ZeMarcopolo,
..mimi nadhani tulichagize bunge letu lenye CCM majority waongozwe na uadilifu kupitisha sheria itakayorudisha serikalini mali zilizoporwa na CCM.
..hizi habari za Mzee Mtei umezitoa wapi? Mzee Mtei ameandika kitabu kuhusu maisha yake, sasa humo unaweza kupata taarifa sahihi kuhusu mchango wake akiwa serikalini.
..Mzee Mtei alitofautiana na bosi wake, wakati huo Mwalimu Nyerere, kuhusu hatua za kuchukua kunusuru uchumi wetu uliokuwa umeyumba kutokana na vita vya kagera. Kutokana na tofauti hizo Mzee Mtei alijiuzulu wadhifa wa waziri wa fedha kwa heshima zote, na Mwalimu Nyerere alikubaliana na uamuzi huo.
..kutokana na ukweli kwamba Mzee Mtei hakuondoka serikali akiwa na rekodi mbaya, Mwalimu Nyerere alimteua kuwa mwenyekiti wa bodi ya TDFL. Baadaye tena Mwalimu Nyerere alipendekeza jina la Mtei kwenda kuwa mkuu wa Idara ya Afrika ktk shirika la fedha la kimataifa IMF. Mtanzania mwingine aliyepata kushika nafasi hiyo ni Peter Ngumbulu ambaye alipendekezwa na Raisi Mkapa.
..baada ya kutumikia IMF, Mzee Mtei alirudi Tanzania na kuteuliwa na Raisi Mwinyi kuongoza Tume ya Raisi ya kurekebisha mfumo wetu wa kodi, ushuru, na forodha. Ripoti ya Tume ya Mtei ndiyo iliyotoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa TRA.
..kwa hiyo mpaka hapo kazi ya Mzee Mtei inaonekana ktk vyombo vyetu vya fedha kama BENKI KUU na MAMLAKA YA MAPATO.
..ZeMarcopolo, huko unakotaka kwenda siko ndugu yangu. Mwananchi kutumikia ktk serikali ya mkoloni, au kutokushiriki waziwazi ktk harakati za uhuru wa Tanganyika haimaanishi kwamba waliunga mkono ukoloni.
..Mimi binafsi Mzee wangu alitumikia ktk serikali ya mkoloni. Baada ya uhuru ametukia serikali yake na kustaafu bila matatizo yoyote yale ya kimaadili. Pamoja na hayo sijawahi hata mara moja kumshuku au kumtuhumu kwa kukosa uzalendo.
..Umezungumzia vita vya Kagera, na hapo umenikumbusha Jeshi letu la wananchi wa Tanzania. Hivi unaelewa kwamba Mirisho Sarakikya mwanzilishi wa JWTZ alipata kutumikia King's African Rifles?? Unafahamu kwamba Abdalah Twalipo, David Musuguri, Ernest Mwita Kiaro, wote walikuwa askari kwenye jeshi la mkoloni. Mbona wazee wetu hao waliokuja kuongoza jeshi letu na vita kwa ushujaa na uadilifu usio na mfano.
..Fitina hizi unazomtupia Mzee Mtei kosa lake haswa ni nini? Je, kwasababu tu ni mwana CDM ndiyo unataka kupuuza mchango wake ktk nchi hii??
cc:
Jasusi,
Dr.W.Slaa,
Tumaini Makene