Nape Ampongeza Lowassa kwa kutii Agizo la Chama

Nape Ampongeza Lowassa kwa kutii Agizo la Chama

Nape wewe ni jembe na ukweli wako ndiyo utakaokikomboa chama na nchi kutoka katika makucha ya wanaotaka kuleta anarchy. Si hao wameufyata na kufunga Duka na kukusanya mahema na viti vyao vya plastic. Wamebaki wachumia tumbo kubwata na kulalama kama mbwa MWITA.


naaaaaaaaaaaaaaape!!!!!
 
Sio aliambiwa na mamvi kuwa mpuuzi huyo msimsikilize? Leo anajikosha. Tutaona mengi mwaka huu.
 
Nape kutamka hadharani kwa kumpongeza Lowassa kwa kutii agizo la chama kwa kusitisha kampeni kabla ya wakati ni wazi kuwa Lowassa wins ilhali Nape lose.

Ni dhahiri shahiri kuwa Nape amesoma alama za nyakati na kutambua kuwa "MAFURIKO HAYAZUILIWI KWA MIKONO".

Umefanya vyema Nape ili hapo baadae uishi kwa amani katika nchi uliyopewa na Bwana Mungu Wako.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Mbariki Lowassa,Mungu Ibariki Tanzania.
 
Nape Nnauye amempongeza comrade Edward Ngoyai Lowassa kwa uwezo wake wa kisiasa na kwa kupendwa na watanzania wengi ambao wamekuwa wakijitokeza kumuomba agombee urais mwaka huu. Haikuweza kufahamika mara moja kama pongezi hizo ni za kheri au za kinafiki kwa kuwa siku chache zilizopita Nape alisikika akimbalaza Lagwanan Lowassa kwa kuwachochea wananchi wanaomiminika nyumbani kwake kumshawishi achukue fomu ya kugombea urais wakati muda wa kampeni haujawadia.

Chanzo: Magazeti ya leo.

MAONI YANGU
Nape ni ndumilakuwili wa hali ya juu na hayafai kabisa kuaminiwa kwa jambo lolote analolitamka. Inawezekanaje leo ambaraze mtu na kesho abadilike na kuanza kumsifu mtu huyo huyo? Nimeamini Nape ana akili za kitoto sana.

:israel:
 
Last edited by a moderator:
Nape sawa na Zito anaye sema Ukawa wasaka tonge Huku tena anasema Ukawa ndo mbadala wa kuiondoa ccm madarakani
 
Nape anacheza ngoma asioijua!

sio tu kwamba anacheza ngoma asiyoijua bali amechanganyikiwa na ameshikwa na kihoro baada ya kushindwa kuzuia mafuriko kwa mikono. amini nakuwambia Lowasa akiingia whitehouse mwezi wa oktoba, Nape atafute nchi ya kuhamia.
 
Nape sawa na Zito anaye sema Ukawa wasaka tonge Huku tena anasema Ukawa ndo mbadala wa kuiondoa ccm madarakani

yeah! hili ndio tatizo la wanafiki na wasioweza kutunza kumbukumbu. ukiwa mnafiki sharti uwe na kumbukumbu nzuri usijejikuta unalamba matapishi yako mwenyewe. nchi hii inashindwa kupiga hatua za maendeleo kwa sababu ya mijitu minafiki kama hili Nape Nnauye.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom