Nyamuleha jr
Senior Member
- Feb 20, 2013
- 185
- 65
Nimemaliza digri 2013 Baada ya kukaa dar mda mrefu kusaka ajira bila mafanikio nimeamua kurudi home, nimewakuta wale tulio soma nao lasaba wametoka kimaisha wamejenga, wanauhakika wa maisha tofauti na mimi ambaye sinahata ela ya vocha, nimekuta watu wamejiingiza sana kwenye biashara ndogo ndogo mbao, ufugaji wakuku, mwezi sasa umekatika watu wananishauri jiingize kwenye hizi biashara ndogo sasa naona noma kweli inshu ambazo ningefanya nikiwa la saba sasa nizifanye nikiwa nimemaliza chuo kikuu, kwanza nahisi nitawakatisha hawa madogo tamaa ya kusoma, nikama nilisha kuwa juu sasa nimerudishwa chini kwenye matope kabisa. Hapa naona bora niende mbali ambapo sijulikani nikafanye izo inshu, au nifanyaje?