Nape aonya waandishi mikutano ya hadhara

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewasihi waandishi wa habari kuepuka kuandika maneno yasiyo ya staha na kuegemea upande mmoja wakati wa mikutano ya vyama siasa iliyoruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Nape alienda mbali zaidi na kusema waandishi wasirushe maundhui yenye matusi na kuwataka kubalance story ili kutenda haki kwa wengine.
 
kazi ya waandishi ni kuhabarisha na sio kubalance story kama waziri anavyodai
kuhusu matusi majukwaani ilipaswa kuwaambia hao walengwa ambao wanasema hayo matusi,,
ila kukimbilia kwa waandishi wa habari ni kama vile mnajihami,mnawatisha waandishi wasifanye kazi yao ipasavyo
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewasihi waandishi wa habari kuepuka kuandika maneno yasiyo ya staha na kuegemea upande mmoja wakati wa mikutano ya vyama siasa iliyoruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Nape alienda mbali zaidi na kusema waandishi wasirushe maundhui yenye matusi na kuwataka kubalance story ili kutenda haki kwa wengine.
Awakumbushe TBC kuwa Hilo ni shirika la umma sio la ccm.
 
kuegemea upande mmoja wakati wa mikutano ya vyama siasa iliyoruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Tayari CCM imeanza kuingiwa na hofu kuu ya uwepo wa uhuru wa kufanya shughuli za kisiasa .

Chama dola kinaweweseka huku wanasema wapo tayari kwa siasa za ushindani lakini hawajiamini wanaanza kuchagiza masharti, vigezo na kanuni zitakazo bana uwepo wa hali huru ya siasa kwa vyama vyote.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewasihi waandishi wa habari kuepuka kuandika maneno yasiyo ya staha na kuegemea upande mmoja wakati wa mikutano ya vyama siasa iliyoruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Nape alienda mbali zaidi na kusema waandishi wasirushe maundhui yenye matusi na kuwataka kubalance story ili kutenda haki kwa wengine.
Nape afanye kazi yake ya uwaziri, awaache waandishi wafanye kazi yao ya uandishi na vyama vinabidi kuwa makini sana inaonekana nape anaandaa mkakati wa kuwablock kwenye media
 
Chama dola kinaweweseka huku wanasema wapo tayari kwa siasa za ushindani lakini hawajiamini wanaanza kuchagiza masharti, vigezo na kanuni zitakazo bana uwepo wa hali huru ya siasa kwa vyama vyote.

9 January 2023

VIDEO: ASKARI POLISI WATAKIWA KUTOSHABIKIA VYAMA VYA SIASA - ''SHABIKIA YANGA, SIMBA''...

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha watakiwa kutojihusisha na ushabiki wa vyama vya siasa.

Hayo yamesemwa leo January 09, 2023 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini kamishina Msaidiz wa Polisi ACP Simon Pasua wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza askari walio fanya vizur zaidi mwaka jana 2022 Mkoani Arusha.

ACP Simon Pasua amesema kuwa askari wanapaswa kushabikia maswala mengine ya kijamiii kama vile michezo amewataka askari hao kujikita zaidi katika ulinzi wa raia na mali zao ili kuleta ufanisi na kupunguza manunguniko ya wananchi.
Source : Global TV Online
 
Back
Top Bottom