EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, juzi alikumbana na msukosuko wa kuzomewa na wananchi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mkoma, wilayani Rorya, mkoa wa Mara.
Nape alizomewa na wananchi hao waliokuwa wakimsikiliza mara tu baada ya kutoa kauli za kukikejeli Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambazo zilitafsiriwa kama matusi na kashfa kwa chama hicho.
Katika uchaguzi huo mdogo kwenye kata hiyo, CHADEMA pia imemsimamisha mgombea wa udiwani. Na hivyo kauli ya Nape kuwa chama hicho ni cha wahuni, kinachotumia salamu ya kunyoosha vidole viwili juu kama alama ya kutukana, ilionekana kuwakera wananchi.
Hata salamu yao ni ya kihuni, ni ishara ya matusi. Na ninyi vijana mnashabikia hiyo bila kujua. Hivyo salamu haiwafai kuonyesha vidole viwili; ni salamu inayowafaa vijana wahuni, alisema mwanasiasa huyo huku akinyoosha salamu hiyo kwa vidole vyake.
Huku akitamka maneno mengine ambayo kimaadili hayaandikiki kwenye chombo cha habari makini kama Tanzaima Diama, Nape aliendelea kuikejeli CHADEMA hatua iliyowakera wananchi na wengi wakaanza kuguna.
Hata hivyo, wakati akiendelea na tafsiri zake kuhusu salamu za CHADEMA ikiwemo ile ya kukunja ngumi na kusema peoples power, ghafla baadhi ya wananchi walianza kumzomea, huku sauti nyingine zikisema, Ongea sera huo uwongo..unatudanganya.
Hali hiyo iliendelea kuzusha zogo kutoka kwa wananchi wengi kila upande mkutanoni hapo na zomeazomea ya ooh oooh ikakolea na kusababisha wananchi kuanza kuondoka.
Nape alionyesha kupuuza hali hiyo na hivyo kuendelea kusisitiza kuwa wakichagua diwani kutoka CHADEMA hawatapata maendeleo yoyote kwa sababu chama hicho hakina serikali.
Aliwataka wamchague mgombea udiwani wa CCM, Jaoshi Warioba, huku akiahidi kuwa ndiye atakayeweza kushirikiana na serikali ya CCM kuanzisha mamlaka ya mji mdogo wa Shirati kwenye eneo hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, si alikuja hapa na alisema serikali inaanza mipango ya kuanzisha mamlaka ya ya mji mdogo hapa Shirati, sasa diwani wa CCM ndiye atakayeweza kufanikisha hilo na si wapinzani, alisema Nape na baadaye kulazimika kufunga mkutano huo kwa haraka na akaingia kwenye gari lake na kuanza kuondoka kwa kasi.
Tanzania Daima ilimtafuta Nape jana bila mafanikio kutokana na simu yake ya kiganjani kuwa imefungwa kwa muda wote.