Napata ndoto za kutisha baada ya kwenda kwa mganga wa kienyeji

Kwanza naona wote wanakupotosha wewe uliambiwa mila za kwenu ndio chanzo, sasa bila kwenda kumaliza hizo mila hakika hutasimama katika kipato chako. Kwanza jiulize ndoto huwa zinatoka wapi unahitaji ushauri upo gizani. Ndoto ni taarifa kutoka kwa malaika wako Mungu aliokujaalia sasa umeonyeshwa maisha yalivyo Ili utafute ufumbuzi. Hayo mambo ya bibilia hayamsaidii mtu kama umeacha mila na desturi zako
 
Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.

Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana.

Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapotea.

Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea.

Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji.

Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni

Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
Siku ya kwanza ukakuta nyomi
 
Biblia inasema, "KUFANIKIWA KWA MPUMBAVU KUTAMUANGAMIZA"

kamwe usikubali Kumsujudia shetani ili upate mali....

Shetani alimuonyesha Yesu milki yote ya Dunia na fahari yake kisha akamuambia "Ukiinama kunisujudia nitakupa"

......itakufaidi nini ukipata utajiri na mali zote za dunia ukamkose Mungu?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Unachoongea ni kweli kabisa lakin kupitia huu Uzi watu wameshamfata dm wengi kumuuliza location ya mtaalamu

Changamoto kubwa ni kanisa haliwezi kutumia ulimwengu wa kiroho kama wa upande wa pili ili kutatua changamoto za wakristo, watu wanaenda na mizigo Yao kanisani na wanarudi nayo kinachofuata ni nin lazima watafute option nyingine

Kanisa na wakristo wafundishwe jinsi ya kutumia damu ya YESU Hilo ndo shuluhisho la kudumu
 
Nadhani kama hudanganyi wewe 'Ulikuwa mtoto Mchanga kiroho'ndiyo maana ulikuwa unachanganya masomo.In maana ulikuwa huna mafundisho ya kutosha ya Neno la Mungu.
Lakini sasa tubu na umrudie Mungu!
 
Wewe siyo wa kwanza kupitia Economic crisis Mkuu..

Tatizo hukupata ushauri sahihi matokeo yake ukashauriwa kuziendea njia za giza..
(kumsujudia Shetani)

Itakufaidi nini ukipata milki zote za Dunia halafu ukamkosa Mungu?

Kwa maana Shetani anao uwezo wa kukupa mali...lakini Mwisho wake ni Kifo tena cha Ghafla ili usipate Muda wa kutubu....

Na hiyo Dhambi utaona ni ndogo lakini...itakuandama wewe na uzao wako wote na ni machungu yasiyo na mfano...

Wewe unajiangalia binafsi yako lakini shetani analenga madhara yatakayokuandama vizazi vyako vyote...

Unajisikiaje unaendesha gari, una nyumba, na mali nyingi halafu moyoni mwako unajua wazi Mdhamini wako ni Shetani?

Hili jambo linaumiza nafsi za wengi wanaopata mali kwa njia za uganga na uchawi sema hawasemi...

SHETANI AKIKUKOPESHA UTALIPA, HATA KAMA UTACHELEWA KUDAIWA.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Well said
 
Nadhani kama hudanganyi wewe 'Ulikuwa mtoto Mchanga kiroho'ndiyo maana ulikuwa unachanganya masomo.In maana ulikuwa huna mafundisho ya kutosha ya Neno la Mungu.
Lakini sasa tubu na umrudie Mungu!
sidhani km Ayubu alikuwa mchanga kiroho alipojaribiwa. sema nimeshindwa kuvuka jaribu langu.
 
Endelea kuroga.....endelea kuroga.....endelea kuroga mpaka kieleweke zaidi ya hapo......

Haya maisha yana Siri nyingi mkuu!!!

Hao hao wachungaji na manabii Wana chale adi mku***ni
 
sidhani km Ayubu alikuwa mchanga kiroho alipojaribiwa. sema nimeshindwa kuvuka jaribu langu.
Sasa Ayubu alienda kwa Waganga wa Kienyeji pamoja na majaribu mazito aliyopitia?
Mtu ambaye amekomaa kiroho anakuwa tayari kwa lo lote hata kufa lakini siyo kuiacha Njia na kumgeukia Shetani hata kama anapita katika majaribu makubwa kiasi gani.Ndiyo mfano wa Ayubu sasa!
 
  • Thanks
Reactions: _ly

kusema hivyo ww uliyekomaa kiroho hutendi dhambi?
 
Maathayo 7...

21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
bibi acha kujichanganya, mitishamba ni dawa kimwili na kiroho. si mwiko kuitumia

EZEKIELI 47:12
Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; NA MAJANI YAKE (MTI HUO) YATAKUWA NI DAWA.

MWANZO 1:11-12, 29-31
Kila kilichoumbwa na Mungu kilikuwa ni chema sana. Mungu asingeumba kamwe kitu chochote kibaya. Mungu aliumba mimea ya kila aina mingine ya dawa, chakula na kadhalika.
 
Nilijenga msingi mzuri wa imani yangu kwa Mungu, kuwa ndio anayeweza kunitoa kwenye hili dimbwi la kukosa kipato licha ya kugraduate since 2014 hizi digrii yeboyebo. Japokuwa Mungu alinisaidia kupata kazi za mikataba ya muda mfupi lakini mishahara ni ile ikizidi sana ni laki nne, sehemu nyingi niliambulia laki mbili, mpk laki moja kwa mwezi.

Kutokana na majukumu ya kusomesha mtoto na mama yake, kwangu inakuwa ni ngumu kusogea kimaisha. Hivyo muda mwingi ninakuwa kwenye stress ya kipato kidogo na madeni mengi.

Nilijitahidi kuwa muaminifu kwenye fungu la kumi na sadaka, maombi na kujitoa kwa kiwango kizuri kumtumikia Mungu. Nilitegemea nikifanya hayo angalau nut zitaanza kulegea kwenye uchumi, lakini ndio mambo yakazidi kuwa magumu sana.

Madeni yakaongezeka kwa sababu natakiwa nilipe ada ya mtoto na mama yake(nilimpa mimba dent kuepuka mvua 30 ikabidi nibebe jukumu la kusomesha private school. kwa sasa anamalizia six on May)

Mapema February kuna jamaa akanishauri anipeleke mahali nikaangalie kwa nini nakula msoto hivi licha ya bidii ninayowekeza kutafuta noti. Bibi wa kupiga bao akaniambia shida yangu ni ishu za mila za kwetu na NYOTA yangu imechezewa. Hivyo, nikamilishe mambo ya mila then nitafute fundi wa kusafisha nyota.

Nikapata ushuhuda mahali kuwa kuna fundi mzuri wa hayo mambo, kwa buku mbili tu ana darubini za kuona rohoni mwako. Siku ya kwanza nikaenda nikakuta nyomi, nikafanikiwa kumuona nkaeleza shida akaniambia nina nyota ya kutoa tu, ila ya kupokea, kutunza na nyingine nmesahau zimefungwa. Nikapewa dawa ya kuogea baada ya kurudi nyumbani

Usiku wa siku nliyotoka kwake, nikaota kuna mtu ananifukuza na ananitupia mishale mingi. Nilipambana kuikwepa kwa nguvu zangu ikashindikana lakini nikakumbuka kukemea kwa jina la Yesu mrusha mishale akapotea.

Nikarudi kwa doctor siku ya pili kwenda kufanyiwa huduma kuu yenyewe ya kusafishwa nyota. usiku wake tena baada ya kutoka huko nikaota tena kuna nyoka black ananishambulia kwa kunirushia mate ya sumu, nilipambana kwa nguvu zangu lkn alitaka kunizidi nguvu, nkakumbuka kukemea kwa damu ya Yesu ndio akapotea.

Nilimpigia kalmanzila kumueleza kuhusu hizo ndoto, akaniambia nirudi akanipe kinga...mpaka muda sijarudi tena huko

Matokeo baada ya huduma yake, ni kuwa nimepata kazi japo ni ya muda mfupi lakini ina maslahi mazuri na kuna HR wa shirika moja zuri aminiahidi soon kuna neema inatoka kwenye shirika lao nitakuwa front line kwa sababu ni qualifications zote na experience wanayoihitaji.

Naweza kusema angalau naona mabadiliko kwenye suala la kibali tofauti na mwanzoni

Sasa wanajamvii nauliza, nirudi kwa kalmanzila nikamalizie dozi au nikatubu nimrudie Mungu.
Mambo naomba nipe no ya mganga wako tafadhali mm jina shida ya mahusiano
 
Acha Ujinga ww nenda huko kamalizie Tiba yako na endelea na ibada zako km kawaida Kwan kuna MTU anaekataza kuwa na source mbili za kipato sindo Vizuri hata mlevi wa Bar kwenda kutumia pombe za kienyeji hakuna shida lengo ulewe tu km unaona mabadiliko endelea na usisahau na ibada pia
 
nifanyeje kiongozi, hawa watu waliweza kuona nyota yangu haijakaa sawa. Kwenye bible kuna vifungu na muongozo mzuri wa kusafisha kibali changu ili mambo yaniendee vizuri. kama ulishawahi pitia maisha ya kukaa mwezi bila kuingiza hata mia utaelewa. efforts zangu haziniletei matunda
Acha upumbavu wewe, Mungu ni mganga wa waganga, hujasoma habri za Daniel..
Kaaa tulia na Mungu wakati wa Mungu ni sahihi, ukimtumkia Mungu kwa uaminifu ni swala la mda tu trust me kabla hujafa utakuwa ushakula sana baraka za Mungu.
 
Back
Top Bottom