Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Haishangazi kauli ya kinyoya kama hii; lakini ni vyema amekiri kuwa kuna upuuzi unaendelea na CCM kupitia kampuni yake.

Labda ingejulikana ni CCM pekee yenye haki ya kuwa na makampuni ya kushindana kwenye tenda maana neno "vested interest" kwa nafasi ya kuwa chama tawala inawahusu wengine siyo CCM.

Wengine wanabeza vyama vya upinzani kutokuwa na Media zao kama Radio, TV na magazeti; wanasahau kuwa hata hilo kuna mwenye dola mpaka apende.

Nashukuru sana kwa taarifa ya Nape maana alitarajia CHADEMA isimamishe shughuli zake kwa mizengwe yake. CHADEMA itaendelea kuiua CCM kwa maslahi ya wananchi na nchi hii hata kama jua likifa
Nadhani umakini wa cdm ume pre empty njama za mafisadi wanaotumia ccm. Hebu Nape atueleze sukita ilikwenda wapi baada ya kufanya nini? Sio ilitumika kuneemesha vigogo wa ccm tu na aliyekua kinara hivi sasa amenasa ana kesi ya kutafuna UDA.
 
think we need another strong opposition political parties nyie wengine mnatubabaisha
 
Mwakyembe! Kwani kuweka Bandari kavu ni lazma katika eneo la CCM? TPA ina maeneo mangapi why sukita only? acheni Ufisadi eti Pertinership? safari hii mpaka kitaeleweka....

TPA haina eneo ndiyo maana inajaribu kuwekeza kwa ubia na wamiliki wenye maeneo yao, mara mumesahau upanuzi wa bandari ya Dar juzi tu ililazimu kuwahamisha wananchi wa Kurasini kwa fidia kubwa.
 
mkuu, hawawezi kukosa wanunuzi. Unajua magazeti ya udaku ndio yanapendwa zaidi, kwahiyo litanunuliwa sana. Ila swali ni je, nani atalinunua na ujumbe unaoandikwa utaleta impact gani?

Sasa hivi kusoma habari za tanzania daima ni sawa na kusoma zile hadithi za uwazi. Unasoma na kuiacha hapohapo kama movie tu...
hivi vikaragosi vya chadema ambavyo hata kauli zao vinaonyesha havijala kwani mabosi wao siku hizi wamevichoka kwa kudoeadoea makombo hasa ukichukulia maandamano yamethibitiwa.maskini vimebaki kubweka bweka na kauli muflsi
 
"Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika."
Nazani CCM wameombwa sidhani kama washakubali ilo ombi tuvute subira.Ila tunashukuru kwa walioliweka wazi ili suala angalau CCM wanaweza ona haya

Mkuu kuongezea kidogo hapo kuombwa ridhaa kunaendana na kuweka na bajeti kabisa?
 
ntoto antetea baba ndogo ake! ntoto uyo antoka kwa akina Mwa...!
 
NAPE POVU LINAKUTOKA- mbona hujataja kampuni zote 144 za CCM zinaendeshwa kwa njia haramu hazilipi kodi hata moja wapo imewekeza fedha Uswisi hiyo ni trailor NAPE ,kampuni moja baada ya nyingine zote zitawekwa peupe peeee,wizi wa kuchota serikalini na kujipa miradi ya serikali kupitia makampuni yenu huku wananchi tukibebeshwa kazi ya kulipa hadi watoto wetu waliotumboni mwa mama zao lazima ukome mwaka huu
 
naa huku tena ccm ni zzaidi ya viwavi jeshi

Wewe unadhani kwa nini wanajiapiza eti hakuna chama kitatawala wanajua wana makampuni kibao kibao hata CAG akiwakagua halafu akaacha kukagua na hayo makampuni yao yataanikwa tu wao walidhani watu hawajui
 
Heshima kwenu wanabodi,

Jana kuna uzi ulianzishwa hapa JF ambao una husu JITEGEMEE TRADING COMPANY LTD ambayo imepatiwa zabuni TPA yenye thamani ya 10 bili.Swali ambalo lilikuwa linagonga vichwa vya wanadau ni mchakato wa upatikanaji wa tenda au zabuni hiyo. Swali la pili likuwa ni nani mmiliki wa hiyo kampuni. Hatimaye leo Nape kupitia Press release yake amethibitisha kuwa kampuni tajwa inamilikiwa na CCM. kusoma hiyo Pres release gonga hapa.
Scribd

Naomba kuwasilisha
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai “Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari”.

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013


Jamani Mwenzenu ngeni Dar es salaaam, hapo ni wapi?
 
"CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha."


Hapa Nnape kajitwalia madaraka ya vikao kwani yeye hana mamlaka ya kusema na kutoa tamko zito hivyo kuwa CCM inaongeza waziri fulani, hii ni kuligawa baraza la Mawaziri kuwa mzalendo na anayefanya kazi ni MWakyembe pekee.......kaul hii itamtokea puani kama NEC wakiamua kwani sio azimio la kikao kuwa wampongeze Waziri mmoja na kuacha Baraza ambalo ni suala la Collective responsibility.......sasa kama hajui maana yake ajue kuanzia sasa,

Mwakyembe naye kawashiwa moto BUngeni na hata kwenye kamati na ikizingatiwa kuwa kamati yenyewe ya miundombinu inaongozwa na Serukamba Ole LOwassa sijui hapo Nnape kukitumia chama kumkinga rafiki yake kama ataachiwa hivi hivi ........kauli hii itachochea moto wa kuundwa kwa kamati ndogo ya kuchunguza na majibu kuwekwa hadharani...


Mark my words...
 
lkn hizo sehemu si zilitengwa kw ajili ya huduma za jamii, kama mngekuwa waungwana baada ya mfumo wa vyama vingi mngevirudisha serikalini vipangiwe matumizi. ebu tueleze mnazo hati za kumiliki viwanja hivyo

Ze Marcopolo aje hapa atwambie mali amabzo CCM wamezipata toka vyama vingi vianze!!
 
Kwa hiyo, Nape amekiri kuwa CCM ina mafisadi ambao walitaka eneo hilo wakawanyima.

we mjamaa kwa kupenda sifa, sasa namba zako za simu unatuwekea ili iweje, tukurushie vocha ili uzidi kupiga umbea
 
Kipato cha ccm kinatoka kwenye makampuni inayo yamiliki na kipato cha cdm kinatoka kwenye bilicanas na mabus ya mtei.
 
We kweli mshamba. Yani hujui kuwa CCM imekuwa na shughuli za uzalishaji mali tangu enzi za SUKITA?

Nyinyi vijana wa juzijuzi wa bavicha mna matatizo sana.

Ni CHAMA GANI DUNIANI kenye MIKATABA na SERIKALI ya NCHI??? KATIBA za NCHI Haziruhusu.... ni ULAFI na WIZI wa VIONGOZI wa CCM... kutaka kuchota PESA za GAS na MADINI...

Niambie NCHI GANI ina HIYO MIKATABA kama ya CCM? KANU? imeshakufa!!!

Enzi za SUKITA nchi ilikuwa ya CHAMA KIMOJA kama CHINA sasa hivi CHAMA na SERIKALI yake vinahusiana kwenye INVESTMENTS... Sio CCM sasa HIVI
 
We kweli mshamba. Yani hujui kuwa CCM imekuwa na shughuli za uzalishaji mali tangu enzi za SUKITA?

Nyinyi vijana wa juzijuzi wa bavicha mna matatizo sana.[/QUOTE

Sukita iliyokuwa inaongozwa na marehemu Kapinga lilikuwa ni mradi wa ccm kuwanufaisha viongozi wake na ndio maana vitabu vyake na miradi yake yote haikuwahi kukaguliwa hata mara moja ingawa ilikuwa na madeni makubwa kwenye benki ya NBC ya wakati huo!! Sidhani kama SUKITa iliweza kulipa yale madeni ya benki ingawa ilifilisiwa bila kuwa na mali za kutosha kulipia madeni yake. Hii inayoitwa jitegemee trading Company inaendeshwa katika misingi ile ile ya ulaji kwani huyo Machunde waliomuweka kuwa Mwenyekiti wa kampuni ni kijana fisadi [ alifukuzwa kuongoza DSE] ambae kwavile anajua hao magamba hawawapendi watu wenye weledi atahakikisha hao watakaoendesha hiyo kampuni ni vilaza ili aweze kuwaibia vizuri; anaebisha aweke wasifu wa mtendaji mkuu wa hiyo kampuni kama sio ushabiki wa magamba ndio kimekuwa kigezo kikubwa cha kumpa kazi badala ya professionalism!! Hivyo basi hii Jitegemee Trading Company iatkuwa sio tofauti na Sukita kabla yake na itakufa kifo kile kile cha mende.
 
politics has no rules Nape,hapo naona dili lenu limebumbuluka
 
Kipato cha ccm kinatoka kwenye makampuni inayo yamiliki na kipato cha cdm kinatoka kwenye bilicanas na mabus ya mtei.

jieleke kwenye hoja watanzania wanataka kujua mchakato wa hiyo tenda na uhalali wa hiyo kampuni imesajiliwa kama limited coy au ngo?
 
majebere, ZeMarcopolo, Mwigulu Nchemba, Chris Lukosi,

..hivi hakuna utata ktk masuala ya ETHICS/UTAWALA BORA/CONFLICT OF INTEREST kwa serikali na mashirika ya umma kufanya biashara na makampuni ya chama tawala??

..ukizingatia kwamba tulikuwa ktk mfumo wa chama kimoja, kwanini hizi mali za CCM zilizopatikana wakati wa mfumo wa chama kimoja hazikukabidhiwa serikalini??

cc: Nguruvi3, Zitto, John Mnyika, Kibunango, Jasusi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom