Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Aug 12, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,519
  Trophy Points: 280
  NA MWANDISHI WETU

  CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

  "Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

  Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

  Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

  "Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama", Alisema Nape

  Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

  "Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

  Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

  "Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa." Alisema Nape.

  Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

  Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

  " Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa." Nape alisema.

  Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.
   
 2. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  boooooo..kwenda aaaaa zako huko
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Thanks god ... CHADEMA is the most famous chorus in this country

  Nape is dancing it now and always will
   
 4. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Kazi ya upande wa mashtaka ni kuthibitisha mashtaka na si kazi ya mshtakiwa" Nape ni mwepesi sana!.. Anataka CHADEMA wataje nini? Kama yeye anadai kuwa anayo 'mikataba' kwanini asiitoe?
  Ujinga ni kumtangazia adui yako "Nimekuzunguka pande zote" ili anyooshe mikono juu!.. Ajipange upya.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Daaah nape bwana..
   
 6. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hii sentensi"wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho". Hii ina maana zile pesa tulizoambiwa zimewekwa Uswisi kwenye akaunti za watu binafsi na makampuni ya gesi na petroli yanayofanya utafiti ni shukrani kwa CDM!
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,984
  Likes Received: 37,640
  Trophy Points: 280
  Mfa maji haachi kutapatapa.Wewe na chama chako ndio mnauza nchi yetu kila kukicha.Hizo ni propaganda zenu kama zile za udini na ukanda.Baada ya hizo kuwashinda sasa mnakuja na propaganda mpya.Tumewachoka na hata nchi wafadhili ni wazi hawana imani na nyinyi lakini unalolisema hawawezi kilifanya kwa lengo hilo.
   
 8. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Huyu dogo amepandikizwa roho ya uchawi kwenye nafsi ya hajitambui msameheni !!!!
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapa nafikiri Nape alipitiwa alikuwa anaongelea DRC labda, kwa Tanzania hizo rasilimali zinachotwa mchana kweupe, AMANI tele haisubiri machafuko wala migogoro.
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Bandubandu humaliza gogo, inawezekana chama cha msim kuihenyesha ccm? Nape tena!

  Nitarudi baadae ngoja niangalie kwanza chesea na man city.
   
 11. y

  yaya JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kwa mtu wa cheo chake kusema vitu kama hivyo.
  Nilidhani yeye mwenye nyumba angekuwa wa kwanza kumtaja mkaazi anayetaka kuichoma nyumba yake kwa kushirikiana na mtu wa nje kuliko kumtaka mchomaji huyo awaambie wakaazi wengine wa nyumba hiyo ni nani anayeshirikiana naye katika njama mbaya hiyo.

  Eti wasipowaeleza wa-Tz ukweli yeye atasema. Ni nini kinachomzuia kusema sasa? Anasubiri mpaka moshi uanze kufuka ndipo aseme jamani nyumba yangu inaungua na mchomaji ninamjua lakini sikutaka kumsema!!?? Wenye akili watamshangaa sana, ndivyo ilivyo kwa kauli hii ya kwake Mhe. Nape.

  Mimi ninadhani kwa ushindani uliopo kwa sasa TZ, yeye angebuni njia rahisi zaidi ya ile ya CDM ili kuhuisha chama chake CCM, kuliko kutoa kauli zenye utata kama hizi ambazo zinazidi kukidhoofisha.
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ooh boy! Mropokaji at work
   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa nashindwa nim-define vipi....Kauli kuwa kuna watu wanavizia utajiri wetu ni ujinga na upumbavu...Ni kweli kuwa huyu Nape Nnauye hajui kuwa kuna wawekezaji wanachimba madini utadhani ni ya kwao kipindi hiki kwa mikataba mibovu iliyofikiwa na chama chake na serikali yake? Ni kweli kwa akili zake anaamini chama chake na serikali yake wamelinda mali ya umma kwa kiwango cha kuridhisha hasa madini na wanyama pori? Ni kweli huyu Nape anaamini kuwa CCM haipokei pesa toka kwa mafisadi na wezi? Ni kweli huyu Nape anaamini kuwa serikali yake haipokei misaada toka kwa hao anaowaita ni maadui wa Tanzania?

  Ukweli ni kuwa CCM na serikali yake wamekuwa na kuweweseka sana wanapoisikia CHADEMA, na hii ni dalili njema kwa CHADEMA, na huyu kilaza Nape anapaswa kufahamu kuwa, hata kama kuna ukweli kuwa CHADEMA inapokea hiyo misaada kwani kuna kosa? Mbona hii ni kawaida kabisa, Mbona wao CCM wanamahusiano ana vyama vingine, na kuna siku Katibu mkuu wa CCM alipokea wageni toka nchi moja(jina limenitoka) wakiwa ni wafanyabiashara wakubwa toka chama kinachotawala kwenye hiyo nchi? Kwanini CCM wanapenda kuleta propaganda za kijinga na kishenzi kwa kila chama wanachodhani kuwa ni kikwazo kwao? Huu ni upuuzi wa Nape na chama chake pamoja na serikali yake.

  Go to hell CCM.
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Lissu aliwataja wabunge wa CCM wenye maslahi binafsi na tanesco, wakaja hivi hivi kubwabwaja bila nao kutaja basi hao wapinzani wanaowatuhumu, Nape mbona anamake cheap propaganda na kudhani hivi zama za 1940, anatakiwa ajue kwamba hiki si kizazi cha wajinga kwani yeye kashindwa kuisamimia serkal yake na mikataba mibovu.
  Pia ni vyema angezungumzia pia na swala la DEO FILIKUNJOMBE on M4C.
   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,120
  Likes Received: 10,470
  Trophy Points: 280
  Nape, Dr. Ulimboka amesharudi. Tunasubiri kauli yako kuhusu kurejea kwake.
  Watanzania tunasubiri kauli yako kwa hamu..
   
 16. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kuna muungwana aliwahi kuleta thread ndani humu '" Chunga Ccm inapoanza kulia rafu"..! hawajamaa ukweli wameshikwa PABAYA. Na bado bwana nape,utavua hadi nguo ya mwisho muziki ukikolea sawasawa. Go Chadema, go!
   
 17. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  carolite at work
   
 18. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  thanks kamanda for your realization on it cheap petty propaganda.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Dalili za mtu mzima kuchanganyikiwa si lazima aokote makopo. Haya mambo ya Chadema kutoka Chama cha Msimu na kuwa chama cha Uwajibikaji kinaichanganya kabisa CCM.

  CCM ikipata nafasi ya kuvuna mapesa ni haki yako, vyama vingine ni makosa, acheni usanii huu akina Nape. Ipo siku Nape utavua Gamba na kuvaa gwanda, na ulivyo kinyonga sitashagaa.
   
 20. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,120
  Likes Received: 10,470
  Trophy Points: 280
  propaganda hizi. hii sasa ikiisha sijui itakuja nn..
   
Loading...