Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

Wana JF,

Napenda kumuuliza nape a very simple QN ni chama gani DUNIA hakipewi misaaada? Ni chama Gani Duniani hakichangiwi na wananchi????

Nadhani Nape Alama za nyakati nawe sasa zimeanza kukupotea au kama kuna mtu anakutumia sasa ukamwambie basi. kwanza hata wakatai umeanza kueleza au kutoa shtuma juu ya michango ya CDM physical appearance yako tu ilikuwa inaonyesha unatunga uongo kwa wale wanao jua kumsoma mtu mwanielewa vyema.

Nape we ungeendelea na kusafisha Chama chako na kuita vijana wakusaidia kukisafisha hao wazeeee watakuangusha na hutofanikiwa. Na dawa nzuri fanya kama Julias Malema former Youth Chairman of ANC alivyo kichachafya chama chake mpaka wakamweka nje na ni bado ni threat kubwa kwao
 
NA MWANDISHI WETU

CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

“Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

“Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”, Alisema Nape

Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

"Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

"Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.

Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

“ Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.

Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.

HIVOOOO HUYU NAPE CCM HANA KAZI ZA KUFANYA THE ONLY THING IS TO CRITICIZE CHADEMA IS THAT ALL HE CAN DO.. aghhhhrrrrrr .......... get to work acha porojo???!!!
 
Its time to discuss fundamental ideas for fundamental change and in advocating this, i call upon all people, especially change aspirants, to support, the strongest opposition political party in the country, CHADEMA. Nape to me is more-less a parrot.
 
Ndugu zangu hii propganda imefeli kabisa wala haina mashiko, just imagine, siku ya ijumaa nilikuwa naangalia Star TV with my little boy ambaye ana miaka 7 na jana akamuona Nape anaongelea kuhusu pumba zake akasema hivi, "Baba hawa wanaona gere kwa sababu wao hawawezi kuchangiwa zile ela kama chama chetu cha CDM", imagine just a 7 yrs boy anajua hii ni pumba, aibu sana NAPE jipangeni upya!
 
tutajie kwanza wamiliki wa KAGODA, wezi wa EPA, waliohusika kwenye ununuzi wa RADA. Andthen ndo uje ututajie wafadhili wa Chadema!! Nyie wakati mna sign mikataba ya madini Uingereza tena hotelini mnadhania c wajinga! We dogo modulaoblanga yako siyo nzima.
 
What if sio propaganda? ni kweli, what if ikathibitika kweli,? what if ....
Bado natafakari, na majibu ya hili hayatoki kwa mnyika anaonewa kijana wetu, wale wazee wenye chadema yao miaka hiyo... wanajua deep inside their heart,
 
Tajiri mkubwa katika Africa, Alhaji Aliko Dangote ambaye pia ni mfadhili mkubwa kwa chama tawala kule nigeria alitembelea ofisi ndogo ya Lumumba hivi karibuni. Sasa hapo watanzania tuambiwe nini!
 
Nape anaiiua ccm kwa mikono yake, maana anatoa kauli za mfa maji.lol!
 
It is widely believed that the
External Payments Account (EPA) at the Bank of Tanzania) was plundered to finance the 2005 elections.

The recipients of EPA money were mostly bogus companies set up for the purpose of emptying the EPA, an old commercial debt facility transferred from the MoF to the BoT.

An audit by Ernst and Young estimated that, out of TShs 130 billion paid to these companies, over TShs 90 billion were based on ‘invalid and fraudulent
supporting documents’ and could
not conclude on the validity of the
remaining TShs 40 billion due to
‘missing information.’

The Bank of Tanzania’s Governor Daudi Balali failed to respond to the auditors’ queries, and ‘the audit team found no evidence of the Board taking timely and effective actions on the
allegations ...’ The Ernst and Young
EPA audit established that most of
the bogus claims paid to local
companies had already been settled with the original claimants.

Kagoda Agriculture Ltd, which was registered in September 2005 and counted Jittu Patel (see text) as a director, received more than TShs 40 billion just before the elections. Deep Green Finance received more than Shs 10bn.

(Registered in 2005, Deep Green took over the assets and liabilities of Meremeta). Attempting to quash rumours, CCM Secretary General Yusuf Makamba denied that ‘CCM has any business links to Deep Green.’ The Governor of the Bank of Tanzania was eventually forced to resign. (He later died in the US, though his body was not brought back to Tanzania for burial).

Subsequently, numerous Bank of
Tanzania officials and EPA recipients, including Jittu Patel, were arrested and charged. An unusual aspect of EPA is that large amounts of money have been returned to the government under an informal amnesty agreement.

Source: Policyforum 2009b; URT 2008 via wikileaks
 
CCM donge limewaganda acheni fitina za kijinga,tuwaulize CDM wanafedha wamezitoa wapi wafadhili wapi wanaoweza kuwapa mabilioni?.hivi hizo fedha mnazokusanya katika viwanja vya mpira,migodi ya dhahabu na sasa bandari haziwatoshi?.chonde chonde zitawatokea puani hizo 2015
 
Nape fanya siasa za busara utaumbuka kama mzee Mkapa shauri zako..! Nilijua utajib kwa harambee kubwa kupita ya CHADEMA kumbe umeamua kufungua mdomo aibu hiyo katibu mwenezi
 
nakubalina nawe mdau cream ya carolite ni mbaya, ndo maana zimepigwa marufuku , sababu zinaharibu akili.Ni jambo la kuhuzunisha kiongozi mkubwa , tena wa chama tawala mwenye cheo nyeti cha itikadi cha kutoa na kutetea mwelekeo wa chama, anakosa utulivu, badala yake anakuwa mropokaji, inatia shaka.Nashindwa kuelewa kwa chama chenye kujivunia mtaji wa wanachama kibao, hakuna mtu mweledi, mwadilifu, msomi , mzoefu na mtaaluma wa siasa kuliko NAPE?je chama kinasababu gani kumwacha akiue huku chama kinaitwa dume?propagada anzozitoa NAPE ni za kizamani sana, katika karne na muda huu, hazitumiki tena.
Uchambuzi na hoja anzozitoa hazina mashiko, mfano;"chadema kupokea pesa kutoka kwa wafadhiri nje na uhusiano wa kuruhusu kupora rasilimali"kwa uzoefu TANZANIA tuna kitengo cha chakuchuguza fedha chafu,inayoingizwa hapa nchini, kwa wamemruhusu kuwa msemaji wao?na je wao wamesemaje kuhusu fedha hizo?na pia kuhusu rasilimali, nani mdhibiti na msimamizi wa rasilimali hizo ?je ni lini chadema wamepata kibali kusimamia na kutoa idhini ya uporaji?serikali kwa kutumia sheria na sera kuhusu rasilimali ndo msimamizi mkuu wa rasilimali, je NAPE anajua mgawanyo huu?kivipi CDM ikurupuke kwenda kusaini mikataba ya kupewa fedha kwa misingi ya kuruhusu kuporwa rasilimali wakati , utekelezwaji wake lazima ufuate sheria, taratibu, na kanuni;je ikifikia hatua hiyo, je vyombo vya dola havitajua na kuzuaia?je je serikali itakubali ikae kimya?huyu nape aache kutapatapa, huu mziki wa M4C unatisha ,na hasa kwa yeye ambaye hana mkakati wa kuyafanya hayo.Mtu mjinga ni kumwacha aropoke, mpaka achoke.Ujinga wake yeye anajua carolite tu.hata hivyo kama CDM imepata wafadhili si dhambi, hata ccm inao wafadhili wengi tu,hoja ya msingi propagada chafu zisizo na mshiko hazimsaiddi nape, jamii ya sasa ni ya waelewa wanamwona mropokaji , roho ya kushindwa na ya kwanini ndo inamsumbua.na hamasa kubwa ambayo inaonyesha kuna dira ya utekelezwaji



Nape anaropoka.Amewakera wengi, nami amenikera.
Kuna ukweli mchungu juu ya Nape kuwa ana tatizo katika ufahamu na ubongo wak
e.
Ninao ushahidi.
Nape,katika matokeo cha Kidato cha Sita alipata daraja sifuri
.Hii ndio asili ya kuwa na uwezo mdogo katika utambuzi na uchambuzi wa masuala.
Hizi habari sijazijua leo wala jana.Ninazo tangu mwaka 2000 ila niliamua kumstahi tu.
Nadhani sasa wachangiaji wataelewa aina ya mtu wanayengaika naye kila leo.
Kwa kuwa yupo hapa JF,naomba athibitishe vinginevyo..Akifanya hivyo nitajutia ''kosa'' langu.Akishindwa kufanya hivyo mimi nitamsaidia kwa kuweka matokeo yake hapa.Nisisikie mtu ananilaumu.


 
na unaposema wafadhili wananyemelea rasilimali kwa mgongo wa CHADEMA unamaanisha CHADEMA ndo chama tawala kinacholinda rasilimali zetu au!?!? Ukiingia usiache kulijibu swali zangu
 
Another example is Rostam Aziz,
Tanzania’s premier political broker. Of Persian origin, Aziz, who is in his 40s, is heavily involved in patronage
politics within the higher reaches of the ruling party, and is frequently referred to as the ‘king-maker’ who master-minded the strategy to finance Jakaya Kikwete’s rise to power.

He was Treasurer of the
ruling party until 2007, when his star began to fall as his association with
the Richmond power fiasco,
described above, and the earlier EPA scandal became public knowledge.
Aziz’s Caspian Construction Ltd is a
successful contracting company. He is also a newspaper owner. Aziz is the nearest Tanzania has to an example of an ‘oligarch’ with a ‘state capture’ agenda.

Aziz and Lowassa were leading
members of the team that brought Kikwete to power in 2005. Opinions are divided as to how well-informed Presidents are by their aides and intelligence services. The President is
often characterised as being
somehow ‘cleaner’ than most of his aides, who are widely thought to have personal and group agendas of their own.

At the same time, it is useful for the President to have the
fallback of plausible deniability as
the main line of defence against
accusations of personal involvement in corruption. The present President has seen fit to allow the prosecution of a number of senior politicians and
bureaucrats in relation to scandals
that originated under former
presidents, though other key (and
more senior) suspects have yet to be prosecuted.35 The latter might be interpreted as complicity by the President in these major deals, or worse, direct involvement; however, it is also congruent with political weakness, and an unwillingness to further destabilize the CCM boat.

Source: wikileaks 2008
 
Back
Top Bottom