake anaparamia watu wasio size yake kiumri na kisiasa</span></font></strong>
 
Baba yako John na Mama yako Anne wameshindwa kuzuia mgao wa umeme na wala kuleta mawazo mbadala kumaliza mgao. The Losers Family... Umeishajichagulia upande unaoona utakufaa kuja kutafuta madaraka ya bwelele ili uendeleze imani mbovu ya nyie watoto wa wakoloni weusi kuwa bila uongozi huwezi kuishi. Mitaji mnayo kwa nini msianzishe biashara tu angalau mtatoa ajira. Mbona Fisadi Lowasa watoto wake wanapiga biashara na wameajiri wabongo kibao, nyie mnataka kuja kuendeleza ukoloni... Nyambafu...

Hii ni kukosa hoja.
 
Kulia lia hakutasaidia kitu, ccm wajibu hoja. Si walitaka uongozi wenyewe, tena wakachakachua,sasa jibuni hoja.
 
nape hana kitu cha maana zaidi ya kulinda mshahara wake tu,kwa nini alikuwa anataka kujitoa ccm na kwenda ccj? Anajua kabisa kuwa ana pretend kuwa ndani ya ccm
 
Back
Top Bottom