Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Kuhusu hili, mimi nadhani serikali yetu bado ina vyonzo vingi sana vya mapato ambavyo haijaviexhaust. Kujiingiza kwenye legal battle ya kugombania mali za CCM itapoteza focus ya kuehaust vyanzo sustainbale vya mapato.

Let us focus kwenye kuachieve goals za vision 2025. Tukishatimiza vision 2025 tunajua hata nchi ikitoka mikononi mwa CCM kutakuwa na backup mechanism za kuhakikisha inaendelea kuwa stable. Sasa hivi hali ilivyo kuikabidhi nchi kwa rookies ni sawa na kuidumbukiza kwenye bubble ambayo inaweza kupasuka anytime!

Kwahiyo masuala ya mali za CCM tusiruhusu yatupotezee malengo.
"Vyanzo suistanable vya mapato"?mapato ya nani na kwa faida ya nani?
 
ZeMarcopolo,

..hizo siyo mali za CCM, ni mali za umma kwasababu zilipatikana wakati wa mfumo wa chama kimoja.

..pia katika kipindi hicho haikuwa jambo la ajabu CCM kuchotewa mapesa kutoka HAZINA.

..tulipoingia ktk mfumo wa vyama vingi, mali hizo zilipaswa kuchukuliwa na serikali.

..labda utueleze ni nini mantiki na uhalali wa CCM kuhodhi mali zilizopatikana wakati wa mfumo wa cham kimoja, chama kushika hatamu??

cc: Mwigulu Nchemba, Zitto, Chris Lukosi, Edwin Mtei, Dr.W.Slaa
Ndo maana wenzetu ie US everything is under the Federal govt.Aje democrat,aje republican haijalishi.

Haya ya ccm kuwa na kampuni ukweli sikuwa nafahamu,tena hiyo sukita ndo kabisa sikujuwa.Nakumbuka watu walikuwa wanapiga mikwanja mirefu tu.

Watu waliokuwa hiyo sukita wakipiga madeal tu na kuvuta mikwanja lakini tukawa tunawaona wajanja(kasumba yetu mbaya).Kumbe yalikuwa ni maccm.

ccm ni chama kibaya sana.Hata kikiondolewa madarakani inabidi kifanyiwe uchunguzi na waliohusika kulifilisi hili taifa wawajibishwe bila kusita.Halafu pia iangaliwe kama kuna haja ya kukifuta.Ni chama kinachorepresent every failure in our country.
 
Nilikuwa bado na mawazo mgando kuwa CCM ni chama cha kisiasa kumbe La! Sasa hii JITEGEMEE kampuni inayojishughulisha na biashara ya kuuza NYARA za Taifa! Tembo wetu watasalia?...

Hivi wakati tulipokuwa tunaingia kwenye mchakato wa vyama vingi? si ilitakiwa MALI zote zilizokuwa chini ya mfumo wa chama kimoja ambayo watanzania tulichangia ama kwa kupenda ama kulazimishwa vilipashwa kurudishwa serikalini zikiwemo mashule, viwanja vya michezo, Sukita kama walivyo fanya Ghana?

...Wanasheria wa humu JF tusaidieni kujua kama sheria inaruhusu kwenda mahakamani kudai mali zetu zinazochezewa na hawa Mafisadi....
 
Mkuu JokaKuu,
Nadhani hili nawajibika kulijibu peke yake ili nieleweke vizuri.
Mzee Mtei ni mmiliki wa chadema. Kila kinachosimamiwa na chadema kimetoka kwa Mtei.
Chadema imekuwa ikitoa kauli ya kukejeli harakati za kupigania Uhuru. Wanasema Uhuru haujapatikana na kwamba Tanzania sasa hivi iko chini ya "mkoloni mweusi". Hizi ni kauli zinazotolewa na viongozi wa Kamati Kuu ya chadema wakiwa pamoja na Mtei. Ndio maana swala la kuhoji mchango wa Mzee Mtei kwenye kupigania Uhuru ni la muhimu. Kama Mzee Mtei anaona Uhuru uliopiganiwa na TANU na ASP sio Uhuru kamili, je ni jitihada gani alifanya ili nchi ipate Uhuru kamili? au alikuwa anangoja mpaka siku atakapokuwa na pesa za kumiliki chama cha siasa ndio aanze kutambua umuhimu wa Uhuru huo?

Kukejeli Uhuru ni dharau kubwa sana kwa waasisi wa Taifa letu na personally siwezi kumuona mtu aliyekataa kushiriki katika harakati za Uhuru anakejeli Uhuru ulipiganiwa na watu waliokubali kuacha ajira zao kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kwahiyo KOSA la Mtei ni kudharau jitihada za waliopigania Uhuru wa nchi yetu.

CORRECTION: Mzee Mtei si mmiliki wa Chadema. Chadema is a movement, it is not a private company.
NB: Unamwitaje Kikwete? Mtu ambaye analeta wazungu walime na kuwaita waafrika waliobanduliwa kwenye maeneo hayo "watu wa pembezoni?" Mkoloni mweusi!
 
Joka Kuu, una roho ngumu Mkuu.. ZeMarcopolo? Butola? Chris Lukosi? mmh! Ninachofahamu ni kwamba leo Nape Nnauye kafanya kweli, kaacha watu wamepigwa butwaa!

Eti mafisadi walioshindikana kuvuliwa gamba, mafisadi ambao wakikamatwa serikali itayumba, mafisadi wanaoitetemesha dola...leo Nape anadai wanatoa siri kwa Chadema! Ameenda mbali na kuthibitisha kuwa Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, kwamba serikali imetuma tu maombi ya Joint Venture!

Kuna mtu hapa nadhani kachanganyikiwa, badala ya kutumia maji kuzima moto, anazidi kumwaga petroli...angekuwa hata na chembe cha akili angesubiri kidogo, hata kwa siku moja tu. Haya, yetu macho. Ndiyo imetoka hivyo tena kwa rangi kijani...Chadema inatisha. Siku ya kufa miti huteleza.
 
Mimi namshangaa huyu anayeona swala la Jitegemee co. kumilikiwa na CCM kuwa ni BIG NEWS. What is NEWS about it? au anataka tumtajie na shughuli nyingine za uzalishaji mali za CCM ikiwemo kutoa huduma za parking ambapo magari ya chadema mengi tu yanalala kwenye ofisi za CCM na kulipia.

Chifu, shughuli zote za uzalishaji mali za CCM zilizoanza enzi ya chama kimoja; na maeneo yote yaliyochini ya CCM, ambayo yalipatikana enzi ya chama dola, kimsingi si mali halali za CCM. Ni mali za taifa.

Ni suala la muda tu, yote yatarudi mikononi mwa wamiliki halali.
 
CCM NI WAFANYABIASHARA sema akili ya biashara hawana

Gaming Management (T) Limited,
Tanzania Green Limited
sasa wana hii JITEGEMEE TRADING COMPANYA, mamlaka ya bandari wanafanya makosa kushirikiana na ccm, sio wasimamizi wazuri hata wa mali zao

YUSSUF MANJI: Mfanyabiashara anayeonekana kuogopwa na wengi ndani ya utawala, amehusishwa na ukwapuaji wa fedha za EPA na katika uuzaji wa majengo kwa mashirika ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PSPF, yenye thamani ya jumla ya Sh. 83.5 bilioni.

Manji alikopa Sh. 9 bilioni kutoka NSSF na kujenga jengo ambalo aliiuzia NSSF tena kwa Sh. 47 bilioni (ikimaanisha amefanya biashara ya Sh. 38 bilioni chapchap) na wakati huohuo akaiuzia PSPF jengo hilo katika mazingira tata kwa Sh. 36 bilioni huku akiendelea kukaa katika jengo hilohilo bila kulipa kodi. PSPF wameamua kumfukuza.

Alikwepa kodi katika mauzo yote hayo hadi waliposhitakiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kupitia kampuni yake ya Quality Group Limited, Manji anadaiwa kuingiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkenge kwa kuchukua leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa iliyokuwa inamilikiwa na CCM.

Hadi sasa anadaiwa na kampuni ya CCM ya
Tanzania Green Limited, Dola za Marekani 50,000 ambazo zilitumika kulipia leseni kwenye Bodi ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania) 3 Mei 2004.

Hadi Bodi ya Bahati Nasibu inaifuta leseni ya bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni
iliyoanzishwa na CCM ya Gaming Management (T) Limited, Manji hakuwa amelipa fedha hizo.

Manji anatajwa katika kunufaika isivyo halali na mabilioni ya shilingi za misaada kutoka serikali ya Japan za Commodity Import Support (CIS).

 
Katika kitabu alichoandika mwenyewe Mzee Mtei hawezi kuelezea ugoi goi wake kwenye harakati za maendeleo ya nchi.

Ukisoma hizo position alizoipewa ZOTE zilikuwa ni ajira na alilipwa mapato manono na serikali kwa kodi za wananchi. Ukimwambia sasa hivi kijana mwenye masters degree kupewa kazi BoT ni kujitolea atakwambia tangaza hizo nafasi za kujitolea uone msururu wake.

Mzee Mtei alikuwa anaringa kwa sababu enzi hizo ni wachache walikuwa na elimu aliyokuwa nayo, ndio maana Nyerere alikuwa anambembeleza kwa namna mbalimbali ili akubali kuajiriwa na serikali. Kwahiyo Mtei alikuwa ni MUAJIRIWA wa serikali na alipoona ajira HAILIPI baada ya uchumi kuyumbishwa na vita vya Uganda AKAINGIA MITINI.

Kitendo cha Nyerere kumbembeleza Mtei kwa kumpa nafasi mbalimbali kisitafsiriwe vibaya. Mtei hakupewa nafasi hizo kwa sababu alikuwa mchapa kazi - HAPANA. Wenye elimu ya level yake walikuwa HAKUNA. Enzi hizo ukiwa na diploma unapewa Ukurugenzi Wizarani!

Rais wa awamu hii hana sababu ya kumbembeleza mtu kufanya kazi BoT kama enzi zile kwa sababu tayari nchi ina wasomi wengi. Mtu akiringa kama alivyokuwa Mtei anachukuliwa mwingine.

Cha ajabu Mzee Mtei amekuwa miongni mwa watu waliochochea kumshawishi Mnyika aache chuo na kujikita kwenye shughuli za chadema. Yeye anasema hakutataka kusaidia harakati za Uhuru kwa sababu alikuwa busy na masomo ya chuo kikuu.

Nadhani unapata picha huyu ni mtu wa namna gani. Sasa hivi yuko busy kuwahasisha vijana wa elimu ya juu kuacha kuzingatia masomo yao na kujikita kwenye shughuli za CHASO na M4C wakati yeye wajukuu zake wanasoma Ulaya!
ZeMarcopolo,

..my friend u r all over the place, mara Mtei alikuwa anaringa, mara alikuwa anabembelezwa na Mwalimu Nyerere!! where do you get all this stuff from??

..Mtei alipojiuzulu uwaziri wa fedha moja kwa moja alikwenda kujikita kwenye ukulima wa kahawa. hivi kitendo hicho kweli unaweza kukiita "kuingia mitini."?? Hivi unataka kutueleza ktk hali ile ya uchumi tuliyokuwa ukulima wa kahawa ulikuwa ajira ya uhakika kuliko uwaziri wa fedha.

..Hivi unapata faida gani kusema uongo, kuzusha, na kuchafua rekodi za watu namna hii? Hivi kweli uko serious unaposema Mzee Mtei alikuwa goi goi ktk kushughulikia majukumu yake na kusukuma gurudumu la maendeleo la nchi hii?? Waziri wa Fedha wakati wa vita ya Kagera kwa maoni yako ni goi goi??

..Kuhusu elimu za watumishi wa serikali wakati tunapata uhuru, ni kweli kabisa walikuwa hawana elimu kubwa kubwa kama walizonazo watumishi wa siku hizi. Lakini naweza kusema mapungufu hayo ya kielimu yalifichwa na uzalendo na uadilifu wao. Leo hii tuna watumishi wamesoma kwelikweli lakini uadilifu ni zero na ndiyo maana mnaona nchi imekwama haiendelei.

..Uadilifu na uchapakazi wa Mzee Mtei ndiyo uliomuwezesha kuteuliwa gavana wa bot, PS wizara ya fedha, Katibu Mkuu EAC, waziri wa fedha, Mkurugenzi IMF, na mwenyekiti wa tume iliyopelekea kuundwa kwa TRA.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JokaKuu,
Nadhani hili nawajibika kulijibu peke yake ili nieleweke vizuri.
Mzee Mtei ni mmiliki wa chadema. Kila kinachosimamiwa na chadema kimetoka kwa Mtei.
Chadema imekuwa ikitoa kauli ya kukejeli harakati za kupigania Uhuru. Wanasema Uhuru haujapatikana na kwamba Tanzania sasa hivi iko chini ya "mkoloni mweusi". Hizi ni kauli zinazotolewa na viongozi wa Kamati Kuu ya chadema wakiwa pamoja na Mtei. Ndio maana swala la kuhoji mchango wa Mzee Mtei kwenye kupigania Uhuru ni la muhimu. Kama Mzee Mtei anaona Uhuru uliopiganiwa na TANU na ASP sio Uhuru kamili, je ni jitihada gani alifanya ili nchi ipate Uhuru kamili? au alikuwa anangoja mpaka siku atakapokuwa na pesa za kumiliki chama cha siasa ndio aanze kutambua umuhimu wa Uhuru huo?

Kukejeli Uhuru ni dharau kubwa sana kwa waasisi wa Taifa letu na personally siwezi kumuona mtu aliyekataa kushiriki katika harakati za Uhuru anakejeli Uhuru ulipiganiwa na watu waliokubali kuacha ajira zao kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kwahiyo KOSA la Mtei ni kudharau jitihada za waliopigania Uhuru wa nchi yetu.
ZeMarcopolo,

..nimekuuliza mbona Mkapa na Malecela walikuwa masomoni wakati wa harakati za uhuru lakini huwapigii kelele?

..CDM wanasema nchi iko chini ya mkoloni mweusi kutokana na dhuluma zinazoendelea chini ya utawala wa CCM.

..hii hoja ni rahisi sana kuielewa, nadhani tatizo lako ni lilelile la kujaribu kupotosha watu kwamba CDM wamekashifu harakati za uhuru.

..CCM msitegemee kubakia madarakani kwa hoja za kilaghai. Salama yenu ipo ktk kutatua kero za wananchi, tatizo ni kwamba mko too busy kuchafua vyama vya upinzani. These to me a signs of desperation.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JokaKuu,
Nadhani hili nawajibika kulijibu peke yake ili nieleweke vizuri.
Mzee Mtei ni mmiliki wa chadema. Kila kinachosimamiwa na chadema kimetoka kwa Mtei.
Chadema imekuwa ikitoa kauli ya kukejeli harakati za kupigania Uhuru. Wanasema Uhuru haujapatikana na kwamba Tanzania sasa hivi iko chini ya "mkoloni mweusi". Hizi ni kauli zinazotolewa na viongozi wa Kamati Kuu ya chadema wakiwa pamoja na Mtei. Ndio maana swala la kuhoji mchango wa Mzee Mtei kwenye kupigania Uhuru ni la muhimu. Kama Mzee Mtei anaona Uhuru uliopiganiwa na TANU na ASP sio Uhuru kamili, je ni jitihada gani alifanya ili nchi ipate Uhuru kamili? au alikuwa anangoja mpaka siku atakapokuwa na pesa za kumiliki chama cha siasa ndio aanze kutambua umuhimu wa Uhuru huo?

Kukejeli Uhuru ni dharau kubwa sana kwa waasisi wa Taifa letu na personally siwezi kumuona mtu aliyekataa kushiriki katika harakati za Uhuru anakejeli Uhuru ulipiganiwa na watu waliokubali kuacha ajira zao kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Kwahiyo KOSA la Mtei ni kudharau jitihada za waliopigania Uhuru wa nchi yetu.
ZeMarcopolo,

..nimekuuliza mbona Mkapa na Malecela walikuwa masomoni wakati wa harakati za uhuru lakini huwapigii kelele?

..CDM wanasema nchi iko chini ya mkoloni mweusi kutokana na dhuluma zinazoendelea chini ya utawala wa CCM.

..hii hoja ni rahisi sana kuielewa, nadhani tatizo lako ni lilelile la kujaribu kupotosha watu kwamba CDM wamekashifu harakati za uhuru.

..CCM msitegemee kubakia madarakani kwa hoja za kilaghai. Salama yenu ipo ktk kutatua kero za wananchi, tatizo ni kwamba mko too busy kuchafua vyama vya upinzani. These to me a signs of desperation.
 
Last edited by a moderator:
Nape, tatizo unakurupuka bila kujua nini kinaendelea ,

1. Ni kuwa kwenye kikao cha mamlaka ya Bandari kilichoketimwezi Machi tayari walishatenga fedha kiasi cha shilingi bilioni kumi za kitanzania kwa ajili ya kuwalipa CCM na baadhi ya wajumbe walipinga sula hilo kwa hoja kuwa hapakuwa na tenda wala utaratibu uliofuatwa ili kuipatia kampuni hiyo ya CCM tenda , kampuni hii inasimamiwa na Peter MAchunde, Sam Mapande et al, na ndio inajenga ukumbi wa kisasa kule Dodoma ( Jitegemee)

2. Chadema , haiwezi kukaa kimya tena mpaka yatokee yale ya Deep Green , Tangold na wenzake ambao unawajua vizuri, sasa kila hatua itafuatiliwa kikamilifu kuelekea 2015 kwani Chadema wanajua kuwa tangu 1995 mmekuwa mkijichotea fedha za walipa kodi kwa ajili ya chaguzi kama ifuatavyo,

1995 ......Zimbabwe na Malaysia kwa IPTL .....Waliofanikisha dili hilo ni Marehemu Kolimba na Abdalah Kigoda.

2000....... Aggreko, Wartsila, Barrick Gold et all

2005....... BOT kupitia Tangold, Deep Green, Meremeta, wahusika wakuu humu walikuwa Chenge, GRey Mgonja,IMMA Advocates ,et all

2010...... Elections mnajua mlivyochota Hazina, zikaenda Canada kuchapisha mabango, hamkulipia kodi magari bandarini nk.......

2015 ...... Mmeanza na Bandari, Mikataba ya Kichina 17 etc


Yapo mengi nafikiri ni suala la muda tuu.....

and add it in 2015 China is going to print all ballot papers free of charge. Kinana has started working on this; CCM are thugs whom you don't need to underestimate. They are at all the time advanced on fraud!
 
Nape msijifiche chini ya mwavuli wa PPP, Kumbuka hata hiyo PPP ilipitishwa bungeni kwa mbinde na ilikuwa ni njama ya magamba kuendelea kuitafuna nchi kupitia PPP.

Je unajua ni viongozi wangapi wenye hisa kwenye makampuni mengi na mikataba mingi kwa mgongo wa PPP, hata kwa kupewa hisa tu ili kufanikisha dili hata kama hawajachangia mladi. Hapo mmenasa huo ni ufisadi mkubwa.
 
Intelijensia ya Chadema iko juu, Nape acha kuwahadaa watanzania labda uwahadae wadanganyika wa CCM!

Nasema Intelijensia ya Chadema iko juu kuliko ya polisi wa TZ na TISS ni kwamba Intelijensia inagundua michakato ya matukio ya kifisadi kabla hayajatokea na kuzuia yasitokee otherwise hiyo Intelligensia ni feki kama mchakato wa CCM wa kuvuana magamba! Chadema imegundua mipango ya kifisadi mapema na kuianika hadharani...kweli wanastahili kupongezwa na watanzania wote wenye fikra na utayari wa kukombolewa na ujinga wa CCM waliolishwa kwa kipindi cha miaka 51 tangu Uhuru!!!
 
...Wangehoji hiyo kampuni ni ya nani isingekuwa tatizo, tatizo wamesema kampuni hiyo imepewa "tenda" na bandari kifisadi, na kuulinganisha mchakato huo na ule wa Richmund, sasa ndugu yangu ebu angalia ulinganifu huo? ndio maana naamini Chadema wanapaswa kuongeza uhakiki wa taarifa zao kabla ya kuzitoa kwa umma, kukurupuka kutoa taarifa kisha zikabackfire kama hivi kunaweza kupunguza credibility ya chama....

Mkuu unaweza kuwa na hoja ya msingi ila hayo unayoyazungumza CDM wameyatake into consideration ila yawezekana muda ndo imekuwa shida.Ila kumbuka once biten......EPA,Richmond and the like ukifuatilia vizuri yawezekana CDM wamemwaga Maji wakati mpishi anaandaa Unga.CDM wamefanya kazi yao sasa tuvute subira mamlaka husika wafunguke
 
uko nchi gani?
Niko Tanzania, lakini sijawahi kumsikia NAPE akiwataja kwa mdomo wake zaidi ya kutamka kuna mafisadi, magamba lakini hakuna anayethubutu kuwataja.... INAWEZEKANA UNAYEMUWAZIA WEWE MKUWA NDIYE GAMBA/FISADI, KUMBE SIYO... TUMEACHWA WENYEWE TUAMUE NANI NI NANI... Usije shangaa mi nikawaza wewe ndo fisadi A.K.A GAMBA
 
Wewe ndio mbulula Bandari imeshindwa kutafuta viwanja maeneo mengi yalivyotapakaa,ila waliona kwenye Bonde karibu na mabwawa ya mavi na maji taka ya buguruni,Bondeni ambako mwaka jana tuu mvua zake zilisomba makontena kutoka kwenye yadi nyingi zilizo pembezoni mwa sukita,mbona huo ni ukosefu wa weredi kama TPA wanaweza kutaka kuweka mradi wa makontena pale wanapaswa nao kuulizwa intergrity ya hiyo mamlaka ya Bandari iko wapi,safari hii CCM wametangaziwa kiama na lazima wapelekwe nahka ya afrika mashariki,Arica ,The Hague kwa kukiuka haki za binadamu kwa kutumia mapato y nchi hovyo na kusababisha mfumuko wa bei
Pamoja na kukusanya trilioni 1.2. kwa mwezi bado fedha kwenye mzunguko haipo nina uhakika zinafichwa kwa ajili ya uchaguzi

....duh, so unadhani mahakama ya ICC ina deal na mambo ya Ufisadi?wewe kweli ni mbulula plus...
 
we nape sidhani kwamba kabla ya kuongea na kuandika unafanya vikao binafsi kichwani, manake unaropoka tuuu...!
Nina shaka na uwezo wako.....! think big like a man...!
 
Sasa kama mali za CCM ni za watanzania wote kwani kuna ubaya gani? CCM inatambua kuwa mali zake ni za watanzania wote na ndio maana inamkaribisha kila mtanzania kuwa mwanachama wa CCM na kugombea nafasi za uongozi. CCM ni chama kilichojengwa kwa nguvu za watanzania wote, ni tofauti na vyama vingine vilivyojengwa na pesa za familia moja ambayo baadae inahodhi nguvu zote za kufanya maamuzi.

CCM ni mali yako, ITUNZE...

Mkuu hizi mali zingekuwa zinanufaisha watanzania wote tusingekuwa tuna watanzania wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Mali hizo zinanufaisha wachache SSM na watoto wao ndiyo maana hata vyeo mnapeana. Wanachama walala hoi ssm wanatumika kama bendera fuata upepo tu kushabikia mikutano na kampeni lakini maisha yao ya kimaskini yapo pale pale. Sana sana pesa hizo mnatumia kukodi mabasi na pikipiki wakati wa kampeni na publicity materials nyingi ambazo hazimsaidii mlala hoi.

Kama kweli mnapendwa mbona mnatumia nguvu kubwa hivyo ya publicity? At the same time dola kwa sana? Nilifurahiswa mwenyekiti wenu alivyo sema ...tutumie njia imara na sahihi kujiimarisha, tutaendelea kutumia polisi hadi lini?........" rejea alisema live na vyombo vya habari vilimnukuu!!!

Finally, hata kama vyama vyote vya upinzania vitakufa sitaweza kujiunga SSM!!!! Hapa nilipo sina kadi ya chama chochote cha Siasa ila mimi ni mpiga kura mzuri sana kwa kiongozi yeyote anayenifaa mitaani kwetu, kijimbo na kitaifa bila kujali anatoka chama gani. Kwa mfano diwami wangu anatoka SSM na nilimpigia kura only kwa kuwa wagombea kutoka vyama vingine walikuwa wrong appointed. Mbunge wangu CDM.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013

Mkuu Ngalikihinja naona umesahau?
Nape aliwahi kuwataja Mafisadi na alitaja jina la E.N.Lowasa na Manji kuwa waliusika na ufisadi wa mikataba ya upangaji ardhi na majengo mali ya UVCCM. Kwa kuwa UFISADI ni dini ya CCM Makamba alimfuta uanachama. Alipotubu alisamehewa na kupewa u-DC Masasi. baadae aliokoka na sasa ni muumini mzuri wa UFISADI dini rasimi ya CCM.
 
Back
Top Bottom