Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

and vice versa is true ndio mana mnauwa watu na mmeamua kuwakaribisha akina kamerun na wale wazee wadenmark kuanza kutunisha mfuko... japo inasemekana zinafanyiwa dili kwenye ziara za emfoc eti zimeibiwa kumbe ni janja ya nyani

Anae ua ni Ighondu na wanaomtuma.
Huwajui?
 
Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “CHADEMA wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa CHADEMA alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.
HADEMA kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.
Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa CHADEMA kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.
CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-



Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013

Wewe Nape na Mwakyembe wakom hamna lolote subirini kiama chenu 2015. Huyo Mwakyembe aliyekuwa analalamika mbona sasa yuko na haohao aliokuwa anawalalamikia.
 
we kweli mshamba. Yani hujui kuwa ccm imekuwa na shughuli za uzalishaji mali tangu enzi za sukita?

Nyinyi vijana wa juzijuzi wa bavicha mna matatizo sana.

ivi wewe! Unaweza kutuambia maccm wanakulipa sh ngapi?
 
hongera mkuu caricullum specialist kwa kuingia kwa jina lako halisi...mungu akupe nguvu na uhai mrefu tuitumikie nchi yetu.....naona chadema wanajitahidi sasa kumchafua mwakyembe baada ya kushindwa kwa wengine

cha kushangaza ni pale wanapomuunga mkono Lowassa na kumzushia Msafi wa wasafi.
Hatakama mimi ni cdm kwa hapa ninapatwa na kichefuchefu.
Labda waeleze kwamba sio wanachadema walioandika ile thread ya kumkubali Lowassa ambaye hata yeye mwenyewe anajijua kuwa ni mchafu kuliko hata choo.
 
Nape ametumia nguvu kubwa sana kuituhumu CDM kwenye hili jambo. Lakini kwa ufukunyuku wa haraka haraka inaonekana hiyo kampuni ya JITEGEMEE TRADING Co. LTD anayosema Nape kuwa inamilikiwa na ccm haijasajiliwa/haipo kwenye orodha ya makampuni yaliyosajiliwa BRELA.

Kwa mantiki hiyo na kwa kuwa Nape amekiri kuwa hiyo kampuni inamilikiwa na CCM, ni vyema akatoa ufafanuzi kuhusu usajili wa hiyo kampuni, lini imesajiliwa BRELA, imesajiliwa kwa shughuli gani, wakurugenzi wake

ni nani na kama imeshawahi kulipa kiasi chochote cha kodi kwa TRA kwa kipindi chote tangu ianzishwe.
Mkuu, hapa ni magumashi tuu. Baada ya kusoma uzi huu,nilimpigia simu Mzee wangu mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM. Kwa vile nilikuwa nafahamu kuwa yeye sio kizazi cha digital nilijua atakuwa hajasoma au kusikia mtanange huu na majibu ya Nape.
Nilipomwambia hiyo kampuni yenu ya Jitegemee Trading Company Ltd mbona inapendelewa! Mzee kaja juu na kuikana kuwa hiyo kampuni sio ya CCM. Nikamwambia huelewi wewe! Kaapa na kusema yeye ni mjumbe wa NEC hiki ni kipindi cha pili asijue Kampuni za Chama wakati wao ndio wenye chama?
Swali: jee si kweli kuwa Jitegemee inajulikana kwa wachache tuu kama sehemu ya kufanyia magumashi yao? Iweje Wajumbe wa NEC ambacho ni kikao cha juu cha Chama wawe hawajui uwepo wa Kampuni hiyo mpaka Chadema wawazindue? Niwaambie wana CCM,chama hicho sio chenu,CCM ina wenyewe!
Hata haya mavuvuzela yanayopiga mayowe hapa JF nina hakika hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua kuwa kampuni hiyo ni ya CCM, ila Chadema wakiwatoa tongotongo wanafyatuka na matusi na kauli za kuchanganya mambo kama alivyo changanya mambo Senior Resident Vuvuzela Nape
 
Itatumika kufisa fedha za wizi kwa ajili ya kampeni ya CCM 2015.
 
Huu ni mgongano wa kimaslahi mkubwa sana, CCM inatutia hofu watanzania, je ni makampuni mangapi ambayo hatuyajui yanayokamua kodi za wananchi? CCM ni aibu kwenu kufanya ukatili huu kwa watanzania! Mwakyembe usikubali kuchafuliwa!
 
HIVI,ule UFISADI WA JENGO LA UVCCM ulitakaswa na nani ndugu NAPE...Tangu ulipopewa ukuu wa Wilaya Masasi hukutoa pua tena kuushadadia!Hicho unachosema CHADEMA wanapitia wakati mgumu ni wakati mwepesi sana kama hujui!CCM mmetumbua macho yote kwenye ile video mliyorekodi wenyewe!Ni bahati mbaya kwenu kwamba mmeileta wakati ambao mfa maji hana hata nguvu za kutapatapa!PROPAGANDA inayoweza kuwafanya angalau kutapatapa ni kupunguza gharama za maisha na kuboresha elimu...Hizi sarakasi mnazozifanya ni kutusahaulisha hayo.MMEKWAMA.
 
Heshima kwenu wanabodi,

Jana kuna uzi ulianzishwa hapa JF ambao una husu JITEGEMEE TRADING COMPANY LTD ambayo imepatiwa zabuni TPA yenye thamani ya 10 bili.Swali ambalo lilikuwa linagonga vichwa vya wanadau ni mchakato wa upatikanaji wa tenda au zabuni hiyo. Swali la pili likuwa ni nani mmiliki wa hiyo kampuni. Hatimaye leo Nape kupitia Press release yake amethibitisha kuwa kampuni tajwa inamilikiwa na CCM. kusoma hiyo Pres release gonga hapa.
Scribd

Naomba kuwasilisha
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013
There must be conflict of interest hapawezi kuwa na ushindani hapo wizi mtupu! Nape mambo mengine kuyaongea ni aibu! and Tanzanians are tired Mwakyembe hukuona hilo au hujui MAJAMBAZI WA MCHANA MCHANA viva CDM mUngu awabariki! Aluta Continua tuta shinda tu!
 
Nnape, tatizo unakurupuka bila kujua nini kinaendelea ,

1. Ni kuwa kwenye kikao cha mamlaka ya Bandari kilichoketimwezi Machi tayari walishatenga fedha kiasi cha shilingi bilioni kumi za kitanzania kwa ajili ya kuwalipa CCM na baadhi ya wajumbe walipinga sula hilo kwa hoja kuwa hapakuwa na tenda wala utaratibu uliofuatwa ili kuipatia kampuni hiyo ya CCM tenda , kampuni hii inasimamiwa na Peter MAchunde, Sam Mapande et al, na ndio inajenga ukumbi wa kisasa kule Dodoma ( Jitegemee)

2. Chadema , haiwezi kukaa kimya tena mpaka yatokee yale ya Deep Green , Tangold na wenzake ambao unawajua vizuri, sasa kila hatua itafuatiliwa kikamilifu kuelekea 2015 kwani Chadema wanajua kuwa tangu 1995 mmekuwa mkijichotea fedha za walipa kodi kwa ajili ya chaguzi kama ifuatavyo,
1995 ......zimbabwe na Malaysia kwa IPTL .....WAliofanikisha dili hilo ni Marehemu Kolimba na Abdalah Kigoda.

2000.......aggreko, Wartsila, Barrick Gold et all

2005....... mkuu natumia cm ningekupa like
 
Join Date : 1st February 2013 Posts : 1,411 Asante jf naona mmetengeneza ajira.Almost 26 posts per day! utaifakwanza wewe hauna kazi nyingine tofauti na hii?
 
ushauri wangu kwa ccm kama kweli mnataka muendeleee kutawala nchi hii tatueni matatizo ya msingi ya wananchi, msipoteze muda kuwachafua watu kwani ukweli unajulikana na mnawafanya watu wasiwaamini tena hata pale mtakaposema ukweli.

huu ni ushauri wa bure kwenu ccm na serikali yake

It sounds good. Ila lakufa aliskii dawa....mfano mzuri wafuasi wao hapa jf na wanvyojitahidi kupotezea mada.
 
Mkuu, hapa ni magumashi tuu. Baada ya kusoma uzi huu,nilimpigia simu Mzee wangu mmoja ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM. Kwa vile nilikuwa nafahamu kuwa yeye sio kizazi cha digital nilijua atakuwa hajasoma au kusikia mtanange huu na majibu ya Nape.
Nilipomwambia hiyo kampuni yenu ya Jitegemee Trading Company Ltd mbona inapendelewa! Mzee kaja juu na kuikana kuwa hiyo kampuni sio ya CCM. Nikamwambia huelewi wewe! Kaapa na kusema yeye ni mjumbe wa NEC hiki ni kipindi cha pili asijue Kampuni za Chama wakati wao ndio wenye chama?
Swali: jee si kweli kuwa Jitegemee inajulikana kwa wachache tuu kama sehemu ya kufanyia magumashi yao? Iweje Wajumbe wa NEC ambacho ni kikao cha juu cha Chama wawe hawajui uwepo wa Kampuni hiyo mpaka Chadema wawazindue? Niwaambie wana CCM,chama hicho sio chenu,CCM ina wenyewe!
Hata haya mavuvuzela yanayopiga mayowe hapa JF nina hakika hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua kuwa kampuni hiyo ni ya CCM, ila Chadema wakiwatoa tongotongo wanafyatuka na matusi na kauli za kuchanganya mambo kama alivyo changanya mambo Senior Resident Vuvuzela Nape

Ukiwaambia CCM ya sasa imegeuzwa kuwa club ya familia ya Kikwete na marafiki zake; wasiojua pengine kwa kupumbazwa na buku wanazopewa, airtime pamoja na wali wanaishia kutukana na kutoa kejeli.

Ngoma inayopigwa ndani ya CCM ni wachache mno wanaojua mwelekeo wake hata hao akina Nape bado hawaijui CCM kiundani, wanaishia kutumiwa kwa faida ya wachache basi. Jana Nape alipoulizwa kuhusu hiyo kampuni alikosa jibu lakini leo ameibuka na taarifa nyepesi isiyo na mashiko akijifanya anaijua ilhal hata BRELA kwenyewe haijasajiliwa.
 
Hapo tuu ndipo CHADEMA ninapoikubali! Hivi akili ndogo tu ya kawaida, hata kama ni kuandika barua, eti TPA inaomba kushirikiana na kampuni ya CCM, hapo jibu unategemea nini? Wateule wa pale TPA wamewekwa na Mwakyembe na Mwakyembe ni Waziri toka CCM, jamani acheni siasa hapa, Asante Nape kwa kuivua nguo CCM. Kumbe ndiyo maana mnafiki Mwakyembe aliwafukuza hovyo baadhi ya wafanyakazi huenda alitaka iwe rahisi kuptisha deals kama hizi kirahisi. Poleni sana watu wa Mbeya naona Mwakyembe anawasaliti lakini hii laana itamtafuna milele.
 
Kumbe NAPE unawafahamu mafisadi???
Hivi hawa mafisadi kumbe hawako CHADEMA..ila wanawatumia CHADEMA kumchafua Mwakyembe?
Mwakyembe treni la dar limeenda wapi...tulikuwa tushasahau daladala....
 
There must be conflict of interest hapawezi kuwa na ushindani hapo wizi mtupu! Nape mambo mengine kuyaongea ni aibu! and Tanzanians are tired Mwakyembe hukuona hilo au hujui MAJAMBAZI WA MCHANA MCHANA viva CDM mUngu awabariki! Aluta Continua tuta shinda tu!

Asante CHADEMA kwa kutuokoa na huu Ufisadi Mkubwa! CCM sasa ione aibu kutetea mambo kama haya! Nape unajibagarguza kuihusisha CHADEMA na ufisadi wakati nyie ndo mafisadi wenyewe! Ukitaja UFISADI kwenye hii nchi unakizungumzia chama tawala!
 
SUKITA ilinifurahisha sana wakati ule nasoma Msimbazi Boys kwa jinsi walikuwa wanafuga mangurue mengi hadi basi......hivi bado wanayafuga yale mangurue?
 
Chadema ni mchangia pote na wamebaki kukimbizana nch za watu kupiga kelele na kurudi kapa. Kama kenya waliambulia kilio tu.
 
Back
Top Bottom