We binti, acha kupoteza muda wako. Huyo jamaa anaonekana ana shida sana. Kijana wa umri huo kutokuwa na msimamo, kwa kweli ni shida. Anakutamkia ndoa sababu anajua we una shida ya kutamkiwa hivyo. Kweli kwa umri wako unapoteza muda kugombea mwanaume wa mtu? Akikuzoea atakumwaga na atarudi alipotoka. Wanaume akili zao... hiyo inayomfanya amponde kwako, afanye kila njia ubaki kwake ni tamaa. Siku utakuja. Atakuweka kipaumbele hadi utajiona malkia. Lakini ile curiosity ikiisha, atakucompare wewe na yule. Akifanya hivyo ndio ujiulize bond yako wewe na yule ipi ni kubwa? Je kama alikuja akamponda yeye kwako atashindwa nini kurudi kukuponda? Nenda katengeneze maisha yako. Hayo unayoyawahi hayana faida yoyote kwako. Ndoa zipo. Kama iliandikwa ni yako hata iweje itakuwa hivyo. Ila kama si yako jisumbue na kupoteza muda wako.