Nape azomewa tena Rorya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape azomewa tena Rorya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Oct 1, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, juzi alikumbana na msukosuko wa kuzomewa na wananchi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mkoma, wilayani Rorya, mkoa wa Mara.

  Nape alizomewa na wananchi hao waliokuwa wakimsikiliza mara tu baada ya kutoa kauli za kukikejeli Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambazo zilitafsiriwa kama matusi na kashfa kwa chama hicho.

  Katika uchaguzi huo mdogo kwenye kata hiyo, CHADEMA pia imemsimamisha mgombea wa udiwani. Na hivyo kauli ya Nape kuwa chama hicho ni cha wahuni, kinachotumia salamu ya kunyoosha vidole viwili juu kama alama ya kutukana, ilionekana kuwakera wananchi.

  “Hata salamu yao ni ya kihuni, ni ishara ya matusi. Na ninyi vijana mnashabikia hiyo bila kujua. Hivyo salamu haiwafai kuonyesha vidole viwili; ni salamu inayowafaa vijana wahuni,” alisema mwanasiasa huyo huku akinyoosha salamu hiyo kwa vidole vyake.

  Huku akitamka maneno mengine ambayo kimaadili hayaandikiki kwenye chombo cha habari makini kama Tanzaima Diama, Nape aliendelea kuikejeli CHADEMA hatua iliyowakera wananchi na wengi wakaanza kuguna.

  Hata hivyo, wakati akiendelea na tafsiri zake kuhusu salamu za CHADEMA ikiwemo ile ya kukunja ngumi na kusema ‘people’s power’, ghafla baadhi ya wananchi walianza kumzomea, huku sauti nyingine zikisema, ‘Ongea sera…huo uwongo..unatudanganya.’

  Hali hiyo iliendelea kuzusha zogo kutoka kwa wananchi wengi kila upande mkutanoni hapo na zomeazomea ya ‘ooh…oooh’ ikakolea na kusababisha wananchi kuanza kuondoka.

  Nape alionyesha kupuuza hali hiyo na hivyo kuendelea kusisitiza kuwa wakichagua diwani kutoka CHADEMA hawatapata maendeleo yoyote kwa sababu chama hicho hakina serikali.

  Aliwataka wamchague mgombea udiwani wa CCM, Jaoshi Warioba, huku akiahidi kuwa ndiye atakayeweza kushirikiana na serikali ya CCM kuanzisha mamlaka ya mji mdogo wa Shirati kwenye eneo hilo.

  “Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, si alikuja hapa…na alisema serikali inaanza mipango ya kuanzisha mamlaka ya ya mji mdogo hapa Shirati, sasa diwani wa CCM ndiye atakayeweza kufanikisha hilo na si wapinzani,” alisema Nape na baadaye kulazimika kufunga mkutano huo kwa haraka na akaingia kwenye gari lake na kuanza kuondoka kwa kasi.

  Tanzania Daima ilimtafuta Nape jana bila mafanikio kutokana na simu yake ya kiganjani kuwa imefungwa kwa muda wote.
   
 2. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uzuri Nape yupo hapa JF atatuambia nini kilimsibu huko Rorya.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi na ww kwa akili yako unategemea tanzania daima liandike mema ya ccm. Hili lajulikana ni gazeti la mbowe, unataka wenzako wanyimwe mshahara km wasipo andika mabaya ya ccm. TANZANIA DAIMA = MBOWE = CDM , unategemea nn sasa hapo !
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi huyu nape yuko timamu kweli
   
 5. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #5
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katika kichwa cha habari nilifikiri alikuwa anapita sehemu akazomewa na wananchi wote, kumbe habari ilikuwa inamaanisha kuzomewa na BAADHI ya wananchi katika mkutano. Kunatofauti kubwa sana kati ya kuzomewa na wananchi na kuzomewa na baadhi ya wananchi.

  Unaweza ukapandikiza watu wawili wa kuzomea katika mkutano wa watu 500 na bado ukaandika alizomewa, na hiyo inakubalika kabisa iwapo utaongezea kazomewa na baadhi, na hiyo ni kawaida.

  Ukiwa kiongozi wa watu 10 halafu wote wanasema NDIO NDIO, jua una kundi bovu sana. Kuzomea, kubishana ni sawa, ila haya ya Igunga ya bastola, tindikali, kutoa vilemba, kuteka nyara, n.k. yanaelekea kutuvua utu wetu kabisa.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah ataingia humu usiku wa manane kuangalia kazi iliyofanywa na vijakazi wake ili kujustfy kama bado wanastahili malipo.

  Hawezi kueleza kilichomsibu, sana sana ataandika mipasho na taarabu kama kawaida yake na kutokomea.
   
 7. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mhariri wa gazeti la UHURU?
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asante Mungu.
   
 9. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Nape Kijana anayejimaliza mwenyewe kisiasa, ananga'nga'na na mfupa chama kilichokosa dira na mwelekeo, jamani nisaidieni nani anayejua ni kwa nini Nape hashiriki kampeni za Igunga????????????

  Kuna mtu aliweka dau la $100 endapo nape ataonekana Igunga, maskini alishiriki tu si ya mazishi!!!!!!!!
   
 10. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata mumseme nape hawezi kata tamaa lile ni greda anakatua go nape go on!
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red panadhihirisha kuwa Nape Nnauye ni mlemavu wa kufikiri. Ishara ya vidole viwili ni sign of victory na hii sign inajulikana universally yani mtoto wangu wa baby class ukimuonyesha alama ya vidole viwili anakuambia ni sign of victory. Alama hii inatumika kama ishara ya ushindi.

  Sikutegemea kijana msomi kama Nape Nnauye unaweza kuchemka kutafsri ya alama hii ya kimataifa na umeamua kufanya siasa za maji ya chooni kama layman, Inshort nimegundua Nape Nnauye umepanic, hali ni tete juu yako na CCM, kazi uliyopewa ni ngumu na sio nyepesi kama ulivyodhani awali.


  hand showing victory sign
  pipo pawa1.jpg Nape Nnauye nakushauri uwe na tabia ya kujisomea ile uende sawa na kizazi hichi, tenga mda na tengeneza ratiba ya kujisomea vitu mbalimbali kwa manufaa yako.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi atakuja Kuleta Mipasho
   
 13. FREDRICK KIMARO

  FREDRICK KIMARO Member

  #13
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli bos mimi nilikuwepo kwenye mkutano huo nimesika mwenyewe na kuona hawa magamba wamechoka kwa nini hawakubali?
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi huyo kijana aitwae Nape amekua damu gani hiyo huko mikoani; ni damu kunguru au ya bundi???
   
 15. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jamani huu ni wakati wa nape nae kujitengenezea posho na night uwa anajua yatakayompata katika mikutano ila anaona ni bora haende ili kaposho kasimpite pembeni.Nape karibu na mwanza kwenye kampeni za kumnadi diwani wa kirumba baada ya kifo cha diwani wa cdm.
   
 16. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Anafahamu Mkuu maana ya hiyo sign, ila hii ndo kawaida ya magamba kuwachukulia watu wa vijijini kuwa hawajui kitu hivyo unaweza kuwamanipulate kwa lugha tu wakaridhika. Hiki ndo kinachoenda kuiua ccm maana wanadhani kuwadanganya watu siyo issue ilimradi wao wamepewa kura.

  Lakini ndo mwisho wa uongo umekaribia ngoja tungojee.
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  rudi kule kwenye jukwaa la watoto
  wewe si ndio ulikuwa unaomba msaada ufundishwe jinsi ya kupata mwanamke?
  kisa ni kwamba unalalamika kuwa unpiga punyeto mpaka unachubuka!!!
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 19. paty

  paty JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  we zero brain ndo nape mwenyewe, na kwa taarifa yako nape ni mtu muhimu kuiangusha ccm na nashukuru , mwisho wa ccm umekuwa mfupi kuliko nlivyodhani
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Tingatinga lenyewe limeshasalimu amri na kujituliza huko Mvumi ije iwe hako kagreda kanako piga kelele za kujivua gamba? Kwanza hata huko CCM wamekachoka ndio maana kamepigwa red card Igunga
   
Loading...