Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Mkuu Hata EPA ilikuwa hivyo hivyo tofauti tu ile walitumia kampuni za watu hii wameamua kuanzisha kampuni yao kabisa kweli ukistaajabu ya CCM utavuna mabua.

Wanataka kukomba tena kama walivyofanya wakati wa EPA na wanaandaa mazingara ya kufanya hivyo kwa kumuhusisha gavana wa BOT kwenye mikutano yao ya ndani!!
 
Heshima kwenu wanabodi,

Jana kuna uzi ulianzishwa hapa JF ambao una husu JITEGEMEE TRADING COMPANY LTD ambayo imepatiwa zabuni TPA yenye thamani ya 10 bili.Swali ambalo lilikuwa linagonga vichwa vya wanadau ni mchakato wa upatikanaji wa tenda au zabuni hiyo. Swali la pili likuwa ni nani mmiliki wa hiyo kampuni. Hatimaye leo Nape kupitia Press release yake amethibitisha kuwa kampuni tajwa inamilikiwa na CCM. kusoma hiyo Pres release gonga hapa.
Scribd

Naomba kuwasilisha
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013


“Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na Sheria na si kwa akili zao wenyewe.”

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyasema haya wakati akihimiza Watanzania kulinda Katiba na sheria za nchi.
 
Wanataka kukomba tena kama walivyofanya wakati wa EPA na wanaandaa mazingara ya kufanya hivyo kwa kumuhusisha gavana wa BOT kwenye mikutano yao ya ndani!!

mkuu haya yanayotokea yana neema za mungu akijaribu kutuangazia na kutufungua macho tuone ni jinsi gani ccm wanavyoitafuna hii nchi.
 
Mkuu usimtukane mtu usiye mjua.Kwani mlishawakutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mnamiliki hiyo kampuni? Kosa langu nikutofahamu kuwa CCM wanamiliki hiyo kampuni?Behave. nasiyo kila anayeandika kitu hapa ni Bavicha.

Mwambie huyo gamba. Hajui siye wengine bado ni TANU Youth League tunasubiri Nyerere afufuke nayo...ebo!!
 
we mjamaa kwa kupenda sifa, sasa namba zako za simu unatuwekea ili iweje, tukurushie vocha ili uzidi kupiga umbea

Tuna safari ndefu sana.
Akili za namna hii huku kwenye vijiwe vya mitandaoni ni tatizo.
Kama huyu ndo akili yake hii, je wale wa kule Kambi Katoto na Lupa Tingatinga watakuaje?
 
Nnape aache kuwarubuni Watanzania.
Nnape anawaambia nini Watanzania kuhusu kitu kinachoitwa CONFILICT OF INTEREST between CCM and CCM Government???

Kama Nnape amepata ujasiri wa kukiri kuwa Jitegemee Trading Co. Ltd ni ya CCM, basi aweke wazi pia kuhusu Makampuni yafuatayo ambayo ni ya CCM:

  1. KAGODA LTD.
  2. DEEP GREEN.
  3. MEREMETA.

Makampuni haya ndiyo yaliyotumika kuhamisha pesa toka BOT kwenye scandal ya EPA ambayo ilihusisha vigogo wengi wa CCM walioingia kwenye LIST OF SHAME!

Ukweli unabaki palepale kwamba Chama Tawala hakiwezi kuingia MKATABA WA KIBIASHARA NA SERIKALI. Hakuna Biashara kama hiyo popote duniani. Sheria ya Manunuzi kulingana na PPRA hairuhusu kitu kama hicho.

Hapa lazima kuna UFISADI unaotengenezwa kati ya CCM na Serikali yake. Najua CCM wameshaanza kutafuta pesa za Kuhonga kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015!
 
We kweli mshamba. Yani hujui kuwa CCM imekuwa na shughuli za uzalishaji mali tangu enzi za SUKITA?

Nyinyi vijana wa juzijuzi wa bavicha mna matatizo sana.

Wewe ZeMarcopolo acha hizo. Mali zote mnazodai ni za SSM ni za watanzania wote, wale wa SSM na wa vyama vya upinzani. Imefika mahali sasa tugawane hizo mali. Hata ndoa zikivunjika wanagawana mali walizochuma pamoja. Watanzania wanataka mali zao. Hizo kampuni kama zile za Deep Green si ndizo mnafisadi nazo? Meremeta!! You name all!!! Kwa hiyo usitake kulaumu eti vijana wa Bawacha!! Kuna wazee kama sisi tuna taarifa zote.
 
Hakuna kitu huwa kinanikera kama kuambiwa hiki ama kile ni mali ya CCM. Kinawezaje kuwa ni mali ya CCM ilihali vilichumwa na umma wote wa watanzania wakati wa mfumo wa chama kimoja? Tukiwa wanachama wa vijana chipukizi wakati huo na pia umoja wa vijana tumeshiriki kwa hali na mali kujenga hivi vyote ambavyo leo CCM wanajivunia kuwa ni vya kwao. Kwa hakika upinzani ukichukua nchi, hivi vyote viuzwe tugawane. Huu ni uhuni, wanajivuniaje tulivyovitolea jasho sisi wote.
 
cha kushangaza ni pale wanapomuunga mkono Lowassa na kumzushia Msafi wa wasafi.
Hatakama mimi ni cdm kwa hapa ninapatwa na kichefuchefu.
Labda waeleze kwamba sio wanachadema walioandika ile thread ya kumkubali Lowassa ambaye hata yeye mwenyewe anajijua kuwa ni mchafu kuliko hata choo.

Kwahiyo nyie mnaona ni sawa tu CCM ikianza kufanya biashara na serikali yake! Inatosha CCM mmetuingiza kwenye udini, msiharibu hata utaratibu wa heshima ya utawala, huo ni mgongano wa maslahi chama tawala kuanza kufanya biashara na serikali ambayo inaiongoza, ni mtu mchovu wa fikra ndie anaweza kuunga mkono aina hii ya uongozi! Mwakymbe hakutangazwa kuwa mtakatifu yeye bado ni binadamu akikosea lazima tumwambie! Nape amekiri kuwa kampuni ni yao na wako kwenye mchakato wa kuipata hiyo tender now what are you complaining about!
 
Nchi tajengwa na wenye moyo na italiwa na wenye meno...

Paka akibanua kwenye kona anakuwa mkali kuliko chui>>> nape na maneno yaliyojaa hasira na chuki yanatoka wapi, kama ni kukanusha hoja ongea kama mwanasiasa aliyekomaa na sio kuropoka ...hizi ni dalili za mwisho kwa ccm
 
Paka akibanua kwenye kona anakuwa mkali kuliko chui>>> nape na maneno yaliyojaa hasira na chuki yanatoka wapi, kama ni kukanusha hoja ongea kama mwanasiasa aliyekomaa na sio kuropoka ...hizi ni dalili za mwisho kwa ccm
 
Kweli ulevi wa madaraka ni mbaya sana. Hivi huyo Nepi haoni a conflict of interest kwa kampuni inayomilikiwa na "chama twawala" kushiriki kwenye mchakato wa zabuni na kampuni binafsi!!!! Katika mazingira ya rushwa na ufisadi yaliyopo mchakato huo unawezaje kuwa fair?!? Huyu Nepi haoni hilo!!! Au ni umbururu wa akili uliokolezwa na jeuri ya kifisadi!!! Anyway, hawa watu siku zao zipo ukingoni na niseme waziwazi hapa kwamba jeuri hiyo na Nepi ni mojawapo ya vichocheo vya wananchi kuendelea kuchukia hiki chama kinachochungulia kaburi.Nawashukuru cdm kwa kuibua suala hili linaloonyesha sura halisi ya ccm.
...angalia mkuu isijekuwa wewe ndio ukawa mbulula kwenye hili,......ebu pata facts vizuri, hiyo kampuni "Jitegemee" haijaomba zabuni Bandari, bali bandari ndio wameomba watumie kiwanja cha kampuni hiyo ya "Jitegemee", kama kuna hatari ya mchakato kutokuwa fair ni kwa sababu kuna hofu namna gani kampuni hiyo ya CCM itawatendea haki "makampuni mengine" yanayokitaka kiwanja hicho sasa baada ya "taasisi ya serikali, Bandari" nao kuomba kukitumia kiwanja hicho,....
 
Nnape aache kuwarubuni Watanzania.
Nnape anawaambia nini Watanzania kuhusu kitu kinachoitwa CONFILICT OF INTEREST between CCM and CCM Government???

Kama Nnape amepata ujasiri wa kukiri kuwa Jitegemee Trading Co. Ltd ni ya CCM, basi aweke wazi pia kuhusu Makampuni yafuatayo ambayo ni ya CCM:

  1. KAGODA LTD.
  2. DEEP GREEN.
  3. MEREMETA.

Makampuni haya ndiyo yaliyotumika kuhamisha pesa toka BOT kwenye scandal ya EPA ambayo ilihusisha vigogo wengi wa CCM walioingia kwenye LIST OF SHAME!

Ukweli unabaki palepale kwamba Chama Tawala hakiwezi kuingia MKATABA WA KIBIASHARA NA SERIKALI. Hakuna Biashara kama hiyo popote duniani. Sheria ya Manunuzi kulingana na PPRA hairuhusu kitu kama hicho.

Hapa lazima kuna UFISADI unaotengenezwa kati ya CCM na Serikali yake. Najua CCM wameshaanza kutafuta pesa za Kuhonga kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015!

mkuu ukitaka kuthibitisha hayo unayoyasema ccm wa kijarida chao kinaitwa uhuru mteja mkubwa wa uhuru ni serikali kupitia mawizara,wakala na taasisi zake.hili lilifanyika baada ya kuona linakufa kupitia sekula ikiwalazimisha wizara kununua gazeti la uhuru
 
We kweli mshamba. Yani hujui kuwa CCM imekuwa na shughuli za uzalishaji mali tangu enzi za SUKITA?

Nyinyi vijana wa juzijuzi wa bavicha mna matatizo sana.

Hizo mali hazikuwa za CCM. Usitake kutudanganya. mali hizo ni za waTanzania wote. Kwa umoja wetu tulizichangia kwa kukatwa mishahara ili kuanzisha vitega uchumi vyote vinavyo daiwa kwamba ni vya CCM. Mali zote zilitakiwa kuwa chini ya serikali baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Ni jambo la kushashangaza kwamba, maeneo mengine hata vituo vya mabasi vinamilikiwa na CCM. Maeneo haya yalikuwa chini ya Halimashauri za Wilaya lakini leo hii eti ni mali za CCM. Mja asili haachi asili. Ndio maana hata leo laana ya kudhulumu bado mnaiendeleza ndani ya nchi hii. Ufisadi umetamalaki kila pembe ya Tanzania.

Tunajuwa kwamba muda utafika na siku moja mali hizo zitakuwa ni za waTanzania wote. Na hili ndilo CCM inalo liogopa na kuhakikisha kwamba, kwa namna yoyote ile, demokrasia na uhuru wa kweli unagandamizwa kwa waTanzania wataka mabadiliko.

"HE WHO LOUGHT LAST LOUGHT LONGEST".
 
Butola Kosa la CDM liko wapi? kuhoji uhalali na nani mmiliki wa hiyo coy ni kosa? Hivi wewe ulikuwa unajua kuwa ccm inamiliki kampuni inayoitwa Jitegemee Trading Company ikiwa ni mbadala wa SUKITA?Information is power mkuu
...Wangehoji hiyo kampuni ni ya nani isingekuwa tatizo, tatizo wamesema kampuni hiyo imepewa "tenda" na bandari kifisadi, na kuulinganisha mchakato huo na ule wa Richmund, sasa ndugu yangu ebu angalia ulinganifu huo? ndio maana naamini Chadema wanapaswa kuongeza uhakiki wa taarifa zao kabla ya kuzitoa kwa umma, kukurupuka kutoa taarifa kisha zikabackfire kama hivi kunaweza kupunguza credibility ya chama....
 
Samahani kaswali ka uzushi: ETI MAFISADI AMA FISADI HUWA ANAPATIKANA WAPI? AMA TAASISI GANI? WAPI ANAFANYA HUO UFISADI WENYEWE? ANSWER PLEASE
CC: Mapilili, Henge, Bongolala, Nyambu et all................
 
Tatizo lako hujui maana ya trustees. Unataka nianze kuandika vitu hata ambavyo sitakiwi kuandika.

Kuhusu hiyo tenda unayozungumzia, taarifa iliyotoka inasema HAKUNA tenda. Kinachofanyika ni majadiliano ya uwezekano wa PPP na majadiliano hayo bado yako kwenye hatua za awali sana.

Hapo kwenye red. Kwahiyo majadiliano yakiisha na wakawa wamekubaliana, ndio watangaze tenda!!!!!! (ridiculous)
 
Dr Mwakyembe nakuamini sana na naelewa kuwa unatambuwa kuwa watanzania wapo nyuma yako,kama kiwanja ni mali ya CCM hiyo haina shida ni kiwanja chao na hakuna atakaweza kuwaingilia ktk hili.
cha msingi hapa ni wewe Dr Mwakyembe kusimamia misingi na usikubali kuyumbishwa,tayari kazi yako inaonekana na watanzania wanafaidi matunda ya uwepo wako kama waziri wa uchukuzi,simamia misingi na epuka mafisadi kwani unaelewa nini walitaka kukifanya kwako,katu usiwape nafasi.
 
Back
Top Bottom