Naona kama ananijaribu...

Starwars91

Member
Jul 12, 2020
52
47
Nilikutana na Dada mmoja mzuri kiasi. Nikamuomba namba. Nikawa nachat nae kidogo siku kadhaa nampotezea. Nikamuomba kidogo tukakae mahali tuongee alikubali. Nikakaa kama mwezi weekend moja nikasema niko free twende tukae mahali tuongee. Akaja kweli, tukakaa, tukanywa, tukala tukabadilishana mawili matatu nikamwambia shida yangu. Akaniambia ana mpenzi na anajulikana mpaka kwao. Lakini kabla ya hapo kila nikimuuliza alikuwa ananiambia hana.

Sasa najiuliza alijua namtaka, nikamwita akaja, akanisikiliza akajumuika na Mimi. Kama kweli ana mtu anajulikana mpaka kwao, inakuwa je akubali kuja kujumuika na Mimi tena wawili tu? Je ananipima au anamaanisha? Kama muda wote hakuniambia, mpaka tumetoka, ndo anasema ana mtu wake, ina maana kabla ya huko kote asingeweza kukaataa kutoka out na Mimi kisa ana mtu? Nataman kupotezea lakin roho inakataa. Nahisi ananipima. Wanawake hawa jamani.

Changieni mawazo kidogo watanzania.
 
Bila shaka sababu ni hii.

Na Brother usihofu, ni mizani yake tu, ila ukijaribu kwa mizani ya mwanamke mwingine utafiti.

So achana nae , usiwaze wala hizo sababu.

Be you, na anayekustahili atakaa na ww.
Me naamini mwanamke wakati unamwingia tu tayari anakuwa kashajua nia yako. So, na wao huwa wanaanza kukupima kama ambavyo sisi uanza kuwapima. Ukifiti wala hutakuwa na haja ya kumtongoza atajaa mwenyewe.
 
Mkuu kanishangaza sana. Kwa sababu yan mpaka kanifata mwenyewe lakin mwishoni eti kabadili gear angani.
 
Inawezekana kweli ana mtu wake ama hajavutiwa na wewe baada ya kukaa na wewe masaa kadhaa kimaongezi,muonekano wako na mazaga zaga kama hayo

Kama unaweza jitafakari ulikosea wapi mlivyokutana halafu umtafute tena labda atakukubali ama kubaliana na maneno yake kwamba ana mtu wake

Hata hivyo kutoa namba,kukutana na mtu sio kigezo cha mtu kukutaka kimapenzi
Mimi naweza kufanya hayo yote na nikakukataa kiroho safi
 
Inawezekana kweli ana mtu wake ama hajavutiwa na wewe baada ya kukaa na wewe masaa kadhaa kimaongezi,muonekano wako na mazaga zaga kama hayo

Kama unaweza jitafakari ulikosea wapi mlivyokutana halafu umtafute tena labda atakukubali ama kubaliana na maneno yake kwamba ana mtu wake

Hata hivyo kutoa namba,kukutana na mtu sio kigezo cha mtu kukutaka kimapenzi
Mimi naweza kufanya hayo yote na nikakukataa kiroho safi​
Cjui nilicheza wap foul? Kwa kweli sijui nilicheza wap?
 
Back
Top Bottom