Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

RITZ; Hapo ndipo nashangaa kwa nini kila siku anazidi kuwapoteza CDM pamoja na wasomi wake wote nguvu ya umma! Kaenda mpaka moshi, Arusha, hii ya moshi na Arusha ndio nimeshangaa nilitegemea kuona wazee wanachukuwa kadi za magamba kumbe ata vijana wa kichagga bado wanaipenda magamba wanaminika kwa wingi kuchukuwa kadi tena ni Wasomi!

Jana nilikuwepo Masoka (Tumaini university); vijana waliokuwepo ni wana vyuo vya KCMC, Mwenge, na Masoka ambao ni wana CCM wanaotokea mikoa ya Tabora,Tanga na hakuna mwenye akili timamu aliyechukua kadi kwa Nape. Huku kasikazini ccm haipo, watu wamekereka na tatizo la umeme.
 
Nape anafaa kupongezwa.Ni kijana ambaye anaonesha ukomavu wa kisiasa na ameweza kwa kiasi kikubwa sana kurudisha matumaini ya watanzania waliowengi kwa CCM.Haendeshwi kwa itikadi bali anawatetea watanzania wote masikini wa nchi hii.Viva Nape.
Ungekuwepo jana hapa Moshi usingethubutu kusema hayo!Nape ni mtu wa majungu,mnafiki,mwanzilishi wa CCJ!jana kaongea pumba mpaka nikamkumbuka hata babu mropokaji Makamba!yani badala ya kueleza namna ya kutatua matatizo!mipasho na majungu ndiyo vilitawala hasa kwa hao wanaCCM Mahasimu wake!mpaka vijana wakaanza kumzomea wakisema..."hatutaki majungu tunataka umeme.."nikamwona kama anapotezea ila baada ya dk 5 hivi akashuka jukwaan maana angeendelea yangemtokea ya kumtokea!NAPE ACHA MAJUNGU UNABOMOA CHAMA CHAKO a.k.aCHAMA CHA MAJUNGU!
 
Jaman nadhan mnajua kuwa nape anafanya kazi ya PROPAGANDA,Sasa kila analofanya lazima lioneshe +ve image ya chama kwa jamii,unadhan wataacha kuonyesha watu waliochukua kadi????utajuaje kama walipewa hata buku 5 5 kwa ajili ya wao kupokea kadi,na pia mjue ukiwa na kadi ya ccm wakat wa kura za maoni kwa ccm,wapiga kura ndani ya chama hupata pesa kwa kadi zao,hankuona watu walivyokuwa wakipewa bahasha???hamkuona kadi zilivyokuwa dili at that tym??????mi sishangai saana,hapo anaweza akaenda kiongoz wa chama kingine wakapokea KADI
 
msomi yupi mwenye akili za kisomi anaweza chukua kadi ya gamba??labda Kama hana uellewa wa kuchambua Mambo ndo anaweza yumbishwa na wanasiasa uchwara Kama alivyosema RA. Jana nlikuwepo mkutanoni moshi stand kuu. Kuna hoja ya sababu za kupanda Kwa gharama za mafuta aliichambua kibabaishaji na wananchi wenye uelewa finyu wa Mambo walifurahi Kweli. Nkajua CCM inatuongoza kwa vile tu wananchi walio wengine wanauelewa funyi wa Mambo yanayotuzunguka. Ila tukipata ufahamu wa mambo. Chama Kama CCM kuongoza watu itakuwa ni Ndoto. Ccm endeleeni kuneemeka Kwa kutumia ujinga wa watanzania....
 
kakushika ww pabaya.!!! ule umati wa primary jana ndo mnaona mmepata.!? subilini kitu cha igunga uone tunavyojichukulia jimbo

Basi namsaidia jenifa, Nape kawashika pazuri kama pabaya hampataki au unasemaje? au sio Junior?
 
Nape hana lolote,pia acha uzushi, kwenye mkutano Moshi nilikuwapo..hakuna umati wa watu, na sijawahi kuona watu wachache kiasi hicho katika shughuli za kisiasa hapa Moashi toka 1995! Dont exaggerate
Ndakilawe natamani tungeonana jana pale stendi maana hata mi nilishangaa iweje katibu mwenezi tena stendi awe na watu wachache kiasi kile!
 
Hapo ndipo nashangaa kwa nini kila siku anazidi kuwapoteza CDM pamoja na wasomi wake wote nguvu ya umma! Kaenda mpaka moshi, Arusha, hii ya moshi na Arusha ndio nimeshangaa nilitegemea kuona wazee wanachukuwa kadi za magamba kumbe ata vijana wa kichagga bado wanaipenda magamba wanaminika kwa wingi kuchukuwa kadi tena ni Wasomi!

Si wamesha ona joto la magwanda!
 
Nape anafaa kupongezwa.Ni kijana ambaye anaonesha ukomavu wa kisiasa na ameweza kwa kiasi kikubwa sana kurudisha matumaini ya watanzania waliowengi kwa CCM.Haendeshwi kwa itikadi bali anawatetea watanzania wote masikini wa nchi hii.Viva Nape.
Akishawatetea hao masikini nini kinaendelea? Je anafanya jitihada zipi kuhakikisha huo umasikini unakwisha au unapungua? Umaskini unamalizwa na kelele za majukwaani? Wacha wewe kajipange upaya kumtetea huyo mme wako.
 
hao ndo wanasiasa uchwara bro, usibishane nao, utamaliza maji kumuosha nyani kiganja, weusi ndo rangi yake
 
Kabla ya Nape sijawahi kukisikia sana cheo chake hiki, wakati huo mtu maarufu kwenye chama ukiacha JK alikuwa ni Makamba, Lakini kwa sasa ni kama vile Mukama hayupo na Nguzo na tegemeo kubwa la CCM sasa limebaki kwa Nape, ndiye mwenye uthubutu wa kwenda kilimanjaro, Arusha na Mbeya. Kijana atakumbukwa sana huyu

Inaonekana ni shwahiba wako,mimi ninaona katika watu waliopotea CCM ni kumpa nape hiyo kazi,ni mropokaji mfano, anadai CDM ni Cha wachaga sasa anafanya nini Moshi?mropokaji siku zote hana muda wa kufanya utafiti na nicho kitakacho mgharimu huyu kijana.Mukama ni kiongozi mzuri huwezi kumlinganisha na Nape hata siku moja.
 
Nape mbona ni kafala yule as si unajua lengo la JK anataka amtibue EL ambaye walishatibuana toka jengo la vijana pale dsm EL alipokula parefu
 
kuna mambo ya kujipongeza,mtoa mada ungetakiwa uumpe pole NEPI,kwa sababu zifuatazo

1:anajenga hoja za kuwadanganya watanzania ili waamini CCM Haijaishiwa hoja.

2.anajenga hoja za chuki dhidi ya chama cha CHADEMA ili watu wapuuze UKWELI unaotangazwa na chama cha Democrasia na maendeleo.

3.anatatua matatizo ya ya chama chake kwa siasa nyepesi zenye uwongo na zinazolenga kukisafisha chama.

4.Anatumia Vuvuzelaism kukisafisha chama,anafumba masikio kwa mambo yawazi yanalolikabili taifa hili ili mradi tu amfurahishe bosi wake.

Kuna mengi anayoyafanya ila swala la kujivua gamba ndo kifo cha C cm.
Nape ni bomu kali kuliko Makamba.
 
Nape anajiita msemaji wa Serikali, lakini badala ya kuelezea umma wa watanzania mustakabali wa nchi yao ambayo kimsingi ipo ktk "auto pilot"! Anatumia muda mwingi kusengenya wapinzani badala ya kuongea Sensible issues Kwa mustakabali wa taifa letu, Kweli nchi Sasa wamekabidhiwa wahuni... Lugha anayotumia hakika siyo ya mtu wa kuisemea Serikali, Kwann hawajifunzi huko wanakotafuta wawekezaji????
 
Nimefungua thread hii haraka sana nione unavyomsifia na unatumia vigezo gani..Baada ya kukusoma nimevuta pumzi.Nimekuelewa na tuko pamoja
 
Mimi naona Nape anatumia nguvu nyingi ambapo baada ya mwaka ukimwambia aevaluate impact anajikuta workdone is closely and approximately to 0.00000000099
Mbona unampendelea namna hiyo?workdone = -ve 'infinity'
 
NAPE acha kutapatapa wewe umeshika makali walioshika mpini wanakucheki kwenye site mirror.you are looser man.think about joining CDM ili uwe diwani ktk kata moja huko kasulu.
 
Nimefungua thread hii haraka sana nione unavyomsifia na unatumia vigezo gani..Baada ya kukusoma nimevuta pumzi.Nimekuelewa na tuko pamoja

Afadhali kama umenielwa mkuu, wako wanaodhani Nape anafanya kazi nzuri kwa taifa lakini kimsingi hata ndani ya chama anafanya kazi kwa niaba ya kambi moja, ipo siku atajuta kuzaliwa siku anaowafanyia kazi watakapoachia uasukani, sijui atakimbilia wapi.

Bifu lake na EL ni la tangu enzi za kugombea kwake uenyekiti wa UVCCM na anazidi kulikuza, wahenga wanasema adhaniye amesimama aangalie asianguke, watch out Nape
 
nape na watoto.jpgnape na watoto.jpg
Malecela,umewah kuona nape akihutubia????huwa anawahutubia wanafunz tena wa shule za msingi,sasa hawa watoto kwanini watolewe shule wamsikilize NNAUYE????,
 
kuna mambo ya kujipongeza,mtoa mada ungetakiwa uumpe pole NEPI,kwa sababu zifuatazo

1:anajenga hoja za kuwadanganya watanzania ili waamini CCM Haijaishiwa hoja.

2.anajenga hoja za chuki dhidi ya chama cha CHADEMA ili watu wapuuze UKWELI unaotangazwa na chama cha Democrasia na maendeleo.

3.anatatua matatizo ya ya chama chake kwa siasa nyepesi zenye uwongo na zinazolenga kukisafisha chama.

4.Anatumia Vuvuzelaism kukisafisha chama,anafumba masikio kwa mambo yawazi yanalolikabili taifa hili ili mradi tu amfurahishe bosi wake.

Kuna mengi anayoyafanya ila swala la kujivua gamba ndo kifo cha C cm.
Nape ni bomu kali kuliko Makamba.

Kila mwenye upendo wa kweli na wa dhati kwa binadamu wenzie nadhani hatapingana na maneno yako.Nachukia sana dhana ya kutumia advantage ya watu wajinga kuzidi kuwaumiza kwa kujifanya eti msafi ,ilhali moyoni unajisuta jinsi gani ulivo nyoka
 
Back
Top Bottom