ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,690
jamani embu acheni dhambi this way, mnaweza kumwogopa Mola hata kidogo??, kwanini watu muwe makatili na waovu this way?kwanini mtu usiamue kusema ntatenda haki daima kama kiongozi..?? maneno unayoyaandika unajua utakuja kutoa hesabu yake..??
Personally nilimsikia Mwalimu nyerere akiweka bayana kwenye kikao kikubwa cha CCM kwamba, kama CCM imeridhia kuingia kwenye mfumo wa Vyama vingi, basi hapana kuingia nusunusu, ni kujitosa jumla, mali zote za UMMA ambazo Serikali ya CCM Ilikuwa na nmamlaka nazo, yakiwemo makampuni ya Umma Sukita, SIDO na mengineyo, maeneo yote ya wazi ya serikali ambayo chama kiliyahodhi ikiwamo Viwanja vya mpira na ziada ya majengo pamoja na vyuo, kama unakumbuka chuo cha mafunzo magogoni na vinginevyo vilifungwa na vingine kurudishwa serikalini..MWALIMU alitaka hata ofisi za CCM zirudi serikalini lakini wajumbe walilalamika sana, basi majengo ya chama na magari ya chama tu ndiyo yaliyobaki kuwa sehemu ya chama, lakini kukawa na ukimya na sidhani kama sheria iliundwa kuvinakili as governmental assetS!!
BABA wa Watu mwalimu NYERERE hatunae leo, polepole mnaanza kujimilikisha mali hizi, nimeshtushwa mwaka jana kusikia eti KIWANJA CHA BIAFRA NI CHA CCM, Mwembeyanga na vinginevyo, leo tena mtu hapa anabwatuka SUKITA ilikuwa kampuni kaenda mbali zaidi na kusema ya CCM.. hii dhambi mtaitubuje??..
hakuna mambo ya nadharia, uundwaji wa vyama vya kisiasa umeweka wazi jinsi chama kinavyojipatia mapato. ingawa sheria nyingi zinasisitiza
1. uuzaji wa kadi (kama tu mna watu milioni tano, kila mtu akalipa ada yake ya 1000, mna billioni 5.. haziwatoshi?)
2. uuzaji wa machapisho yao
3. ruzuku ya serikali
4. wafadhili
hakuna cha kuwa na kampuni, kampuni ni kitu kingine, kampuni ina mmiliki, sio wamiliki, share holder wote hata kama wako mia bado POWER IF ATTONEY inamtambua mmoja tu na ndiye mwenye dhamana ya kampuni.. kampuni ni mali ya mtu binafsi.. ieleweke.. chama au kikundi huundwa na katiba inayowapa wanachama wake equal play role ndani ya chama lakini kampuni linaundwa na memorundum inayommilikisha mmiliki uhalali wa kuexecute lolote na chochote muda wote ndani ya kampuni yake..
Jinsi ulivyomweleza Mwalimu hapo imedhihirisha hujui unalosema. Kikao gani hicho unachokizungumzia?
Nenda kajifunze kuhusu kufirisika kwa SUKITA kwanza.