Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

"Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

"Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama", Alisema Nape

Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

"Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

"Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa." Alisema Nape.

Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

" Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa." Nape alisema.

Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.

SOURCE : Mjengwa blog.

My take, kama kweli kuna hao wafadhili nadhani wangekipa chama kilichopo madarakani ili kiweze kujiimarisha na kutengeneza mikataba yenye masharti magumu kuvunjwa hata kama kitaondoka mararakani.
uoni fai

Sasa CCM imesha UZA NCHI? MADINI hatuoni faida ya kuchimba GOLD, GAS; Mnapeana MASHAMBA ya GEZAULOLE

MNAPEANA MALI ZA TANESCO wananchi wanakosa UMEME... HALAFU ACCOUNT USWISI; MAJUMBA KIBAO;

HAKUNA HESHIMA BUNGENI MNALINDANA KUIBA HADI MMBUNGE asiye na viti maalumu ANAUZA BANGI...

UNA WASI WASI na CHADEMA? HUO SIO UNAFIKI? AU MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA...
 
safi nape.ongelea na la ulimboka make kuna tetesi kuwa linawahusu serikali yako kwani mlisema bungeni LIWALO NA LIWE LIKAWA.kama wafadhiri wanawapa CDM YANAKUHUSU NINI? NDO TATIZO LA VYEO VYA OFFER.ZOEZI LA KUVUA WATU MAGAMBA UMEISHIA WAPI?


La kweli mkuu huyo nyani ni ccm haoni matatizo na zambi anazowafanyia watanzania.

- Elim ovyo kabisa, wajuu huko ccm husomesha makinda yao shule za kulipia.

- ccm wanawachukiza na kutowalipa walim sababu watoto wa masikin wabaki mbumbumbu ili watawaliwe kila siku na akina, kawawa,husen mwinyi, malima, mkapa nk.

-Afya mbaya na ccm haion dhambi kutowalipa madaktar, maskin wakiteketea, wao wanatibiwa india.

- wameuwa reli zote ili magali ya mabosi wa ccm na watoto wao yafanye biashara, kwan mfumko wa bei unawahusu bwana sis walalahoi tukafie mbali inchi si wanatawala wao.

- wameikausha hazina, bila aibu wamegeukia mifuko ya akiba zetu nssf, ppf nk, makato makubwa ya payee si maamuzi yao hata mungu hawaogopi.

Time will tell.......
 
wanataka kuirudisha nchi kwa wananchi na siyo kuiuza maana ilishauzwa siku nyingi na ccm.
 
Hapa Kamanda Mnyika kaongeza kombora lingine....

[h=6]John Mnyika
[/h][h=6]WanaCCM mtanisamehe, lakini imenibidi kutoa kauli hii ya awali kufuatia madai ya uzushi na ya kijinga yaliyotolewa na Msemaji wa CCM dhidi ya CHADEMA. Madai kama haya yanaendelea kudhihirisha kuwa taifa letu limefika hapa lilipo kwa pamoja na sababu zingine ‘upuuzi wa CCM’. CHADEMA haijawahi kufadhiliwa mabilioni kutoka nje, michango kwenye M4C iwe ni kwenye kumbi za hoteli au vijijini tunapochangiwa na wananchi wenye kutaka mabadiliko ya kweli ni ishara ya imani ambayo watanzania wanayo kwa CHADEMA. Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA kuwa inafadhaliwa na mataifa ya nje kupora rasilimali za nchi ikiwemo mafuta na gesi yanapaswa kupuuzwa kwa kuwa CCM ndio inao wajibu wa kuwatajia watanzania viongozi wa Serikali na CCM waliongiziwa mabilioni Uswisi kuingia mikataba mibovu ya rasilimali za nchi yetu. Aidha, CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuwataja kwa majina wanaoingia mikataba mibovu ikiwemo kwenye madini, CCM kwa kuwa ilikubali kuwa ina magamba ya ufisadi irejee kwenye orodha ya mafisadi na kuchukua hatua ya kujivua gamba badala ya kufanya siasa chafu dhidi ya CHADEMA. Majibu zaidi mnaweza kuyasoma kwenye mnyika.blogspot.com na kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kupitia CHADEMA katika kuwezesha Tanzania kupata uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya taifa letu na watu wake wote bila kujali itikadi. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.

[/h]
 
kati ya chama na serikali ipi yeynye dola?mbona mpka kesho inagia mikataba mibovu kama ya pan african energy, nayo ni kuchochea uvunjivu wa amani?na huo mkataba wa bomba la gesi nani kauona hauna chembe ya kuuza nchi, nao umeingiwa na chadema?mkatba wa urani kuchimbwa nani kasaini, serikali au chadema? una masilahi gani na nchi?nao hauna uvunjivu wa amani?mkataba wa kumiliki ekari 200,000 kule mpanda kwa waliokuwa makambi ya wakimbizi ,nani kausaini , serikali au chadema?una masilahi gani na nchi?je nao huu hauna chembe ya uvunjifu wa amani?je ile kesi ya dowans kulipwa , mbona serikali haiwaambii wananchi kama tunalipa au lah?NAPE namhafahamu, cheo walichompa ccm , na mabadiliko ya kisiasa ya M4C ni koti kubwa linampwaya, ni roho ya korosho ,Vyama vinatakiwa kuwajibika kwenda kuzungumza na wapiga kura wao.Leo ccm inaogopa kwenda kanda ya ziwa watakwenda kusema nn wakati wamewatelekeza wakulima wa pamba.
 
nchi mbona ilishauzwa siku nyingi? Kwa mkataba unaodaiwa kuwa wa miaka mia. Miaka mia moja nani atakuwepo. Na kama atakuwepo m2 wa sasa macho yatakuwa hayaoni. Pia hayo makaratasi waliyosaini yatakuwa yamesha chakaa na kuwa kama unga.
 
Kati ya ccm na chadema ni chama gani kinawahadaa watz? Hivi nape amesahau ya chumbani kwake anakimbilia sebureni? Naona ccm Mnaweweseka! Wananchi tunawaona mnavyoruka sarakasi!

Wanaruka sarakasi na mataulo viunoni mwao!
 
nape your such pathetic!! unazungumza vitu ambavyo wewe mwenyewe huviamini!! Hivi toka uanze kuchumia tumbo hujashiba tu??? Huku unako elekea ni ulafi na utaumbuka kijana mwenzetu!! Hivi huwezi kupambana na maisha kama sisi vijana wenzako tunavyo angaika?? kuliko hii biashara ya kuutukanisha utu wako adharani?? just a piece of advice bro!!
 
Niseme najisikia kinyaa kusoma maneno ya Nape kuhusu rasilimali zetu. Wanaongea kama vile wamekuwa walinzi wazuri wa rasilimali zetu kwa miaka yote hii.
 
Kutoa matamko kwa kila jambo wafanyalo chadema nikujivua nguo.

Nimebahatika kufanya kazi geita gold mine (GGM)

- kila alhamisi mida ya saa nne hadi tano ndenge inabeba dhahab directly to SA, hakuna cha tra wala cha ukaguzi wanaokuwepo wanapewa mavumba kidogo nakujifanya vipofu.

- IPTL wanatuibia hadi leo, kisa viongozi wa ccm kuingia mikataba ya kiuhujum uchumi.

- kule EPA CCM walikwiba na kupotezea kwa balali.

-kale kabenk deep green na kagoda wizi mtupu, ccm wanamjua.

-Manunuzi ya kifisadi ya rada na ndege ya rais ccm wanaajuwa aliefaidika ndo sabab mpaka leo wanakanusha lakin mabaki ya fedha kutoka Uk wamepokea! Mungu wangu how?

Tusubili wakitoka madarakani, nikuwapeleka kifungon directly no court involvement nor hearing because is very clear beyond doubt mkapa, kikwete, lowasa, karamagi, rashid-tanesco, Rostam and the likes must face the concequence or else should they need to live in peace are to free and live abroad.

Uchambuzi mzuri mno ni muhimu sana Nape auone ili umsaidie kuona upuuzu wake
 
Kwa tafsiri yoyote ile (kweli au sikweli) inaonyesha udhaifu mkubwa wa serikali ya magamba, dunia nzima sasa hivi inataratibu za kuhamisha fedha toka upande mmoja kwenda mwingine kama ni chafu zitaonekana tu. Kama kuna uwezekano wa cdm kuingiza fedha au vifaa (magari, piki piki nk) bila kuwa na ushahidi wa zilikotoka fedha basi ujue watawala wamelala na kimsingi hawawezi tena kupewa haki ya kutawala.
 
Hapa nafikiri Nape alipitiwa alikuwa anaongelea DRC labda, kwa Tanzania hizo rasilimali zinachotwa mchana kweupe, AMANI tele haisubiri machafuko wala migogoro.

Ni kweli kuwa inawezekana Nape ana point lakini presentation yake ni mbovu hasa kwa watu wenye elimu ya kata ambayo walifikiri itaendelea kutudidimiza kumbe nasi tunaelewa mambo kwa sasa.Nape fanya hivi taja mikataba na weka hewani hiyo mikataba chadema imeingia ili kuonyesha kweli una back-up za unayo zungumza.
Pili taja kwa majina wafadhili ambao unawajua na uthibitishe ili wao nao wajibu.

Ikiwezekana kasemee bungeni(Mwambie jamaa akuteue hata siku tatu kuwa mbunge si inawezekana)ili usishitakiwe nasikia huko kuna kinga alafu upoe.
ILA KWA MANENO TU AMBAYO HAYANA VIAMBATANISHO HATUTAKUELEWA HATA KAMA UTATOA POVU.Pia ujue kuwa sasa hivi ndo rasilimali zetu zinaibiwa kuliko maelezo na wachache ndo wanafaidi.Kama Gas ilioko chini wajamaa washafungua akount nje na mihela kibao imeingizwa ndo tukichimba itakuwaje?
Nimefurahi kwa kusoma maneno kama haya kutoka kwa mtu kama Nape na nasema mwisho haupo mbali.

CHADEMA FOR LIFE.
 
Sijawahi kuijua akili ya NAPE sijui ni njaa, sijui ni un afiki, sijui ni kujipendekeza maana kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kusema upumbavu wa kiwango hiki. Hivi kupewa pesa ili watu waje kuchuma rasilimali ambazo serikali ya CCM imeisha gawa bure zote ni akili au matope. Pili nani anaweza kutoa pesa ili abahatishe maana CDM hawajawa watawala akahacha kuwapa CCM ambao kwao rushwa ni kama kunywa chai ni HALALI na KAWAIDA. Kama kweli nape ameyasema hayo nimeamini anahitaji maombi
 
Nilishawahi kumwambia "Chama wa Gongo la Mboto" katika siasa za bongo, CDM inainyima sana CCM usingizi! Mapambano bado yananendelea na huu ni mwanzo tu, watachanganyikiwa wengi, siyo Nape tu!
 
Nape mwaka 1960 kulikua na FARU 260,leo wapo 16+3 tuliopewa toka uk juzi,wale 3 wa south africa wote ccm imewaiba!sasa ni nani anayeimaliza tanzania na kuweka vijisenti ughaibuni?nape u ve to think twice on your step in favour of ccm!
 
Ukisoma vizuri maelezo ya Nape,unagundua kuna jambo kubwa linamsumbua,nalo ni kwamba amegundua CCM itashindwa uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom