Nape, 'Kujivua Gamba' ni danganya toto??

Nape,
Wakati naanza kukufahamu nilijua ni kijana ambaye siasa zako zingejinadi zenyewe bila nguvu ya ziada. Nikaamini pia hata viongozi mashuhuri na mafisadi wameanza kuhofia baadae yako. Ndio, kulikuwa na sura ya kipaji, wengi watakiri hivyo. Hofu ya viongozi na mafisadi ndio iliyofanya wakupe hicho walichokupa sasa na kukupa "majukumu chuki". Wao wanafahamu ya kuwa mtaji wa kisiasa ni zaidi ya pesa. Na walifahamu kuwa wasipokupa majukumu ovyo, tena yanayokuaribia mwisho watoto wao ambao ndio warithi watapata upinzani. Mi nadhani unajidhoofisha bila kujua. Unahitaji kujisafisha sana, kurudisha imani kwa watanzania. Acha hawa wazee wapite.
Mwisho, nimeamini cheo ulevi! kila kitu wewe ni jazba, hujengi hoja, angalia ulivojibu hoja hapo juu. We ni kiongozi kijana, safari bado ni ndefu, tafakari-chukua hatua!
Nova,

Kwamba naimba wimbo wa mtu, kwanza afadhali umepiga hatua wewe na mafisadi waliokutuma kusema ni wimbo wa Kikwete very soon, nasema very soon MTAKIRI KUMBE NI WIMBO WA CHAMA AMBACHO MIE NDIO MSEMAJI WAKE....

Mlipoanza mlisema kuwa ni wimbo wa Nape na Chiligati, kwa hiyo hatua uliofikia wewe na wenzako na hasa baada ya kuambiwa Mwanza tuliamua kwenye kikao, ni nzuri sana maana hata shule unaanza darasa la kwanza then unaendelea, kazana ukikua utasema vizuri na kwa usahihi zaidi.
 
matusi kwa kiongozi mwnye dhamana kama wewe hayajengi,wewe ulikuwa rafiki yangu sana tumefanya mambo mengi sn pamoja ingawa kwa sasa kimtazamo haupo na mimi,sikubaliani na style yako ya kazi,tofauti yako na mwenyekiti wako ni kuwa angalau wewe unaongea,lkn kmisingi hoja zenu zenu za kukurupuka,lakini style yenu ya kazi ni zima moto,sera yenu ya kujivua gamba ili fail kabla haijaanza niliwahi kukuonya kwenye hili ukanimwagia matusi ukasema napakatwa na mafisadi,nimehongwa na mafisadi,hii vita ya ufisadi ilipoanza wengine tulifurah na kuunga mkono kuwa angalau raslimali za nchi zitatunufaisha wote,badala yake hoja ikawa ya mtu mmoja[lowssa],lowassa hawezi kuwa fiasadi kikwete akawa salama tuna ushahidi wa pesa ritz 1 alizonazo na hata leo akiulizwa kapataje hawez elezea,sitta,msekwa,membe,ngeleja na wengine wengi ndani ya ccm ni mafisadi ,tatizo lako wewe na kikwete mnapenda sifa hampendi mawazo ya watu wengine,mnabaki mnapiga kelele za hovyo,hela za EPA ndo zilizomwingiza kikwete madarakni alafu leo unasimama jukwani unasema kikwete msafi,kwa taarifa tu ni kwamba kikwete hatokuwa salama baada ya 2015
Mkuu this is more more serious! Haya ni mambo viongozi wetu wanahitaji kuyafanyia kazi vizuri. Lakini tatizo hatuna viongozi, ni mashati tu.
 
Commonmwananchi,
Hivi niambie ukweli bila kujali itikadi ya vyama vyetu, hivi morale ya kazi inatoka wapi kama wafanya kazi wataendelea kuona baadhi ya watu waliopewa dhamana wakijitajirisha kwa kutumia ofisi za umma bila hata kunyooshewa kidole?
Hivi madaktari na wengine wanaoiba dawa za hospitali wataachaje huku wakiona na kushuhudia wajanja wachache wakineemeka wao na watoto wao bila huruma na wao wakiendelea na tumishahara tusitofika mwisho wa mwezi?

Nnauye Jr,
Kwa kauli yako binafsi,ni kwamba unakubaliana na mimi kwamba morali wa waalimu wetu nchini umeshuka kwa kiwango cha juu kama tulivyoona matokeo ya kidato cha nne kama kielelezo cha hilo.

Sasa tukirejea hoja ya msingi,suala hili linakihusu chama chako na serikali yake.kwa vile uko katika vita dhidi ya ufisadi,na walimu ni kundi kubwa sana la wapiga kura nchini tena wengi wao wakiwa wanachama hai wa ccm.ninakushauri uanze kampeni ya kuwahamasisha walimu nchi nzima wajiandae kwa uchaguzi mkuu wa ccm unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wao kwa uelewa wao mkubnwa wakusaidie kutowachagua mafisadi kurudi katika nafasi walizonazo kwa sasa. Na pia wakusaidie kutoa elimu ya uraia kwa nafasi walizonazo kama walimu.

Wewe unatakiwa kutafuta kundi la kutoka nalo kama nguzo yako kuu kukulinda katika umma huu na hii ni pale tu litakapojiridhisha kwamba uko pale kwa uchungu wa kweli dhidi ya dhulma hii ya ufisadi.

Kimsingi sikuchochei ili ufanye maasi ndani ya chama chako,bali ufanye mageuzi ya utendaji yatakayokupambanua kama mpiganaji wa kweli na si kama hao wengine ambao wanapigana kwa staili ya popo.
 
Commonmwananchi,
Umeuliza maswali ya msingi sana kwa hali ya nchi yetu. Nitayajibu kadri niwezavyo..... Lakini la kwanza si kweli kwamba eti kila nikisimama au kuulizwa swali nazungumzia Ufisadi tu, si kweli! Japo naamini ufisadi( kwa tafisiri ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa faida ya mtu binafsi au kikundi kidogo cha watu) ndio msingi mkuu wa matatizo mengi nchini, kwahiyo badala ya kubaki kukata matawi, bora kuchimbua mzizi kabisa. Hili linawakera wengi ndo maana huniita vuvuzela kwa maana sauti ya vuvuzela inakereketa masikioni.[/QUOTE

Nnape Jr,nakushukuru sana kwa kunijibu kadri uwezavyo na kwa manufaa ya wengi humu JF.

Je? kama ni kukata mzizi wa ufisadi ndani ya chama chako ccm,huogopi kwamba kwa kuchimba kwako mzizi utaanguka pamoja na huo mti kwani utakuangukia wewe mwenyewe??
 
Too low. Nova anasubiri majibu ya Nape ambayo anaendelea kujibu. You are the one gossiping.

Great seers knew well in advance what would happen. You can know sense who is too low, gossiping! Never discuss people if you aspire to be ontop list minds.
 
Commonmwananchi,

Nakuomba sana sana wewe na mwingine yeyote ambao bado mnaamini hoja kuwa Nape alipigwa marufuku Igunga mnijibu maswali haya mawili;

1. Ni uchaguzi gani mdogo toka tumeanza chaguzi ndogo nchini chini ya mfumo wa vyama vingi ambapo Katibu Mwenezi wa CCM ameenda kwenye kampeni na akakaa huko mwanzo mpaka mwisho??

2. Hivi mbona Igunga ndo inaulizwa ni kwanini juzi hamjauliza Uzini na nahakika hamtauliza Arumeru Mshariki? Bila shaka unaona hoja hii ilitokana na kuanguka kwa mbuyu ulioasisi matumizi ya pesa kwenye chaguzi, yeye na wapambe kutoamini kwamba sasa wanafikia mwisho?

Nnape JR,
napenda uelewe kwamba,kwako wewe ule uchaguzi wa igunga ulikuwa ni kipimo rasmi cha kuona nini inakuwa mapokeo ya vita yako dhidi ya vigogo ndani ya chama chako.

*Ni pale Igunga tulipotarajia kukuona ukiwathibitishia wana ccm wenzako na wananchi kwa ujumla,ukiongoza jukwaa la kampeni,ikiwa baada ya mmoja wa vigogo watuhumiwa wakuu wa ufisadi ndani ya ccm kujivua gamba.vita ambayo bila shaka huyu ni majeruhi wako.

Hii ingetufanya wengi tuamini kwamba mwenyekiti wako yuko pamoja na wewe.lakini kwa yaliyojitokeza igunga kukuhusu wewe,basi wengi tunaingiwa na shaka kama mnacheza wimbo mmoja na mwenyekiti wako.

Ebu jaribu kutafakari na chukua hatua!
 
Hongera sana ndugu Nape kwa majibu yako.
Nape wewe ni kijana shupavu sana,kama mtu anashindwa kuona effect zako basi huyo atakuwa na utindio.Jambo la msingi,jitahidi kutimiza yale yote muliotuaidi kwani hlo litaongeza heshima yako na chama pia.
 
Commonmwananchi,
Kwanza sasa unaona mmekuwa mkiendesha maneno haya kama sio wewe basi wengine kwa kile mnachohisi kinapaswa kuwa badala ya kufuata uhalisia? Sio utaratibu wa CCM kumtumia katibu Mwenezi kwenye Chaguzi ndogo! Lakini siri iliyopo sasa yeye ndo huwapiga sana wapinzani wakati wa uchaguzi mdogo kwa ngumi zisizoonekana

QUOTE=commonmwananchi;3348373]Nnape JR,
napenda uelewe kwamba,kwako wewe ule uchaguzi wa igunga ulikuwa ni kipimo rasmi cha kuona nini inakuwa mapokeo ya vita yako dhidi ya vigogo ndani ya chama chako.

*Ni pale Igunga tulipotarajia kukuona ukiwathibitishia wana ccm wenzako na wananchi kwa ujumla,ukiongoza jukwaa la kampeni,ikiwa baada ya mmoja wa vigogo watuhumiwa wakuu wa ufisadi ndani ya ccm kujivua gamba.vita ambayo bila shaka huyu ni majeruhi wako.

Hii ingetufanya wengi tuamini kwamba mwenyekiti wako yuko pamoja na wewe.lakini kwa yaliyojitokeza igunga kukuhusu wewe,basi wengi tunaingiwa na shaka kama mnacheza wimbo mmoja na mwenyekiti wako.

Ebu jaribu kutafakari na chukua hatua![/QUOTE]
 
commonmwananchi,
kwanza sasa unaona mmekuwa mkiendesha maneno haya kama sio wewe basi wengine kwa kile mnachohisi kinapaswa kuwa badala ya kufuata uhalisia? Sio utaratibu wa ccm kumtumia katibu mwenezi kwenye chaguzi ndogo! Lakini siri iliyopo sasa yeye ndo huwapiga sana wapinzani wakati wa uchaguzi mdogo kwa ngumi zisizoonekana
nashukuru kwamba bado upo na mimi kwani nilitarajia kwamba umejitoa.kwani umekuwa slow katika kutoa majibu.
Naomba utowe majibu yenye kutoshana na maswali husika kwani kwa mwanzo ulisema utajitahidi kunijibu kadri ya uwezo wako.lakini ghafla umekuwa mtu wa short-cut, ninajua kabisa kwa nafasi yako una mambo mengi ya kimajukumu yanayokusubiri kutekkeleza.
Lakini kwa faida yako na yangu pia ni vema pale unapopata nafasi ya kutembelea humu jf,basi uwe kama uko ofisini pia.
Sias za kisasa ni pamoja na midahalo isiyokuwa rasmi lakini yenye kutoa changamoto kama hii..nikutakie usiku mwema nikitumai kesho utakuja na majibu ya kuyosha si kwangu tu bali kwa wote waliopata nafasi ya kuuliza maswali yao kwako.

Alamsiki.

Quote=commonmwananchi;3348373]nnape jr,
napenda uelewe kwamba,kwako wewe ule uchaguzi wa igunga ulikuwa ni kipimo rasmi cha kuona nini inakuwa mapokeo ya vita yako dhidi ya vigogo ndani ya chama chako.

*ni pale igunga tulipotarajia kukuona ukiwathibitishia wana ccm wenzako na wananchi kwa ujumla,ukiongoza jukwaa la kampeni,ikiwa baada ya mmoja wa vigogo watuhumiwa wakuu wa ufisadi ndani ya ccm kujivua gamba.vita ambayo bila shaka huyu ni majeruhi wako.

Hii ingetufanya wengi tuamini kwamba mwenyekiti wako yuko pamoja na wewe.lakini kwa yaliyojitokeza igunga kukuhusu wewe,basi wengi tunaingiwa na shaka kama mnacheza wimbo mmoja na mwenyekiti wako.

Ebu jaribu kutafakari na chukua hatua!
[/quote]
 
Nataka kujuzwa na Katibu Mwenezi wa CCM:Hivi karibuni,Katibu mkuu Wilson Mukama amenukuliwa akisema,sasa chama kimeamua kuwa hakitafukuza mtuhumiwa yeyote wa ufisadi.
Miezi kadhaa huko nyuma Mukama,ktk taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema chama kilikuwa kimeamua kuwa baadhi ya maazimio kuhusu dhana ya kujivua gamba yalihitaji mabadiliko ya Katiba ya chama chenu..ktk kikao cha hivi karibuni, mmeazimia kuwa sasa wabunge hawataweza kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
Ni dhahiri kuwa, uamuzi wenu huu utawagusa hata wale wachache waliopo CCM ambao ni mawaziri ama wabunge,ambao hawana tuhuma za ufisadi ingawa ni wazi kuwa walengwa halisi wa mpango huu ni wale mapacha wawaili waliobaki.
Nadhani CCM haina ujasiri wa kiuongozi.
 
FortJeasus,
UMEMALIZIA KUWA UNADHANI, WACHA NIKUACHE UENDELEE KUDHANI, MAANA DUNIA YA LEO DHANA ZIKO NYINGI NA UKITAKA KUJIBU KILA MOJA MHHH, HATUTAFIKA

Nataka kujuzwa na Katibu Mwenezi wa CCM:Hivi karibuni,Katibu mkuu Wilson Mukama amenukuliwa akisema,sasa chama kimeamua kuwa hakitafukuza mtuhumiwa yeyote wa ufisadi.
Miezi kadhaa huko nyuma Mukama,ktk taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema chama kilikuwa kimeamua kuwa baadhi ya maazimio kuhusu dhana ya kujivua gamba yalihitaji mabadiliko ya Katiba ya chama chenu..ktk kikao cha hivi karibuni, mmeazimia kuwa sasa wabunge hawataweza kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.
Ni dhahiri kuwa, uamuzi wenu huu utawagusa hata wale wachache waliopo CCM ambao ni mawaziri ama wabunge,ambao hawana tuhuma za ufisadi ingawa ni wazi kuwa walengwa halisi wa mpango huu ni wale mapacha wawaili waliobaki.
Nadhani CCM haina ujasiri wa kiuongozi.
 
Kakaangu Kiungani,

Nashukuru sana, nimekusoma na nimepata muda kurudia tena na tena makala yako, naomba nikushukuru kwa dhati kabisa ya moyo wangu. Ushauri ulioutoa nitaufanyia kazi.

Nina swali moja tu, ungekuwa wewe kwenye nafasi yangu kwa swala lolote chukua mfano wowote wa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi KAMA KATIBU MWENEZI WA CHAMA UNGEFANYA NINI CHA ZIADA ZAIDI YA NILICHOFANYA MIMI?

Nape, umeuliza swali la msingi kabisa.

Kama ningekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kwenye mazingira kama haya ningefanya nini tofauti na haya unayofanya sasa? Ni hypothetical question, lakini ngoja nijaribu kulijibu kwa ujumla wake.

Pambana na mfumo, usipambane na mtu au watu.

Mfumo ndiyo unamfanya Rais anabariki maamuzi ya Baraza la Mawaziri, halafu akiwa kama Mwenyekiti CCM analaani maamuzi hayo hayo (IPTL, Kuuza Nyumba, Kiwira, EPA, Radar, Richmond, Dowans, Buzwagi, Mafuta EWURA, Hali ngumu ya Maisha, Migomo, n.k.)

Mfumo ndiyo unawafanya watendaji (TAKUKURU, IGP, Mwanasheria Mkuu) waseme wezi wa EPA wote washitakiwe, Raisi anasema wakirudisha hela watasamehewa.

Mfumo ndiyo unamfanya Raisi abariki maamuzi ya Baraza La Mawaziri kuwa Dowans walipwe fidia, na serikali imetenga pesa, halafu Mwenyekiti wa CCM na NEC wanalaani malipo hayo.

Mfumo ndiyo unamfanya Mwanasheria Mkuu aseme Dowans lazima walipwe, halafu akiwa Bungeni anaisaidia serikali kusimamia maazimio ya Bunge yatekelezwe (mojawapo ya maazimio ni kupinga malipo ya Dowans).

Mfumo ndiyo unamfanya Mjumbe wa NEC aandae sera za Chama, halafu huyo huyo awe mbunge azipitishe hizo sera, halafu huyo huyo awe Waziri au Mkuu wa Mkoa/Wilaya asimamie utekelezaji wa hizo sera, halafu matokeo yakiwa mabaya analaumu kuwa utekelezaji si mzuri au sera haziambatani na matakwa ya wananchi.

Mfumo ndiyo unawapa Wabunge wetu nguvu ya kujipangia mishahara na marupupu mapya, BAADA ya kuwa wameishakubali kufanya kazi kwa malipo na marupurupu ya awali. Wakati wanagombea wanajua malipo ni nini, wakiishachaguliwa wanaanza kuyabadilisha.

Mfumo ndiyo unamfanya Mtoto wa Mkulima awe na misafara ya magari 45 kwenye ziara moja, wakati Baba yake (Mkulima mwenyewe) hana hata gari moja.

Mfumo ndiyo unamfanya Waziri Mkuu awe na jukumu la kusimamia Mawaziri na Makatibu wakuu ambao yeye hana madaraka ya kuwateua wala kuwawajibisha (Angalia hao nyani wasile mahindi, wakila mahindi njoo uniambie).

Mfumo ndiyo unamfanya Mwenyekiti wa Chama anakuwa na nguvu kuliko Katibu Mkuu ambaye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za Chama.

Mfumo ndiyo unamfanya Mwenyekiti aweze kusema kuwa sasa ni zamu ya mwanamke, na kweli jinsia (uke) inakuwa ndiyo sifa pekee ya nafasi ya uongozi wa kitaifa badala ya uwezo, nia au ufanisi. (Spika Makinda na Wabunge Viti Maalumu).

Mfumo ndiyo unamfanya Raisi ateue mtu yeyote anayempenda kufanya kazi yoyote, halafu kukiwa hakuna ufanisi, Raisi huyo huyo analalamika kuwa wasaidizi wake wanamwangusha. Hakuna kipimo cha ufanisi kama kigezo cha uteuzi wo wote.

Mfumo ndiyo unawaruhusu mke wa Raisi na watoto wake kusomewa taarifa za maendeleo mikoa/wilaya kwa kuwa tu ni mke au mtoto wa Raisi. Hizi taarifa wanazipeleka wapi na kama nani?

Mfumo ndiyo unampa nguvu Raisi wa kuchagua Baraza lote la Uchaguzi, halafu anarudi kama Mwenyekiti wa Chama na kutegemea baraza hilo lisimamie ‘kwa haki’ uchaguzi unaomhusu yeye.

Mfumo ndiyo unawapa Bunge mamlaka ya kutunga sheria kuwa wananchi wanaweza kutoa mawazo yao kuhusu katiba, lakini mtu akiwaelimisha wananchi kuhusu hayo mabadiliko, basi anaweza kushitakiwa na kufungwa. Kwa hiyo watu waseme, lakini waseme kile tu kinachowapendezesha serikali.

Huu mfumo ndiyo umetupa Mkapa, Kikwete, Werema, Hosea, Lowassa, Rostam, Sitta, Membe, Mwema, Mwinyi (Mbagala, Gongo La Mboto) na utitiri wa viongozi na watendaji lukuki wabovu, pamoja na hata mimi na wewe Nape mwenyewe.

Kwa hiyo Nape kama kweli unataka ushauri wangu kuwa ufanye nini, basi tumia nafasi yako kupambana na mfumo na usiangalie jina la mtu au watu. Fanya mapambano yako yawe dhidi ya mfumo mbovu na siyo watu binafsi au kundi la watu Fulani.

Saidia mapambano ya kubadilisha mfumo na ufisadi wo wote uwe wa Lowassa, Kikwete, Mkapa au ye yote mwingine hautakuwepo.
 
kiungani,
UMEZUNGUMZA VYEMA SANA, SASA PENGINE KWA FAIDA YA WENGI PIA HAPA JAMVINI UNAPAMBANA VIPI NA MFUMO? NJIA AMBAYO NI TOFAUTI NA HII NINAYOTUMIA AU AMBAZO NIMEWAHI KUTUMIA HATA HUKO NYUMA TANGU SIJAWA KATIBU MWENEZI? LAKINI NAOMBA KUPANUA UFAHAMU WANGU, NI MFUMO GANI AMBAO HAUNA WATU NDANI YAKE WANAOUFANYA HUO MFUMO UENDELEE KUWEPO NA WAO WAENDELEE KUFURAHIA NA KUFAIDIKA KWENYE MFUMO HUO?

BILA SHAKA KWA NYONGEZA TU VINGINEVYO KUWE NA MFUMO USIOKUWA NA WATU, KAMA KILA MFUMO UNA WATU BILA SHAKA UTAKUTA BAADHI YA WATU WALIOMO WANAFAIDIKA NA MFUMO NA HAO UKITAKA KUBADILI MFUMO NDIO WATAKAOKUPINGA KWA NGUVU ZOTE!! PENGINE NISUBIRI MAJIBU YAKO........

Nape, umeuliza swali la msingi kabisa.

Kama ningekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kwenye mazingira kama haya ningefanya nini tofauti na haya unayofanya sasa? Ni hypothetical question, lakini ngoja nijaribu kulijibu kwa ujumla wake.

Pambana na mfumo, usipambane na mtu au watu.

Mfumo ndiyo unamfanya Rais anabariki maamuzi ya Baraza la Mawaziri, halafu akiwa kama Mwenyekiti CCM analaani maamuzi hayo hayo (IPTL, Kuuza Nyumba, Kiwira, EPA, Radar, Richmond, Dowans, Buzwagi, Mafuta EWURA, Hali ngumu ya Maisha, Migomo, n.k.)

Mfumo ndiyo unawafanya watendaji (TAKUKURU, IGP, Mwanasheria Mkuu) waseme wezi wa EPA wote washitakiwe, Raisi anasema wakirudisha hela watasamehewa.

Mfumo ndiyo unamfanya Raisi abariki maamuzi ya Baraza La Mawaziri kuwa Dowans walipwe fidia, na serikali imetenga pesa, halafu Mwenyekiti wa CCM na NEC wanalaani malipo hayo.

Mfumo ndiyo unamfanya Mwanasheria Mkuu aseme Dowans lazima walipwe, halafu akiwa Bungeni anaisaidia serikali kusimamia maazimio ya Bunge yatekelezwe (mojawapo ya maazimio ni kupinga malipo ya Dowans).

Mfumo ndiyo unamfanya Mjumbe wa NEC aandae sera za Chama, halafu huyo huyo awe mbunge azipitishe hizo sera, halafu huyo huyo awe Waziri au Mkuu wa Mkoa/Wilaya asimamie utekelezaji wa hizo sera, halafu matokeo yakiwa mabaya analaumu kuwa utekelezaji si mzuri au sera haziambatani na matakwa ya wananchi.

Mfumo ndiyo unawapa Wabunge wetu nguvu ya kujipangia mishahara na marupupu mapya, BAADA ya kuwa wameishakubali kufanya kazi kwa malipo na marupurupu ya awali. Wakati wanagombea wanajua malipo ni nini, wakiishachaguliwa wanaanza kuyabadilisha.

Mfumo ndiyo unamfanya Mtoto wa Mkulima awe na misafara ya magari 45 kwenye ziara moja, wakati Baba yake (Mkulima mwenyewe) hana hata gari moja.

Mfumo ndiyo unamfanya Waziri Mkuu awe na jukumu la kusimamia Mawaziri na Makatibu wakuu ambao yeye hana madaraka ya kuwateua wala kuwawajibisha (Angalia hao nyani wasile mahindi, wakila mahindi njoo uniambie).

Mfumo ndiyo unamfanya Mwenyekiti wa Chama anakuwa na nguvu kuliko Katibu Mkuu ambaye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za Chama.

Mfumo ndiyo unamfanya Mwenyekiti aweze kusema kuwa sasa ni zamu ya mwanamke, na kweli jinsia (uke) inakuwa ndiyo sifa pekee ya nafasi ya uongozi wa kitaifa badala ya uwezo, nia au ufanisi. (Spika Makinda na Wabunge Viti Maalumu).

Mfumo ndiyo unamfanya Raisi ateue mtu yeyote anayempenda kufanya kazi yoyote, halafu kukiwa hakuna ufanisi, Raisi huyo huyo analalamika kuwa wasaidizi wake wanamwangusha. Hakuna kipimo cha ufanisi kama kigezo cha uteuzi wo wote.

Mfumo ndiyo unawaruhusu mke wa Raisi na watoto wake kusomewa taarifa za maendeleo mikoa/wilaya kwa kuwa tu ni mke au mtoto wa Raisi. Hizi taarifa wanazipeleka wapi na kama nani?

Mfumo ndiyo unampa nguvu Raisi wa kuchagua Baraza lote la Uchaguzi, halafu anarudi kama Mwenyekiti wa Chama na kutegemea baraza hilo lisimamie ‘kwa haki' uchaguzi unaomhusu yeye.

Mfumo ndiyo unawapa Bunge mamlaka ya kutunga sheria kuwa wananchi wanaweza kutoa mawazo yao kuhusu katiba, lakini mtu akiwaelimisha wananchi kuhusu hayo mabadiliko, basi anaweza kushitakiwa na kufungwa. Kwa hiyo watu waseme, lakini waseme kile tu kinachowapendezesha serikali.

Huu mfumo ndiyo umetupa Mkapa, Kikwete, Werema, Hosea, Lowassa, Rostam, Sitta, Membe, Mwema, Mwinyi (Mbagala, Gongo La Mboto) na utitiri wa viongozi na watendaji lukuki wabovu, pamoja na hata mimi na wewe Nape mwenyewe.

Kwa hiyo Nape kama kweli unataka ushauri wangu kuwa ufanye nini, basi tumia nafasi yako kupambana na mfumo na usiangalie jina la mtu au watu. Fanya mapambano yako yawe dhidi ya mfumo mbovu na siyo watu binafsi au kundi la watu Fulani.

Saidia mapambano ya kubadilisha mfumo na ufisadi wo wote uwe wa Lowassa, Kikwete, Mkapa au ye yote mwingine hautakuwepo.
 
Nape una kazi kijana mwenzangu hapa hao wazee ni vigumu sana kuwabadilisha hata kama si wala rushwa.

Vilevile tunajua shule ambazo zinafelisha Tanzania mwaka hadi mwaka ningependa kusikia kutoka kwa vijana wazo kama hili.

Vile vile CCM hata Vyama vya upinzani hamjajiuliza hili: Je serikali inatakiwa kufanya nini? Sasa serikali inafanya vitu kuliko uwezo wake na kila tatizo likitokea tunataka serikali itatue na iwe kubwa zaidi. Je nyie vijana mmekuja na mpango gani wa kuifanya serikali ya Tanzania kuwa ndogo na ya ufanisi? Sijawahi kusikia Idea yeyote ya maana kwenye hili.

Nimeandika mambo mengi hapa lakini bado Nape nasikitika kwamba vijana hamna "Big Ideas" kabisa. Hata Nape ungeweza kuomba Ideas kutoka kwa watu hata hapa mtandaoni lakini hujawahi kufanya hivyo.

Haya ni baadhi ya mawazo mazuri sana ambao yakifanyiwa kazi, hakika yatatupa dira ya nchi hii in a sustainable way, kwa sababu sioni vijana wenzetu wakiwa na agenda nyingine kubwa zaidi ya ufisadi na kushindana kwa hoja ambazo ni very very short lived. Hakuna Kijana yoyote mwenye uongozi katika vyama vyote vikuu, ambae ana uthubutu kwa mfano wa kusimamia itikadi ya chama chake na kuiuza mbele ya umma kwa kujiamini na kuwa na uhakika na anacho kizungumza, hasa kwa kuoanisha itikadi na sera za vyama vyao, kama kielelezo cha mabadiliko au tuseme maisha bora kwa electorate. Ni bahati tu kwamba watanzania wengi hawaelewi kwamba itikadi ndio life blood ya chama, na ndio huzaa mengine yote yanayohusiana na chama. Mwanakijiji aliandika makala nzuri sana juu ya umuhimu wa itikadi kwa chama wiki iliyopita kwenye Tanzania Daima. Kutokana na vyama vyote kupwaya kiitikadi, ndio maana kurasa za katiba zinazo zungumzia itikadi katika vyama vyao ndio kurasa mpya kuliko zote; kurasa zilizochakaa ambazo ndizo wanazigusa gusa kila siku, ni zile zisizokuwa na lolote la maana kwa maisha ya kila siku ya mtanzania.

Asante sana Kamundu, ni matumaini yangu wenye kukuelewa watachuma katika haya. Vinginevyo kwa jinsi siasa za vyama vyetu zinavyo evolve, it is becoming more evident kwamba the agent of change katika jamii yetu has to be kitu kingine beyond partisan politics, kwani vyama kwa hili vinaelekwa kushindwa, hasa kwa sababu vyama havina muda kuhusisha wasomi na wataalam. Pengine itahitaji think tanks zianzishwe ili ziende moja kwa moja kwenye jamii kuwapatia elimu ya uraia juu ya jinsi gani ya ku influence policies on issues that matter the most kwa maisha yao - kisiasa, kijamii, kiuchumi n.k. Au pengine turejee yale majukwaa ya mijadala pale Mlimani enzi za Mwalimu, ambapo Mwalimu aliwahusishwa vijana/wasomi katika kila sera na kila jambo linalo husu nchi hii. Tunahitaji uongozi wa vyama utakaoiga tabia hii ya Mwalimu.
 
jamani kaka nape! Kwa nini unalewa pombe asubuhi!

watu dizaini yako ndio mnafukuza watu ambao tunapenda tuwe nao humu ili tuwabane kwa hoja na kusikia mengi toka kwao...halafu baadae tunalalamika fulani kaingia mitini siku hizi..
 
Nape, binafisi nakupongeza kwa kazi yako ngumu, umefanya vizuri sana, najua nguvu kubwa waliyo nayo mafisadi, kwa nchi masikini kama yetu, jamaa hawa ni hatari sana maana kwa umasikini wa watanzania wapo tayari kuuza utu wao kwa ajili ya elfu 1 tu. Mimi nina ushauri, najua mtashinda na mafisadi watatoka maana msipofanya hivyo basi mjue chama kinakufa, msidiriki kurudi nyuma hata kama mlikosea, ila ni lazima mafisadi wakitoka ndani ya chama shariti muwatie kizuizini, wakibaki mtaani wataendelea kuleta madahara, kwa akiri yangu Rostam hakustahili kuwa mtaani. Kila la heri mkuu, mie sio mwana CCM ila kwa hili nakuunga mkono, sipendi ccm ife maana tutakosa changamoto.
 
Ndugu Nape Nnauye,
(Katibu Mwenezi wa chama cha mapinduzi,)

Napenda kukumbusha dhamira yako na mkakati wako ulio anza nao kwa mbwembwe nyingi za Kuwavua magamba mapacha watatu ambapo ulikuwa jasiri wa kufikia hatua ya kuwataja majina kuwa ni Ndugu Edward Lowasa, Mtemi Endrew Chenge na King maker Rostam Aziz!

Ni King Maker pekee alieamua kujiengua tena kwa masharti kuwa wewe Nape usishiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga la sivyo King Maker angeweza kukiharibia chama! na ni kweli madai yake yalitekelezwa na chama chako na kukuweka kando kabisa ya kampeni za uchaguzi mdogo. Hata hivyo ulijitahidi kujitutumua kukanyaga Igunga kwa kisingizio ulikwenda kuhani msiba. Nadhani hiyo ilikuwa ni dalili tosha kuwa maadui zako wana mtandao na mzizi mkuu ndani ya chama chako dhidi yako!

Ndugu yangu Nape, Ni kweli kuwa umewashindwa kuwang'oa EDWARD LOWASSA na MTEMI ENDREW CHENGE? kama ulivyojigamba hapo awali kuwa utawang'oa? Tumeshuhudia wiki chache zilizopita Chenge akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ya bunge na kutoka na jina jipya la MTEMI ANDREW CHENGE, hivyo kutoka mzee wa vijesenti hadi MTEMI?! mhhh! Nape Upo hapo?

Na baada ya hapo Edward Lowasa akatoka na single mpya kuwa MAADUI WAKE HAWAMUWEZI!!! na adui mkubwa mmoja wapo ni wewe bwana Nape! Je ni kweli humuwezi bwana Edo! Nape kumbuka ulituaminisha kuwa umekuja kusafisha chama chenu ambacho tumekosa imani nacho hata chembe! sasa bwana Nape tunaomba ukiri wazi kuwa Je ni kweli huwawezi na wewe unaendelea kujichoresha mitaani wakati MAPACHA watatu wanaendelea kujiimarisha?

Je kati yako na Mapacha watatu nani ana sikio la bwana mkubwa JK? Kwa maana Edo alikwisha sema mara kadhaa kuwa yeye na JK hawajakutana mitaani! sasa kijana mwenzetu hebu funguka utueleze kinaga ubaga ule mkakati wa kuwavua magamba umeyeyukia wapi? Nape...I am curious and confussed! Jamaa wamekuja na mkakati wa kuwatetea wakulima wa pamba, kwa sisi wajanja tumekwisha gundua kuwa ndo agenda za kampeni za Uraisi 2015,,,........

Hivyo ndugu yetu vunja ukimya uje hapa jamvini utueleze kampeni yako ya kuvua gamba imefia wapi??

Nitafurahi sana bwana Nape kama utakuwa jasiri wa na kutoa ufafanuzi juu ya mkakati wa kuvua gamba! sidhani kama wewe utakuwa coward wa kisiasa kiasi hicho na kushindwa kujibu hoja zangu, hapo juu. Na kama umeshindwa basi tufahamishe tujue tutakuelewa.

Back
Top Bottom