Naona tatizo lile lile la Kimsingi limeendelea kujirudia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,127
Niseme tu kwamba hakuna ulazima wowote wa kutaka kumuiga Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere jinsi ya kuhutubia hadhara bila ya kusoma mahala popote. Binadamu tunatofautiana sana tu na ikumbukwe kwamba naturally Nyerere alikuwa ni historian hasa hivyo kuzungumza mara kwa mara Kwake kulikuwa ni jambo rahisi mno na ambalo aliliweza pia.

Sisi akina GENTAMYCINE ambao naturally ni Scientists tutake tusitake hatuna ' ubavu ' wa kuzungumza vizuri na kiufasaha kabisa bila ya kuwa na mwongozo wowote wa Kimaandishi ( hapa namaanisha Hotuba nzima iliyoandikwa )

Yafuatayo ni madhara makubwa ya Wanasayansi akina GENTAMYCINE kupenda kuzungumza mbele ya hadhara bila kusoma katika kile ambacho nimeandikiwa na nimeandaliwa Kukizungumza kwa wanaonisikiliza:

  1. Kupayuka sana
  2. Kuongea pumba nyingi
  3. Kurudiarudia jambo lile lile
  4. Kupoteza ' calories ' nyingi na kila mara ukajikuta unakunywakunywa tu mimaji
  5. Kupandwa na Hasira kwakuwa utajikuta unaibua kitu ambacho hukutakiwa kukisema
  6. Kupoteza muda ambao uliandaliwa kuwepo eneo la tukio
  7. Kuwachosha / Kuwaboa Watu japo wanaweza wasikuonyeshe ila mioyoni wanakusanifu tu
OMBI

Wanasayansi wenzangu hebu tujitahidi sana pale tunapokuwa tunaongea mbele za Watu basi tujitahidi au tuwe tunawaomba ' Wasaidizi ' wetu wawe wanatuandalia ' Hotuba ' zetu ili tukiwa tunaongea basi kweli tuonekane kwamba Sisi akina GENTAMYCINE ni ' Wanasayansi ' wa ukweli na hatukubahatisha kupata Degree, Masters na PhD's zetu.

Nawasilisha.
 
Mkuu
 
Hayo ni maoni yako binafsi, ukiniuliza mm ntakuambia mkuu kahutubia vizuri tu na nimemuelewa.
 
Hayo ni maoni yako binafsi, ukiniuliza mm ntakuambia mkuu kahutubia vizuri tu na nimemuelewa.
Utaelewa siku atakapo chaguliwa na wa kigoto pekee yao ndiyo utashindwa kuelewa. Upendeleo ni tabia ya mtu muovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…