Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

Chadema wanataka kuuza nchi gani? Kama Tanzania mbona ccm washaiuza karibia yote? Vimebaki visiwa vya mafia tu na vyenyewe vikipata wateja vitauzwa......
 
jamaniNAPE kumbe unavyaaga suti na tai je C C Nwamepewa bei gani maa kwsasa wanauzi si nchi tu bali wanatoa kila kitu we kaa nahayo kwani hamtaki hii nchi iwe na NEEMA MEJITAHIDI MMEKWAMA SASA ANGALIENI WENGINE WANAWEZA TUMECHOSHWA NA POROJO TUNAONA TUNAELEWA NA WEWE SIOTENA MSEMAJI WA WATANZANI
 
Huyu punguani nape naona amechachawa, anataka kumdanganya nani kuwa hao anaowaita wafadhili hawajui kuwa shortcut ya kugema rasilmali zetu ni ccm ambayo wamekuwa wakiwatumia na wanaendelea kuwatumia mpaka leo hii, huyu hamnazo nape anataka kutuhadaa eti hao anaowaita wafadhili ni wajinga saaana kiasi kwamba wawekeze kwa cdm ambao kuingia kwao madarakani ni hadi bahati nasibu ya uchaguzi ichezwe ndipo mshindi ajulikane ni yupi! wakati wapo ccm ambao miaka nenda rudi wanasaliti maliasili zetu kwa wafadhili hao hao, wafadhili si wajinga watumie njia ngumu ya kubahatisha wakati njia mdebwedo ya ccm waliyoizoea ipo, nape you can not fool anybody, you are just wasting your time fooling yourself!
 
Kati ya ccm na chadema ni chama gani kinawahadaa watz? Hivi nape amesahau ya chumbani kwake anakimbilia sebureni? Naona ccm Mnaweweseka! Wananchi tunawaona mnavyoruka sarakasi!
 
Nape hana meno. Simba mla nyama hatangazi. Kama anao ushahidi, si auweke hadharani? Malumbano ya nini?

Kila anapoona jina lake halijatajwa, basi anaibuka na kuibuka na kuanza kubwabwaja, bila kuweka breki mdomoni! Hahaha!

Nape unaiaibisha CCM. Anayekuzuia kuweka hadharani huo ushahidi wa hayo mabilioni ya CHADEMA ni nani? Weka mambo hadharani, mkono mtupu haulambwi! Kalaghabahoooooo!
 
Toa ujinga wako hapa hizo mali zinazoonyesha dalili ya kuwepo kwani hizo zilizokuwepo na mkagawa buri huzioni.
Hivi wewe unafikiri kila mtu ni mjinga kama wewe.
Mimi ni mfuasi wa chama tawala lakini si mwana ccm kwa ujinga wenu huu wa makundi na hasa wewe kutoheshimu wazee walio kibeba chama mapaka hapo kilipo.unajifanya wewe ndio kilakitu wewe na jamaa mtauwa chama.
Kweli wewe unatukana mzee aliyekuwa anaongea na baba yako wewe leo kwasababu ya siasa unamjibu kwa kejeli naumia binafsi nikiwa bado kijana mdogo nadhani niendelee na kazi zangu za kilimo niachane na siasa.
Sasa ndio mnawapa chadema nguvu na wacha wawazidi maarifa kwasababu wewe si mbunifu sio chama no si mbunifu.
CCM inahazina watu kubwa hilo tu ni tosha kuwazima chadema ila kwasababu unajifanya ndio kila kitu endelea waone wajinga wamekaa kimya siku ikifika wenyewe mtawafata kuwapigia magoti na mwaka 2015 wewe na hao mnaojifanya mnajua anakuja wa CCM ila mtakoma labda muhame nchi.
 
Kutoa matamko kwa kila jambo wafanyalo chadema nikujivua nguo.

Nimebahatika kufanya kazi geita gold mine (GGM)

- kila alhamisi mida ya saa nne hadi tano ndenge inabeba dhahab directly to SA, hakuna cha tra wala cha ukaguzi wanaokuwepo wanapewa mavumba kidogo nakujifanya vipofu.

- IPTL wanatuibia hadi leo, kisa viongozi wa ccm kuingia mikataba ya kiuhujum uchumi.

- kule EPA CCM walikwiba na kupotezea kwa balali.

-kale kabenk deep green na kagoda wizi mtupu, ccm wanamjua.

-Manunuzi ya kifisadi ya rada na ndege ya rais ccm wanaajuwa aliefaidika ndo sabab mpaka leo wanakanusha lakin mabaki ya fedha kutoka Uk wamepokea! Mungu wangu how?

Tusubili wakitoka madarakani, nikuwapeleka kifungon directly no court involvement nor hearing because is very clear beyond doubt mkapa, kikwete, lowasa, karamagi, rashid-tanesco, Rostam and the likes must face the concequence or else should they need to live in peace are to free and live abroad.
 
Katika mitandao ya kijamii kumesambazwa habari zikimnukuu msemaji wa CCM kutoa madai mbalimbali ya uzushi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea kutekeleza mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya umma' katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini.

Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa kwa ukamilifu, hata hivyo kuhusu madai yaliyokwisha sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM nachukua fursa hii kutoa kauli ya awali kama ifuatavyo:

Kuibuka huku kwa CCM na kufanya propaganda chafu ni ishara ya kwamba CCM inaumizwa na namna ambavyo watanzania wanajitokeza kuunga mkono CHADEMA kwa hali na mali hivyo CCM sasa inatapatapa kujaribu kudhibiti wimbi la mabadiliko kwa kutumia siasa chafu. Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anapaswa kueleza watanzania iwapo mikakati hiyo michafu ina baraka zake na za serikali anayoiongoza kwa kurejea pia madai yaliyotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira kuwa CHADEMA itasambaratishwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mbinu mbalimbali.

CCM kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kufanya usanii kuhalalisha fedha haramu kama ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita baada ya viongozi waandamizi wa CCM na makada wake kuchota fedha za chafu kifisadi kama zile za kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na vyanzo vingine vichafu na kuzisafisha kupitia harambee za hadaa zilizofanywa na CCM kwa nyakati mbalimbali; inataka kuichafua CHADEMA inayopata fedha kutoka vyanzo halali kwa njia za wazi ili kukatisha tamaa umma wa watanzania unaochangia vuguvugu la mabadiliko.

Viongozi wa CCM wameamua kujidanganya, kuidanganya Serikali yao na kujaribu kuwapotosha watanzania lakini CHADEMA inatambua kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote; na kwamba watanzania wa leo kwa uwingi wao hawawezi kudanganyika na uzushi wa kijinga wa CCM.

Ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA imekuwa ikifanya harambee kwa uwazi kwa nyakati mbalimbali katika kumbi na katika mikutano ya hadhara ikiwemo ya vijijini ambapo michango hutolewa kwa uwazi, aidha michango kwa njia ya simu inaweza kufuatiliwa na kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba watanzania wameamua kuchangia mabadiliko ya kweli.

Madai ya CCM kuwa CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni ya shilingi kutoka mataifa ya nje ni ya uzushi na narudia kwa mara nyingine tena kuitaka CCM itaje majina ya serikali, taasisi ama makampuni ya nje ambayo CCM inadai kwamba CHADEMA imepokea mabilioni ya shilingi katika siku za karibuni au inatarajia kupokea.

Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA ilipaswa CCM ieleze watanzania orodha ya vigogo wa Serikali inayoongozwa na wanachama waandamizi wa CCM ambao wanaelezwa kuwa na akaunti nchini Uswisi na nchi zingine wakituhumiwa kupewa fedha za kifisadi kutoka kwa makampuni ya utafutaji wa mafuta, gesi asili pamoja na uchimbaji wa madini.

CCM ilipaswa ieleze watanzania sababu za kuendelea kusuasua kujivua magamba ya ufisadi kinyume na maazimio ya CCM yaliyofikiwa baada ya msukumo wa CHADEMA kutaja orodha ya mafisadi kwa kuwa kati ya mafisadi hao ni pamoja na viongozi wa CCM walioiingiza nchi katika mikataba mibovu.
 
Asante mbunge wangu mnyika.
SWALI KUBWA KWA NAPE NA CCM NI JE "RASILIMALI HIZI ZILIZOPO TZ" ZIMEGUNDULIWA HIVI KARIBUNI?

Huu kwa Watanzaania wengi ni uongo na uzushi. Mafuta, gesi, urani na mengineyo yaligunduliwa enzi za Nyerere na mengine enzi za ukoloni. Fuatilia Songosongo uone kisima cha kwanza cha NG (gas asili kilichimbwa lini), fuatilia historia ya Tz kujua uchimbaji wa almasi, dhahabu e.t.c ulikuwa unafanywa tangu lini. Nyerere had most of these natural resources data BUT HE RESERVED THEM FOR "Tanzanians", although magamba has been selling them 4 thenselves.
 
mh mnyika (mb) nimeisoma hii taarifa yako, imekuwa ni kitu cha kawaida sasa kwa cdm kutoa taarifa na matamko kama haya. baadhi ya haya matamko yamekuwa yakifanyiwa kazi na serikali ya ccm kwa kiasi kisicho ridhisha kabisa na mengine na hasa yale ambayo ni muhimu ya msingi kabisa kwa mstakabali wa taifa hili wamekuwa wakiyapuuza kabisa. sasa nyie kama chama makini hamuoni ni wakati mwafaka kabisa kwenda mbele zaidi ya haya matamko na kuwaeleza wananchi wa tz kuwa mtachukua hatua gani hasa kwa mafisadi pale wananchi wa takapo kuwa wa mewaamini na kuwapa nchi ili muwaongoze. muwaeleze wananchi kwa lugha ambayo watawaelewa na kuwa amini bila shaka yeyote kuwa mtatekeleza hayo mnayo wa ahidi.
 
safi nape.ongelea na la ulimboka make kuna tetesi kuwa linawahusu serikali yako kwani mlisema bungeni LIWALO NA LIWE LIKAWA.kama wafadhiri wanawapa CDM YANAKUHUSU NINI? NDO TATIZO LA VYEO VYA OFFER.ZOEZI LA KUVUA WATU MAGAMBA UMEISHIA WAPI?
 
Hebu Nape tusaidie kuuweka hadharani huo ushahidi ulionao. Ongea kwa hoja. Maneno maneno ya nini?
 
Tupo tulikuwa tutakuwa ndo CHADEMA inavyofanya ukombozi,tuachane na mr. carolite.
 
Magamba wanaweweseka na mafanikio makubwa ya harakati za CHADEMA hivyo wameamua kutumia mbinu chafu za kila aina zikiwemo kutoa madai ya uongo ambayo hayana uthibitisho na kutumia vyombo vya magamba wenyewe wanaviita "vyombo vya dola" ili kuminya haki ya kikatiba na CHADEMA kufanya harakati zake mahali popote pale nchini. Kifo cha magamba hakipo mbali.
 
Back
Top Bottom