Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

CCM hakikisheni hamtoki madarakani kwa haya mnayoyafanya! la mkitka ndo utakuwa mwisho wenu! sidhani kama uwezo wa kushindana na nguvu ya umma mnao! Nape amegeuka kuwa mtetezi wa uozo wa maadili ndani ya hii nchi! Bila aibu anatetea CCM KUFANYA BIASHARA NA SERIKALI YAKE INAYOIONGOZA CCM inalipeleka wapi hili taifa?
 

Mkuu Ngalikihinja naona umesahau?
Nape aliwahi kuwataja Mafisadi na alitaja jina la E.N.Lowasa na Manji kuwa waliusika na ufisadi wa mikataba ya upangaji ardhi na majengo mali ya UVCCM. Kwa kuwa UFISADI ni dini ya CCM Makamba alimfuta uanachama. Alipotubu alisamehewa na kupewa u-DC Masasi. baadae aliokoka na sasa ni muumini mzuri wa UFISADI dini rasimi ya CCM.

CCM bado wanadhani watanzania tuna short memory! hatusau kwasasa hata kikombe cha babu wa Loliondo hakikuweza kufuta kumbukumbu zetu!
 
matunda yapi tunafaidika watanzania kwa uongozi wa mwakyembe? Kama wewe unafaidika siyo watu wote mkuu wangu!
we ndio mmoja wa wale waliokuwa wakituibia pale bandari nini? Maana mlikuwa mkifaidi nyie na watoto wenu tu,sasa mmetimuliwa mnaanza kumwona waziri mbaya,hivi huoni aibu kutumia kitu cha umma kwa manufaa yako,familia na jamaa zako?
Nitaendelea kumpongeza waziri kwa kupambana na nyie mliokuwa mkitudhurumu pale bandari,makontena yanapotea kama kanga,nyie watu wabaya sana.ingekuwa ni china ni kunyongwa tu.
 
Nilipoona Dr.Mwakyembe kakubali unaibu waziri nikajua wameshammaliza,na kweli sumu,ufisadi yumo.Wizara inaenda kununua au kukodisha eneo la bandari kwa tsh10bn?jee bodi inafanya kazi gani?kikao cha baraza la mawaziri ni wanaCCM,muuzaji CCM.Ndio maana hata wauza dizeli wanakua na kiburi kwa kuwa vituo ni vya CCM
 
CCM hakikisheni hamtoki madarakani kwa haya mnayoyafanya! la mkitka ndo utakuwa mwisho wenu! sidhani kama uwezo wa kushindana na nguvu ya umma mnao! Nape amegeuka kuwa mtetezi wa uozo wa maadili ndani ya hii nchi! Bila aibu anatetea CCM KUFANYA BIASHARA NA SERIKALI YAKE INAYOIONGOZA CCM inalipeleka wapi hili taifa?

CCM ni disaster; sioni kwa nini Chadema wanashindwa kuteka ngome zote za CCM, sidhani kama CCM wana chochote kilichobaki besides ku-create divison kwa wananchi ili wazidi kutawala. CCM is [holding] a time bomb, which gonna burst any time..
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013

hapo nilipohighlight niambie kiongozi gani wa CCM ANAUWEZO WA KUFIKIRI???KWA TYPE YAKO????
 
Nimepelekewa rasmi nakala ya thread hii, pamoja na kauli au msimamo kuwa CCM walitumia fedha za Serikali kujenga au kuendeleza miradi ya chama wakati wa mfumo wa chama kimoja. Kwa mantiki hiyo, mali hizo zinabidi zigawiwe kwa vyama vya siasa baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Huo ni msimamo wenye mantiki kabisa, na kuanzia mwaka 1992 mfumo wa Vyama vingi vya siasa ulipoidhinishwa kikatiba, mimi binafsi nimekuwa nikisema CCM wana unfair advantage kwa kutumia mali za umma ambapo vyama vingine vya siasa hawavitumii.

Hata hivyo kutokana na ukweli kuwa ni vigumu kubuni (criteria) vigezo vya kugawa mali za CCM zilizotokana na fedha za Serikali , Umoja wa Vyama vya Upinzani ungekazania Bunge kwamba tupate Tume ya Wataalamu wanaojitegemea, labda wengi wao wakiwa si WaTz, ili watupe Formula. La sivyo Upinzani tutajikongoja na ufinyu wetu wa vyanzo vya mapato, hadi hapo CCM itakapotolewa madarakani.

Kwa hiyo tusubiri 2015. Formula ni lazima iambatane na idadi ya Watz. wanaounga mkono vyama hivyo vya siasa.
 
ibara ya ngapi inaruhusu ccm kufanya biashara na umiliki wake ukoje nani shareholdr/trustee
 
Haina tofauti na CEO aliyefukuzwa Tanesco(Mhando), Kuipa tender kampuni inayomilikiwa na Mke,yeye na watoto wake.Hongera Mwakyembe kuwaandikia barua walezi wako(ccm aka jitegemee trading),Kuwaomba ati mushirikiane kuendeleza eneo lao(NI UFISADI TU-mkataba utakuwawaje)
 
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amekiri kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amekipa chama chake mradi wa kifisadi wa mamilioni ya shilingi wa upanuzi wa eneo la bandari jijini Dar es Salaam, kinyume cha taratibu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Nape alisema ni kweli kuwa kampuni ya Jitegemee ni mali ya chama chake, na kwamba iko mbioni kuingia ubia na mamlaka ya bandari nchini (TPA) kwa ajili ya mradi wa maegesho; mradi ambao utatekelezwa katika eneo la Mto Msimbazi, Tabata, jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Nape imekuja siku moja baada ya Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila, kuanika kile kinachoitwa "Ufisadi wa Dk. Mwakyembe".

Kigaila alidai kuwa CHADEMA imepata nyaraka kadhaa zinazoonyesha Mwakyembe akishinikiza bodi ya TPA kujifunga katika mkataba wa kinyonyaji wa mamilioni ya shilingi na kampuni ya CCM ya Jitegemee Trading Company Limited ambayo ni mali ya CCM.

Nyaraka zinaonyesha katika mwaka huu wa fedha 2013/2014, serikali kupitia TPA imetenga kuilipa Jitegemee kiasi cha sh bilioni 10 kama malipo ya awali ya ujenzi wa eneo la mradi.

Aidha mamilioni hayo ya shilingi yanalipwa bila kutangazwa zabuni, kufanyika upembuzi yakinifu na bila kuwapo uchambuzi wa mradi iwapo kama utaingiza faida, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Wakati CHADEMA wakisisitiza kuwa mradi huo haukufuata taratibu, Nape alisema, "Wanachokiita wenzetu wa CHADEMA kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani ‘Joint Venture' kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika."

Hata hivyo, hii ni kawaida ya CCM kukana mikataba inayofungwa yenye harufu ya ufisadi. Mwaka 2008, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alikana kuingia mkataba wa aina hii katika jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), lililoko Lumumba, Dar es Salaam.

Uchunguzi unaonyesha kuwa tayari mradi huo umepitishwa na bodi ya bandari na kuingizwa katika bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2013/ 2014, jambo ambalo linathibitisha kuwapo kwa mkataba.

Mradi wa Mwakyembe unafanyika kuikabidhi kazi ya maegesho kampuni ya CCM ambao unakwenda kinyume cha kusudio la mradi huo la kuondoa msongamano wa magari yanayosubiri kuingia bandarini katika Barabara ya Kurasini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya TPA, mradi uliohamishiwa Mto Msimbazi ulipangwa kufanyika katika eneo la Kurasini, na kwamba wadau wakuu wa usafirishaji waliupitia mradi huo katika bajeti ya mwaka 2010/2011.

CHADEMA inapinga mradi huo kwa kuwa umefanywa kinyume cha sheria na kwamba eneo lililotengwa halifai kwa matumizi hayo. Inasema eneo hilo liliwahi kufugwa nguruwe, lakini waliishia kusombwa na mafuriko.

Habari hii kwa hisani ya Tanzania Daima.


ANGALIZO:
Kama ilivyo mara nyingi, Tanzania Daima wanakuja na habari za kulisha maneno watu au taasisi kwa manufaa wanayoyajua wao kama kichwa cha habari kinavyodai.

Nape Nnauye amesema tofauti kabisa kwenye hii video na kusisitiza kuwa hakuna mkataba au makubaliano yaliyokubaliwa baina ya Jitegemee Trading co- na Mamlaka ya bandari nchini (TPA) tofauti na maombi ya Mamlaka ya bandari kavu kutaka kuwekeza katika eneo hilo kama walivyo wawekezaji wengine ambao pia wameomba kuwekeza.
Maelezo kamili yako kwenye video, anzia kuangalia katika dakika ya 5:40.

Hizi ndizo siasa za Tanzania. Nani kwa sasa aliyebaki wa kuaminiwa katika jamii kwa vile hata magazeti nayo yamekuwa kama wanasiasa huku makanisa yanakuwa ni kimbilio la matajiri wa kisiasa na kiuchumi.



 
Last edited by a moderator:
This is ludicrous news.

Read this news from Nipashe.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema madai kwamba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amekiuka masharti ya zabuni kwa kuipa Kampuni ya Jitegemee Trading Limited zabuni ya ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa na makontena, wenye thamani ya Sh. bilioni 10, kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma, ni ya uwongo uliotengenezwa na baadhi ya mafisadi na kuwalisha Chadema.

Madai hayo dhidi ya Waziri Mwakyembe, yalitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mkurugenzi wake wa Organaizesheni na Mafunzo, Singo Kigaila, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam juzi.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa madai hayo ya Chadema ni ya uwongo kwa kuwa hadi sasa hakuna mkataba wowote, ambao Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imekwishaingia na kampuni hiyo.

Hata hivyo, Nape alithibitisha kampuni hiyo pamoja na kiwanja, ambacho mradi huo unataka kujengwa, kuwa vyote ni mali ya CCM.

Alisema kiwanja hicho kilikombolewa kutoka zilizokuwa mali za Shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania (Sukita), ambalo pia lilikuwa kampuni ya CCM.

“Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote,” alisema Nape.
Alisema eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi, wakiwamo TPA na kwamba, masharti waliyopewa waombaji wote ni kupeleka mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

“Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo

Alisema pamoja na CCM kuimiliki, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa jumla.

Aliipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dk. Mwakyembe, hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam na kuwataka kutokatishwa tamaa na mafisadi wachache, badala yake wachape kazi kwa uzalendo waliouonyesha.
 
Nilichojifunza hapo ni kwamba maovu na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na ccm ni makusudi kwani pindi wanapoumbuliwa wanakataa kwanguvu zote mpaka mapovu yanawatoka puani angali ni kweli
 
Makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ni wapi Nape?

Hili swala si la CHADEMA tu badala yake tuipongeze kwa kutufumbulia macho kwa vitendo vya kuiua nchi kiuchumi kwa maslahi ya wachache.Nichukue fulsa hii kumwomba Mh.Mwakyembe akumbuke heshima aliyokwisha pewa na watanzania asianze kuchafua mikono yake.Daima simamia ukweli hata kama uko katika kundi la manyang'au ukweli utajidhihilisha.
 
Wapate wapi hela za kununulia kofia, kanga na tisheti?!!!!... Na bado makampuni mengi ya kihuni tutayaona kabla ya 2015!!!!
 
Nape kilaza tu hakuna maeneo mengine zaidi ya hayo? Mbona mnatuibia hv hv? Na hao mafisadi ni wapi hao unaoshindwa kuwataja? Ambao wapo ccm?
 
Nimepelekewa rasmi nakala ya thread hii, pamoja na kauli au msimamo kuwa CCM walitumia fedha za Serikali kujenga au kuendeleza miradi ya chama wakati wa mfumo wa chama kimoja. Kwa mantiki hiyo, mali hizo zinabidi zigawiwe kwa vyama vya siasa baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Huo ni msimamo wenye mantiki kabisa, na kuanzia mwaka 1992 mfumo wa Vyama vingi vya siasa ulipoidhinishwa kikatiba, mimi binafsi nimekuwa nikisema CCM wana unfair advantage kwa kutumia mali za umma ambapo vyama vingine vya siasa hawavitumii.

Hata hivyo kutokana na ukweli kuwa ni vigumu kubuni (criteria) vigezo vya kugawa mali za CCM zilizotokana na fedha za Serikali , Umoja wa Vyama vya Upinzani ungekazania Bunge kwamba tupate Tume ya Wataalamu wanaojitegemea, labda wengi wao wakiwa si WaTz, ili watupe Formula. La sivyo Upinzani tuatjikongoja na ufinyu wetu wa vyanzo vya mapato, hadi hapo CCM itakapotolewa madarakani.

Kwa hiyo tusubiri 2015. Formula ni lazima iambatane na idadi ya Watz. wanaounga mkono vyama hivyo vya siasa.

ahsante mzee kwa busara zako! Hakika historia mpya itaandikwa na jina lako kutukuzwa.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013
Ingekuwa vema kama Nape angefanya yafuatayo; kuwataja hao mafisadi anaodai wanashirikiana na chadema.pia aeleze uongo dhahili wa chadema katika suala hili. Kisha atueleze mwenyekiti wake anasimama wapi wakati wa kulinda maslahi; upande wa chama na kutelekeza maslahi ya nchi au upande wa serikali na hivyo kuwawajibisha watu anaowatuma kwa maslahi ya chama chake maana kitendo hiki kimefanywa na watu wanaofikiri vema kwa mujibu wa Nape. La mwisho nawashauri mods hapa JF kutoruhusu kuwa jukwaa la matusi kwani mtu kama Nape anapoandika kuwa wengine ni mbumbumbu ni kuonesha alivyo mtaalamu wa kutukana na asivyo na lugha ya ustaarabu.
 
Heshima kwenu wanabodi,

Jana kuna uzi ulianzishwa hapa JF ambao una husu JITEGEMEE TRADING COMPANY LTD ambayo imepatiwa zabuni TPA yenye thamani ya 10 bili.Swali ambalo lilikuwa linagonga vichwa vya wanadau ni mchakato wa upatikanaji wa tenda au zabuni hiyo. Swali la pili likuwa ni nani mmiliki wa hiyo kampuni. Hatimaye leo Nape kupitia Press release yake amethibitisha kuwa kampuni tajwa inamilikiwa na CCM.

Andy was the founder Chairman of Air Tanzania Corporation following the breakup of the East African Community in 1977 and is a past Chairman of Tanzania Railways Corporation and Tanzania Harbours Authority, Barclays Bank (Tanzania) Limited and 'Jitegemee Trading Company Limited'. For over 25 years he served as Chairman of Tanzania Standard Newspapers Limited (publishers of the Government owned newspapers – Daily News and Sunday News) – and of the National Museums of Tanzania.

I am just passing...
 
Back
Top Bottom