Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

atuambie mwenyekiti wake anapoenda kuomba neti anapishana na ndege imebeba madini ni sawa?kilaza mkubwa humpati mtu kwa huu upumbavu wako...
 
ccm ni sawa na nyoka tuliyekwisha mponda kichwa, hichi kilichobaki na nepi anachokifanya ni mtikisiko wa mkia tu hauwezi kunga'ta lazima mwisho nyoka afe tu. haaaah hhaaaa CHADEMA MWENDO MDUNDO, FICHUA MAFISADIIIIIIIIIII.
 
kama misaada hiyo ni kwa maendeleo ni.vema lakini kama ni kusaidia kuiondoa ccm madarakani basi nchi imeuzwa chadema ni kuogopa kama ugonjwa wa sukari
 
huyu mnauye jr anaweweseka na mafisadi yamemshinda anabaki anahaa tu na chadema, amalize ya chama chake kwanza asihangaike kuwasemea watu wengine ambao wanafanya mambo kwa akili zao na sio za kushikiwa kama yeye.
 
kinachonishangaza ni Nape kuongelea machafuko wakati Tanzanites,Diamonds,Gold zimekuwa zikichukuliwa kwenye migodi kupitia ndege binafsi,hebu tukumbuke ile ndege iliyovamiwa ikiwa na dhahabu ambayo idadi ilikuwa siyo kama walivyosema wakati wa kusafirisha.Watz wanauawa migodini ila sijaona machafuko yoyote yale iweje CDM kuchangisha hela Nape adai zitaleta machafuko?
 
Nasikitishwa sana na madai ya kipuuzi ambayo hutolewa na CCM.
Katibu Mkuu Mukama naye amewahi kutoa kauli za kipuuzi kama hizo huko Igunga ati CDM wameingiza magaidi kutoka Afghanistan na kupewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari, baada ya uchaguzi akiambiwa athibitishe anajiuma uma.
Hizo raslimali, CCM wanaweza kusema zimetusaidia vipi kama nchi?
Hiyo misaada tunayopokea na kuwa nchi ya 3 baada ya Afghanistan na Iraq imetusaidia nini Tz hadi sasa?
Nchi yetu tunakosa siasa safi na uongozi bora.
 
WanaCCM mtanisamehe, lakini imenibidi kutoa kauli hii ya awali kufuatia madai ya uzushi na ya kijinga yaliyotolewa na Msemaji wa CCM dhidi ya CHADEMA

. Madai kama haya yanaendelea kudhihirisha kuwa taifa letu limefika hapa lilipo kwa pamoja na sababu zingine ‘upuuzi wa CCM’. CHADEMA haijawahi kufadhiliwa mabilioni kutoka nje, michango kwenye M4C iwe ni kwenye kumbi za hoteli au vijijini tunapochangiwa na wananchi wenye kutaka mabadiliko ya kweli ni ishara ya imani ambayo watanzania wanayo kwa CHADEMA.

Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA kuwa inafadhaliwa na mataifa ya nje kupora rasilimali za nchi ikiwemo mafuta na gesi yanapaswa kupuuzwa kwa kuwa CCM ndio inao wajibu wa kuwatajia watanzania viongozi wa Serikali na CCM waliongiziwa mabilioni Uswisi kuingia mikataba mibovu ya rasilimali za nchi yetu.

Aidha, CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuwataja kwa majina wanaoingia mikataba mibovu ikiwemo kwenye madini, CCM kwa kuwa ilikubali kuwa ina magamba ya ufisadi irejee kwenye orodha ya mafisadi na kuchukua hatua ya kujivua gamba badala ya kufanya siasa chafu dhidi ya CHADEMA.

Majibu zaidi mnaweza kuyasoma kwenye mnyika.blogspot.com na kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kupitia CHADEMA katika kuwezesha Tanzania kupata uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya taifa letu na watu wake wote bila kujali itikadi. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke
 
"Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.

Hata kule Mara na Shinyanga kwenye migodi ya dhahabu na Arusha kwenye Tanzanite, wanachi wananyanyaswa na wawekezaji wakati serikali ya CCM inashangilia!!!!!! Tuambie watanzia tulivyofaidika na rasilimali zetu mpaka sasa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru. Unazifahamu nchi za Malasia na Singapore ambazo zilipata uhuru takribani miaka sawa na Tanzania?
Huna jipya Nape au umetumwa na nani? Tuambie fedha za EPA, Meremeta, Kagoda nk na hizo zilizofichwa huko Uswiss na mabwana zako vigogo wa CCM uziweke wazi kwanza halafu hizo za CHADEMA.
Umefilisika kimawazo kabisa. Ungejua unaijenga CHADEMA bila kujijua. Pole sana utakosa usingizi bureeeeee!
 
kama serikali ya chama tawala mnashindwa kudhibiti pesa chafu kuingia vyama vya upinzani tuna serikali kweli just resign and let a sensible party to lead this land!!
 
Asee....nimependa uwazi aliouonyesha Mnyika. Mtu akiwa mjinga na mpuuzi ni vyema ukamwambia machoni kwamba ni mjinga na mpuuzi.
 
okay, tumemsikia ngoja na sie tuchuje kwanza kabla ya kutoka povu.

CDM, kufichua madhambi ya CCM haizuii wao kufadhiliwa.
 
Chadema wauze nchi ipi wakati CCM walishaipiga mnada? Rejea kufichuka kwa kashfa ya meli za mafuta za Iran kutumia bendera ya Tanzania kukwepa vikwazo. CCM hawana adabu wala maana. Kama ni madai ya kuuzwa nchi yanaweza kutolewa na wengine hata ndege lakini siyo CCM. Kweli waso haya wana mji wao na mji wao ni Tanzania. Hakika nyani haoni kundule. Kuna watu wameiuza Tanzania tena kwa bei ya kutupwa kama CCM? Uliza uchumi wetu unashikiliwa na nani kama siyo wahindi na wawekezaji? Hata serikali yetu iko mifukoni mwa magenge haya. Kwa ufupi Tanzania iliuzwa siku alipoondoka Nyerere.
 
Nape huijui CCM wewe, ccm inawenyewe na wewe ni vuvuzera tu. Hivi hujiulizi ni kiongozi yupi anakuheshimu ndani ya ccm tofauti na mwenyekiti unayempelekea umbeya na ndiyo maana nchi imemshinda. Nenda zako huna lolote.
 
Yaani hata walio katika payroll ya Nape wanaona noma kuchangia thread hii kwa jinci boci wao alivyochemka..!

Sent from Tora Bora..
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom