Naona BORA TUACHANE MAANA NAHISI NAKUBOA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naona BORA TUACHANE MAANA NAHISI NAKUBOA...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tugutuke, May 26, 2012.

 1. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Husika na kichwa cha habari hapo juu.
  Nina rafiki yangu wa kiume,mshikaji wangu sana anasema ana demu ila hamuelewi elewi. Story kwa kifupi iko hivi.. Demu anafanya kazi yake kwenye maeneo ambayo yanawahusisha sana wanaume yaani Restaurant & Bar. Sasa mshikaji anadai wanapendana na huyo demu ila demu ana mambo mengi ambayo huyu jamaa hayakai sawa kwake. Mfano,demu akiwa job kwake mara ashikwe shikwe,mara apewe ofa za kunywa bia akinunuliwa na wateja wake,anatongozwa mara kwa mara. Sasa jamaa anasema kila akijaribu kumuelimisha demu wake namna ya kuwa mstaarabu anaambulia majibu haya toka kwa demu wake "sikia,hapa nipo kazini unajua,na mimi ni mwanamke natakiwa niongee na watu vizuri ili nifanye kazi yangu vizuri. Hata nikitongozwa we usiwe na noma coz siwezi kuwakubalia wote na niko kazini,na please ukiona napewa ofa na wanaume wenzio usilete mambo ya wivu hapa,naomba utulie! Sawa? Au bora tuachane maana nahisi nakuboa sana japo nakupenda".
  Sasa huyu bro anasema kauli hiyo ilimboa sana,zaidi ni pale kila mara demu anapomwomba aachane naye kwa kisingizio cha kuwa anahisi anamboa bwana'ke. Sasa je,hapa kuna mapenzi ya dhati kweli? Na huyu bro afanyeje ili kukabili hali hiyo,na kwani demu hawezi kujiheshimu na kazi ikaendelea kama kawa yaani wateja wakaja vile vile? Ushauri na maoni yenu wadau ni muhimu sana. Jamaa atapita hapa ntamwonesha kilichojiri na ili afanya maamuzi ya busara.
  Kwenu wadau.
   
 2. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kama uwezo anao na anampenda amuweke nyumbani amlipe mshahara sidhani Kama atakua analipwa zaidi ya laki kwa mwezi.na asisahau kua kunguru hafugiki......
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hili ni tatizo lingine la kulelewa...nahisi donation kubwa ya bugdet pale home inaletwa na dem..let her do her job!! AAche wivu bana!!
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Lol! Akamsemelezee kwa mamake. Kuuza bar tu ndo hadi ashikwe? Mbona @Aspirin anatoaga ofa za bia bila kushika shika?
   
 5. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  SINZIGA,ninavokwambia huyu jamaa naishi naye nyumba moja it means tumepanga kila mtu geto lake! Speaking of donation.. Sidhani,na naambiwa kuwa hata huyu jamaa akienda pale kunywa bia analipia hata chakula analipia. Hataki kubebwa bebwa na demu. Anamushemu naona,[sio kwamba namtetea,ni kwa mjibu wake]
   
 6. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  apo chachaaa! Unadhani nini tatizo? king'AST
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. D

  Dotowangu JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  huyo jamaa ako naona kazi ya kusokota mpini haimudu vizuri ndo maana anadharaulika...mwambie ajifunze sio kila kitu tunazaliwa tunajua...
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Tobaaaa!Unekwisha wewe!
   
 9. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hapo siwezi kumsemea aisee! Ila je ndo sababu kubwa?
   
 10. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Wanawake wengi wanaofanya kazi katika maeneo hayo wapo hivyo,huyo friend wako anatakiwa achague moja kati ya kuizoea hiyo tabia au kutafuta ustaarabu mwingine,unless otherwise asitegemee huyo mwanamke atabadilika cause ndo tabia yao..
   
 11. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mshauri jamaa ako amtafutie huyo demu kazi
  tofauti na kuuza bar, kwani nijuavyo mimi kwa mazingira ya bar ......mh..
  ni chakula ya watu....
   
 12. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  sawa kabisa,kula like yangu mkuu
   
 13. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  kazi ndo inamruhusu kufanya hayo kwa sababu walevi wakishapata moja moto akili inaruka na yeye pale ndipo anapata pa kuchuna,sasa kama kakangu we hupendi hiyo tabia mara mia utafute mahali pengine pa kushika coz umemkuta anafanya hiyo kazi na ameshaizoea umemwelimisha hasikii wa mbili havai moja siku zote zaidi sana unatafuta maradhi,think twice fanya maamuzi ya busara wanawake ni wengi.
   
 14. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Maelezo ya dada yalikua sahihi kosa tu ni kusema bora tuachane! Mwambie mshikaji wako aanze kutafuta replacemnt kabla aache kabla hajaachwa kwa majonzi makubwa! Huyo anapenda vya pembeni atamsumbua sana.
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Sasa huyo jamaa yako anategemea gari la kibuku liwe na harufu ya chungwa?
   
 16. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  :smash: :smash: :smash:
   
 17. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  bila watu kama nyinyi,cjui tungekuwa tunacheka saa ngapi! Duh!
   
 18. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  ukipenda boga.......
   
 19. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  ila mademu siku hizi hata apewe nini, kama ni maharage ya mbeya, ni ya mbeya tu! wanagongwa sana kha!
   
 20. Tugutuke

  Tugutuke JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  true! So tumshaurije sasa.
   
Loading...