Kuna Hii kitu inaitwa "Convert Incest", njoo nikuelezee.

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,999
Reaction score
23,543
Covert Incest au Emotional incest ni aina ya unyanyasaji ambao unahusisha mzazi/mlezi kutegemea msaada wa kisaikolojia au ushauri wa kisia kutoka kwa mtoto wake ambao alitakiwa kuupata msaada huo kutoka kwa watu wazima wenzake anaolingana nao au waliomzidi umri.

Neno covert humaanisha siri au nyemelezi au chinichini au kimya kimya, wakati neno incest humaanisha muingiliano usiokuwa wa kaiwaida au kiafya baina ya watu wawili ambao wanashare damu.

Hii kitu imekuwa normalized sana kwenye jamii yetu kiasi kwamba imefikia hatua inafanyika kwa kiwango kikubwa na inaonekana kuwa ni jambo la kawaida sana ile hali kuwa ni form of abuse.

Sasa tukumbushane kuwa tukikubaliana kwamba jamii yetu inapashwa kupambana sana kukomesha aina zote za abuse iwe ni emotional au physical abuses ili tuwe na watu wenye afya imara ya akili.

Kwa takwimu za kitaa, wanawake ndio wanaoongoza kwa kutenda abuse hii kwa watoto wetu kwa kiwango cha kutisha sana.

Ni mara ngapi umekutana na binti wa miaka 15 ila kifuani ana chuki ya kutisha juu ya wanaume hadi unajiuliza huyu binti hii chuki ameitoa wapi. Binti anakwambia mimi sitakuja kuolewa nitazaa na kulea mwenyewe.

Au unakutana na binti mrembo tu ila eneo la mahusiano anakuwa kama ashikwa na pepo anashindwa kusettle na wanaume sababu ana hofu ya kufanyiwa kitu kibaya kuumizwa hisia, kutelekezwa, kunyanyaswa.

Je umeshawahi kujiuliza kama hili jambo ni la kawaida?

Mtoto akipigwa tunashtuka na kuita abuse, mwanaume akimtukana na kumpiga mkewe tunashtuka sababu ni abuse, binti akiomba kazi akaombwa kutoa uroda tunashtuka sababu ni abuse, tunashtushwa na haya yote sababu elimu imeshatolewa na tumeweza kuyatambua kuwa yana madhara.

Ni muda muafaka sasa tuliongeze na hili la Covert Incest kwenye mijadala yetu sababu ni miongoni mwa vyanzo na chanzo kikubwa cha ongezeko la single mothers, fatherless kids, Emasculated males, Toxic masculinity na vinginevyo vinavyotuharibia muktadha wa malezi na ujenzi wa familia bora.

Tukemee.
 
Dalili za mtu anayefanya "Covert Incest".

1. Kumtegemea mtoto akupe faraja, utulivu, na msaada wa kimawazo na hata kifedha muda mwingine.

2. Kuomba ushauri kwa mtoto ambao ni nje ya rika, umri na uwezo wake wa kudadavua mambo. Mfano unamhadithia mtoto madhira ya mume au bwana wako ili kupunguza stress. Au changamoto za ndugu zako au marafiki zako.

3. Kuingilia faragha ya mtoto wako mfano kutaka kujua anadate na nani na kufuatilia mahusiano yake wakati ameshavuka miaka 18 au zaidi. Unamgeuza shost yako na kutaka akuhadhithie mambo yake as if ni shoga yako.

4. Kumchukulia mtoto kama replacement ya mwenza. Mfano masingle mother husema huyu mtoto ndio baba yangu, ndio mume wangu, yeye ndie kila kitu changu. Sihitaji mwanaume. Unamtumia mtoto kama replacement ya mwanaume kiasi kwamba akija binti anataka kuanza nae mahusiano unamuona kama anakunyang'anya mume au partner wako wa maisha.

5. Kutarajia mtoto awe source ya inspiration na praising number one fan wako. Hii ipo sana kwa masingle mother pia kutaka mtoto ndie awe cheering fan wako, na kutaka asheherekee na kuwa proud na zile harakati zako za kupambana na maisha ukimpambania sababu hakuna anayekupongeza wala kukupa heko. Hii ni abuse kwa mtoto.

6. Wivu mtoto anapoingia mahusiano na mwanaume au mwanamke aliyependana nae. Nadhani hili tumelishuhudia sana. Mama kugombana na mkwewe sababu anaona atanyang'anywa kijana wake na attention itahama.

7. Kuharibu mahusiano ya mtoto ili kuweza kumcontrol mtoto na kuzuia influence ya mwanaume au mwanaume mwingine kwenye maisha yake.

8. Kujadili mada chafu za ngono, uasherati na zisizo na maadili mbele ya mtoto bila aibu wala tahadhari (hivi ni tahadhari au tahadhali)
 
"covert incest" sio abuse ni hali ya kihinsia ambao ni involutary inao hitaji tiba ya kisaikolojia,.......naomba ujifunze zaidi hiyo hali, usitegemee hao wanao tafsiri kiingereza kwa kiswahili wata kulisha matango pori, mkuu.
 
Madhara ya Covert Incest

1. Mtoto hupata madhara ya kudumaa maeneo ya hisia, mahusiano, jinsia, na mahaba. Tabia ya mzazi kumtemea sumu za maisha yake huathiri uwezo wake wa kupenda watu wa rika lake, humfanya kushindwa kutengeneza emotional bonds sababu ya kuona negative outcomes kwa jambo ambalo hata halijatokea na mbaya zaidi kukosa uwezo wa kuunda na kukuza mahaba na mwenzake.

2. Mtoto anakuwa na mahusiano ya upendo uliochanganika na chuki ndani yake dhidi ya mzazi wake kiasi kwamba anashindwa kuprocess nini maana ya mzazi katika maisha ya mtoto na yeye anajikuta anachukia maisha yake na kuwa na majuto kwann alizaliwa kwa mzazi huyu lakini pia hawezi kuendelea mchukia sababu ndie kamleta duniani.

3. Mtoto kupata ugumu kuanza au kufanya mahusiano serious kwasababu ya hofu mzazi ataingia na kuyaharibu, kuhofia tabia ya mzazi wake kutaka details za mahusiano, kuwaza mwanaume au mwanamke wake atamuweka wapi ambapo mzazi hatakuja waingilia etc.

4. Kuwa na low self-esteem. Mtoto anashindwa kujikubali na kukosa amani muda wote katika maisha yake anaishi kwa wasiwasi kama mfungwa anayetazamwa na askari. Maisha yake yanakuwa na huzuni wa chini chini ila hatakwambia.

5. Kushindwa kujitambua ni nani au mtoto wa nani kutokana na kukosa thamani ya utoto kwa mzazi. Mtu yoyote anayefanyiwa abuse hupatwa na hii hali ya kukosa identity. Mfano, ukibakwa unakosa nguvu ya kujiamini kama mwanamke, au ukilawitiwa unakosa nguvu ya kujiamini kuwa ni mwanaume tena. Ukipigwa na baba yako inakunyima nguvu ya kuamini kuwa unaweza kuja kuwa na mtu mwenye kuheshimiwa, ukitukanwa na mkeo mbele ya watoto au ukitukanwa na mumeo mbele ya watoto unakosa kujiamini kwenye mamlaka ya kuwa baba au mama mbele yao.

6. Mtoto atajenga tabia ya kupenda kuwa people pleaser sababu hajui thamani yake na hauelewi nini anahitaji kwa watu wengine.

7. Matatizo mengineyo ya kiakili kama stress, anxiety, kukosa usingizi, kuumwa kichwa mara kwa mara, uvivu, kuwa na hasira kali za ghafla, kuwa na majibu mabaya ya dharau, kuwa antisocial na kadhalika.
 
"covert incest" sio abuse ni hali ya kihinsia ambao ni involutary inao hitaji tiba ya kisaikolojia,.......naomba ujifunze zaidi hiyo hali, usitegemee hao wanao tafsiri kiingereza kwa kiswahili wata kulisha matango pori, mkuu.
Umemaanishaje sasa hapa mbona kama haujajua unachokisema.

Unasema ni hali ya kihisia kwa mlengwa au muhanga?

Kumbuka ili process itokee lazima kuwe na muhusika yaani msababishi halafu kuwe na mhanga.

Watoto ndio wanakuwa wahanga na wasababishi ni wazazi au walezi. Sijui umesoma nilichoandika ukakielewa vema mzee.
 
Namna ya muhanga wa Covert Incest ataweza kujitibu na hii abuse aliyoipata kwa wazazi wake kabla na yeye hajakwenda nayo kwa watoto wake na kurudia kosa.

1. Hatua muhimu ni utambuzi kuwa upo katika mazingira ya kutendewa hii Covert Incest na mzazi au mlezi wako. Utatazama viashiria ambavyo vitakuonyesha mahusiano yako na mzazi wako au mlezi si yenye mipaka na yanaonyesha kila dalili kuwa na walakini na sio kawaida. Nimeainisha kule juu dalili za mahusiano kati ya mzazi au mlezi yanayoashiria wapo katika Covert Incest relationship.

2. Mtoto anatakiwa kuweka mipaka na mzazi ambaye anamuendea kwa aina ya mazoea ambayo si ya adabu na yasiyo na mipaka. Mfano, mama yako anakuhadithia wewe binti mambo yamhusuyo baba yako ambayo ni ya kimapenzi, au mambo ambayo wewe binti hupaswi kuyasikia toka kwa mama yako kuhusu wanaume then mara moja mkatishe au muonyeshe hauna sababu ya kumsikiliza au kukaa nae kuongelea hizo topic sababu wewe haupaswi kuzisikia wala sio size yako.

Kama mzazi atakuwa bado anakutengenezea mazingira ya kukuingiza katika mazingira ambayo yanakuweka uncomfortable kuzungumza nae unaweza kuhama kabisa mazingira alipo na kwenda kuishi mazingira ambayo utahisi upo salama na haupii wala haufikiwi na tabia zake.

3. Tazama ni maeneo gani ambayo tayari ulishaanza kuathirika mfano fikra zako kuhusu mahusiano, au kushindwa kubond na jinsia tofauti, au kumchukia baba yako, au kushindwa kuwa na emotional connection na jinsia tofauti then anza kutafuta msaada mapema kabla madhara hayakomaa na kuunda tabia.

4. Jaribu kutafuta role models ambao wanaweza kuwa ni wazazi wa rafiki yako wa karibu, ndugu wa karibu wa familia, mwalimu, au mtu ambaye anakuonyesha mfano mzuri na uweze kufuatilia nyendo zake na kujijenga kupitia yeye na kuweza kupata msaada wa kimalezi kupitia mtu huyo ili upate parenting energy ya kukukuza ukue na kuwa imara.

5. Tengeneza mtandao wa msaada kwa kuwa na marafiki au ndugu ambao unaweza waendea pale unapoelemewa na madhara ya abusive behavior ya mzazi wako ambaye amukuwa akikuandama.

6. Jitahidi usije kurudia tena tabia ile ile ya covert Incest kwa watoto wako. Jitahidi kubreak the cycle sababu kuna guarantee kubwa kwamba alivyokulea mzazi wako ndivyo na wewe utalea vile vile watoto wako.

7. Muhimu zaidi, nenda kwa wataalamu wa afya ya akili (psychological therapist) waweze kukupa therapy ya kukutoa na kukupa ufahamu wa shida gani ulikuwapo ndani yake na namna ya kutoka. Hii hali inatibika na inamalizika na mtu kurudi sawa kabisa.
 
Dalili za mtu anayefanya "Covert Incest".

1. Kumtegemea mtoto akupe faraja, utulivu, na msaada wa kimawazo na hata kifedha muda mwingine.

2. Kuomba ushauri kwa mtoto ambao ni nje ya rika, umri na uwezo wake wa kudadavua mambo. Mfano unamhadithia mtoto madhira ya mume au bwana wako ili kupunguza stress. Au changamoto za ndugu zako au marafiki zako.

3. Kuingilia faragha ya mtoto wako mfano kutaka kujua anadate na nani na kufuatilia mahusiano yake wakati ameshavuka miaka 18 au zaidi. Unamgeuza shost yako na kutaka akuhadhithie mambo yake as if ni shoga yako.

4. Kumchukulia mtoto kama replacement ya mwenza. Mfano masingle mother husema huyu mtoto ndio baba yangu, ndio mume wangu, yeye ndie kila kitu changu. Sihitaji mwanaume. Unamtumia mtoto kama replacement ya mwanaume kiasi kwamba akija binti anataka kuanza nae mahusiano unamuona kama anakunyang'anya mume au partner wako wa maisha.

5. Kutarajia mtoto awe source ya inspiration na praising number one fan wako. Hii ipo sana kwa masingle mother pia kutaka mtoto ndie awe cheering fan wako, na kutaka asheherekee na kuwa proud na zile harakati zako za kupambana na maisha ukimpambania sababu hakuna anayekupongeza wala kukupa heko. Hii ni abuse kwa mtoto.

6. Wivu mtoto anapoingia mahusiano na mwanaume au mwanamke aliyependana nae. Nadhani hili tumelishuhudia sana. Mama kugombana na mkwewe sababu anaona atanyang'anywa kijana wake na attention itahama.

7. Kuharibu mahusiano ya mtoto ili kuweza kumcontrol mtoto na kuzuia influence ya mwanaume au mwanaume mwingine kwenye maisha yake.

8. Kujadili mada chafu za ngono, uasherati na zisizo na maadili mbele ya mtoto bila aibu wala tahadhari (hivi ni tahadhari au tahadhali)
Nmekuelewa sana mkuu
 
Nzuri

Sasa malizia ni mtu wa aina gani yuko more likely to practice hiyo covert incest, na njia ya kujitoa ili usimuelemee mtoto.
 
Ila hapa moja kwa moja single maza wanashtakiwa...
Basi atokee semaji la single maza hapa tusikae kinyonge😀
 
Nzuri

Sasa malizia ni mtu wa aina gani yuko more likely to practice hiyo covert incest, na njia ya kujitoa ili usimuelemee mtoto.
Wanawake ndio wanafanya sana hii kwa watoto wao both wa kike na wakiume. Wa kike ni ile unaona mama anamgeuza binti yake kuwa shost yake na kumfanya kama shoga yake badala ya kuwa mzazi kwa mtoto.

Au unakuta mwanamke analea mtoto wake wa kiume halafu anakuwa nae benet sana na kumpa majukumu kama baba wa familia ili aendelee kuwepo kuziba pengo la upweke alilo nalo.

So mwanamke ndie mtekelezaji mkuu wa huu unyanyasaji wa kisaikolojia.

Wanaume ni very rare kukuta wana hii tabia ingawa inawezekana mwanaume nae akafanya aina hii ya abuse but it's not common in Men.
 
Ila hapa moja kwa moja single maza wanashtakiwa...
Basi atokee semaji la single maza hapa tusikae kinyonge[emoji3]
Sio tu single mothers, anaweza kuwa bibi, shangazi, mama wa kambo, dada, hata baba.
 
sasa tungejuaje kama ni typing error? ungetumia lugha yetu wala usingepata shida ye kujitetea.
Mambo ya kisaikolojia ukiongea kiswahili unaonekana kama haupo serious lazima utie English ndipo uonekane upo serious.
 
Sio tu single mothers, anaweza kuwa bibi, shangazi, mama wa kambo, dada, hata baba.
Kwa ujumla katika makundi yote tajwa hapo, amini nakwambia asilimia kubwa ya wapandikiza chuki na mambo kama hayo ni masingo maza..
 
Ni kweli kabisa aisee ni changamoto kubwa sana hii
 
Dalili za mtu anayefanya "Covert Incest".

1. Kumtegemea mtoto akupe faraja, utulivu, na msaada wa kimawazo na hata kifedha muda mwingine.

2. Kuomba ushauri kwa mtoto ambao ni nje ya rika, umri na uwezo wake wa kudadavua mambo. Mfano unamhadithia mtoto madhira ya mume au bwana wako ili kupunguza stress. Au changamoto za ndugu zako au marafiki zako.

3. Kuingilia faragha ya mtoto wako mfano kutaka kujua anadate na nani na kufuatilia mahusiano yake wakati ameshavuka miaka 18 au zaidi. Unamgeuza shost yako na kutaka akuhadhithie mambo yake as if ni shoga yako.

4. Kumchukulia mtoto kama replacement ya mwenza. Mfano masingle mother husema huyu mtoto ndio baba yangu, ndio mume wangu, yeye ndie kila kitu changu. Sihitaji mwanaume. Unamtumia mtoto kama replacement ya mwanaume kiasi kwamba akija binti anataka kuanza nae mahusiano unamuona kama anakunyang'anya mume au partner wako wa maisha.

5. Kutarajia mtoto awe source ya inspiration na praising number one fan wako. Hii ipo sana kwa masingle mother pia kutaka mtoto ndie awe cheering fan wako, na kutaka asheherekee na kuwa proud na zile harakati zako za kupambana na maisha ukimpambania sababu hakuna anayekupongeza wala kukupa heko. Hii ni abuse kwa mtoto.

6. Wivu mtoto anapoingia mahusiano na mwanaume au mwanamke aliyependana nae. Nadhani hili tumelishuhudia sana. Mama kugombana na mkwewe sababu anaona atanyang'anywa kijana wake na attention itahama.

7. Kuharibu mahusiano ya mtoto ili kuweza kumcontrol mtoto na kuzuia influence ya mwanaume au mwanaume mwingine kwenye maisha yake.

8. Kujadili mada chafu za ngono, uasherati na zisizo na maadili mbele ya mtoto bila aibu wala tahadhari (hivi ni tahadhari au tahadhali)
Be right back
 
Back
Top Bottom