Naona jamii yetu ya siku hizi wanaona single parenting kama kitu cha kawaida

kamba0719

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
804
1,904
Sijui kwa upande wenu ila kila nikitizama siku hizi single parenting imekuwa kama trend yaani kitu fulani ambacho vijana hawakiogopi.

Nikitizama zaidi nawaona hawa wana saikolojia/motivation speakers ambao kidogo wamebase kwenye biashara hili jambo wamelichukua kibiashara zaidi. Mfano siku hizi kuna makongamano ya jinsi ya single father/mother wanavyo takiwa waleee watoto, nimeona imekuwa kibiashara zaidi.Naona kuna vipindi mpaka vya TV vya kuwaelimisha single parenting jinsi ya kuwalea watoto wao.

Ila sijaona juhudi za kukazania jinsi ya kuwajenga vijana wapende maisha ya familia, maisha ya ndoa, umuhimu wa familia.

Najua jamii yetu imekengeuka vijana siku hizi hawataki kubeba majukumu yao, jamii yetu imekuwa shaghala baghala,Jando na unyago hatutaki kuvisikia na maisha ya wakubwa ambayo vijana wanatakiwa kujifunzo kupitia wao nao wanahisi maisha ya hovyo.

Kila nikitizama kama tumeamua kuupromote huu usingle parenting now kupitia media na hizi semina (sio kitu kibaya kuwatia moyo single parents) ila naona kama mafunzo ya kuwaeleimisha vijana kuishi maisha ya ndoa na familia yao kama tuna yapuuzia.

Sijui kwa wengine ila kwangu kuna kitu na kiona sio kizuri kwa jamii yetu ijayo.

Naamini familia bora,hutengeneza jamii bora na taifa bora.
 
Tatizo ni kwamba watawala ni sehemu ya uovu katika Taifa lolote linalopuuza maadili . Wanasiasa wengi ni wahuni na wanafanya uhuni na umalaya Kwa uhuru zaidi panapokuwa na single parent wengi.

Ni Awamu yenye wahuni Kwa Mujibu wa Komredi ,mzalendo, mcha Mungu,shujaa na mwadilifu Hamfrey Polepole.
Tatizo linaanzia pale Bungeni na ndani ya vyama vya siasa .
Kuna mabilioni yanatolewa kufadhili promotion ya single parent lakini hakuna hata mtu anayezungumzia uadilifu ndani ya Ndoa na namna ya kulinda ndoa na hata kuweka SHERIA ya kulinda Wana ndoa waadilifu wasibughudhiwe na watu walaghai wanaotumia fedha na madaraka kuhujumu ndoa za watu .

Taifa lisilo na maadili Haliwezi kuwa na Wazalendo .
Watu wengi Wanahasira na chuki kubwa sana kuhusu mahusiano ndani za ndoa na hata uchumba kwasababu za usaliti.
Walioko juu wanaona ni sawa ila Hali itakua mbaya sana muda sio mrefu.

Vijana wasio na matumaini ya kuishi ndani ya Ndoa na kuwa na familia ni hatari sana . Kuna siku watu wataingia kwenye uhasama Kwa sababu ya mambo madogo sana kutokana na stress zinazowakumba watu hasa wanaume . Watu wa namna hizo hawana Cha kupoteza . Ni hatari Kwa usalama wa nchi na amani ya kweli Kwa Taifa. Wanaume wengi wanakuwa wastaarabu Kwa sababu wanaogopa kuacha familia zao.Usione wakenya wanaandamana au Sudani . Watu Wana matatizo kuanzia kwenye familia.

Nakumbuka wakati ule wa Ngangari na Ngunguri . Lipumba na Dr.Slaa walikua na ujasiri mkubwa . Waliosoma Cuba wamenielewa.

Serikali inapaswa kuonyesha Kwa vitendo kuchukizwa na huu uhuni unaozoeleka wa single parent na kujenga Taifa la watu malaya Malaya .
Viongozi wa dini wanapaswa kukataa kabisa kuendelea kuwasifia watu walioshindwa kujenga Taifa kiuchumi na kijamii. Wameshindwa hawafai hata mbele za Mungu. Kuwavumilia ni kuliweka Taifa Zima chini ya laana na kusubiri adhabu Toka Kwa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom