Kaunga, Relax....
Acha nature nayo ichukue mkondo wake. Mfano; siku mwanao alipoanza tambaa.... Si ulimuogopea anapokwenda atajiumiza? ...lakini yeye mwenyewe hakuacha jaribu kusimama mpaka akajifunza na kutembea.
Assure him you are and will always be there for him...He will be Ok.
oooh jamani
soo sad
sijui kama mtoto wangu nitaweza kumpeleka boarding aisee
hapa tu sijamzaa nammiss vibaya mno
kweli mbuLoL, wewe Smile wewe....
My son anaenda kuanza form one, (preform one next month) boarding school he is going to be 12 next year.
As a mother namuambia nini? Nafeel kuna kitu napaswa kumwambia sijui nimwambie nini na jinsi gani.
Sijasoma boarding school O'level so sijui kunakuweje, nasikia ushoga unaanziaga huko. Bullying inanitia wasiwasi ukizingatia umri wake ni relatively Mdogo.
Nisaidieni nini cha kuongea naye.
N.B Namlea mwenyewe as a single mom.
Ila wifi unajua bado natafakari hili toka jana. Ina maana huyu mwenetu anamiliki simu tayari? Why? Manake ba unoko wangu ningemuwekea ttcl kabisa ili nimpigie mwenyewe. Kids dont need simu jamani.
Hata mimi la simu nimejifikiria nikasema labda mimi ni wa zamani...
Maana kuna mambo ya kwenda na wakati...wenzake wote wana simu yeye kama hana atajiona mnyonge...
Kwa kweli sijuhi kama shule zote zinaruhusu mtoto kumiliki simu...
na sijuhi umri gani ni proper kwa mtoto kuwa na simu...
Unajua akishakuwa na simu maana yake ana access na internet...hapo ndio balaa linapoanza.
ha haaaa, kumbe wazee tupo wengi? lol!Hata mimi sikubaliani na mambo ya simu kwa watoto wadogo. Hata Tv huwa wanaangalia kwa ratiba maalumu. Hivi vitu. ni vizuri ila pia madhara yake ni makubwa!
Wakati mwingine unatamani uwe mlinzi wa yule umpendae hata mahali ambapo NGUVU KUU inahusika na usimamizi huo,usijani sweetie,he'll be fine as long as Jesus is there for him . . . . !!
Jamani sikumbuki kutukana Boflo, ila kama nimeshawahi; nisamehewe.
sijasema kumpa mtoto hela nyingi maana yake hatakuwa mzuri darasani.Kumbuka this kid goes to Feza, may be you huifaham ipo vipi? Chakula ni kizuri sana but canteen napo kuna various options as most of kids wanakuja na pocket money nzuri.. So atleast mtoto asijisikie vibaya wenzake wakinywa soda etc awe na pocket money nzuri.... I remember those days watoto wa kiarabu wanawekewa mpaka bills na mama zao wachukue wanachotaka anytime at schools na bado hao watoto wanakimbiza darasan na wengi wao wanaongoza family business baada ya varsity.... Kumpa mtoto wa sekondari pocketmoney nzuri sio kumuharib but unaaanza kumfundisha financial management mapema as wengi tulikuwa tunaseve hela tukirudi likizo tununue sneakers etc
Kabla hatujawa mabest au baada?
(i) simu umempa saa hizi wakati anaenda shule au alikuwa nayo tangu zamani?FP sijajibiwa bado, madhara ya simple simu kwa 11yrs boy ni yepi?
Sababu ya kumpa ni kuwa naye mbali, mimi niko kwenye one end of the country naye yuko kwenye another.
Anaitumia weekend tu, tena ni zile weekend ambazo anakuwa amechukuliwa na uncle zake (shule hairuhusiwi)
Tunaongea 2 times a day, the rest tunabofyana tu kwa SMS.
Sioni tatizo, na hakuna tatizo lililotokea so far.
(i) simu umempa saa hizi wakati anaenda shule au alikuwa nayo tangu zamani?
(ii) kwa nini usitumie simu za hao ma-uncle kuwasiliana naye?
kama ndo kwanza umempa simu hutaweza kuona madhara kwa haraka hivyo. ila kadiri network itakavyoongezeka ndo utaona madhara. Mtoto ambaye anatumia simu ya mzazi, ni ngumu sana kuwasiliana kwa uhuru na watu ambao si muhimu sana kwake, ila aliyekuwa na simu yake anaweza akafanya lolote. Juzi kuna mtu alileta mada hapa anashangaa binti wa kama miaka 13 kamuomba namba ya simu na kampigia kumwambia anampenda. nina uhakika huyo mtoto asingekuwa na private simu asingefanya hivyo.
Tukubali/ tukatae, kuna hali ambayo watoto wetu wanapitia wanapokua, wote tulipita huko, na tunajua nini yanatutokea. Mungu ni mwema anaweza kusaidia mtoto wako asiathirike sana na ile negative side ya ukuwaji, ila pia ni jukumu lako mzazi kumpunguzia mwanao kila kitu ambacho unadhani kinaweza kuwa kichocheo cha hayo mambo.
Mimi mara nyingi huwa napokea sms za binti, lakini kwa vile wanaomtumia wanajua namba ni ya mama basi zinakuwa za adabu. kama huko shule hawaruhusu simu, mimi nadhani unaweza wasiliana na mwanao nyumbani kupitia simu za uncle zake.