Naombeni ushauri wakubwa zangu

Cindy123

New Member
May 28, 2021
2
5
Mimi ni binti wa miaka 23 sasa. Nimekuwa kwenye mahusiano na kijana wa miaka 32. Mahusiano yetu ni ya mbali.

Yeye yupo Dar ila mimi nipo mkoa wa mbali sana ambapo kukutatana kwetu ni pale tu inapotokea likizo toka chuo kurudi nyumbani. Hapo tunaweza kuonana.

Tumeanza mahusiano huu ni mwaka wa tatu. Mahusiano yetu yalikuwa kwenye simu, kupigiana na kutext. Kiukweli mwenzangu ana tabia nyingi mbaya ambazo nimezigundua ingawa simjui vema. Nakumbuka nikiwa mwaka wa kwanza kipindi cha likizo fupi, niliwahi safiri na kwenda kwa mwenzangu. Amepanga gheto, na anafanya kazi.

Hofu yangu ni hii. Mwanzo nilimpenda na kumuamini sana. Ingawa mwenzangu anapenda sana starehe na anafanya akidai kuwa sababu mimi nipo mbali naye. Jambo ambalo kidogo sasa linanipa mashaka kama ni kweli ataweza badilika ama hapa najifanganya. Maana kiukweli mimi sipendi kabisa lifestyle yake. Hawezi hata kunitumia pesa ya matumizi hadi tugombane. Na pesa kubwa anayotuma ni 15000 hiyo ni kubwa sana.

Jambo la pili na kubwa linalonitia mashaka ni kwamba nimegundua kuwa mara kadhaa amekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda mrefu sana. Miaka 9. Wanaachana na kurudiana. Na kuachana kwao hakufiki mwezi. Wapo mkoa mmoja. Na huyo mwanamke wana umri sawa ingawa mwenzangu amemzidi kidogo.

Mwanzo mwenzangu alikataa. Lakini baada ya kupata ushahidi, aliweka wazi na kuomba msamaha. Lakini amekuwa mara kwa mara akirudia kosa hilo. Kila mara nagundua kwa ushahidi kuwa wamerudiana. Jambo ambalo mimi linanikwaza sana.

Hiki kitu kimenifanya niwe addicted kumfuatilia yule mwanamke anafanya nini, yuko wapi na nani. Yaan sina raha hata kidogo. Najikuta badala ya kuongelea future mara nyingi namuongelea huyu mwanamke.

Kijana huyu ameapa kuwa ananipenda na amenichagua mimi ila yule mwanamke anamnganda. Lakini najiuliza kama kweli angekuwa anagandwa, ina maana yeye hana uwezo wa kujicontrol juu ya mwanamke huyo? Tena mbaya zaidi ni mwanamke ambaye wamesaidiana sana kabla ya mwenzangu kupata kazi. Hadi sasa hata ikitokea shida yoyote wataongea na kusolve.

Kwenye starehe mara kwa mara nashuhudia picha wakiwa wamepiga wanafurahi pamoja. Mwenzangu nikimuuliza ananiambia anajilazimisha tu hapo. Na amenitamkia ndoa.

Sielewi jamani. Ni kweli hapa ni pa kukaa? Na kama kuna ndoa inawezekana huyu mwanaume anafanya haya kwa kuwa mimi nipo mbali au ni tamaa zake tu? Mwaka huu namaliza elimu yangu na ninategemea kuwa karibu na kijana huyu kuanza mahusiano ya karibu. Naombeni mnisaidie kwa ushauri ndugu yenu. Kama ninaangamia ama la.
Shukrani.
 
Samahani. Una maanisha nini unaposema ananihitaji? Je yeye hana upendo nami?
Naam, anakuh
Samahani. Una maanisha nini unaposema ananihitaji? Je yeye hana upendo nami?
naam, anakuhitaji kwa sababu umekuwa tulizo la kero au mambo fulani anayokosa kule. Anakuhitaji uzibe pengo. Pili, mwenye upendo huacha yote/wote awe na wewe. Hajafanya hivo ila wewe uko radhi kuacha wote kwa ajili yake.
 
Kwanza njoo pm kijana wa kike nikupe mapenzi yenyewe maana inaonekana umri wako ni mdogo naaa jamaa hakupendi,,, ujue sis wanaume tutabaki kuwa wanaumetu hata atokee papa wa kike,,


Kiiufupi haupendwi hapo ilatu anakudanganya huyo.

Af mistake nyingne mbna kakuzid mbali kiumri hvyo! Au umefata pensheni kwake bibie!!?

Lastly, don bother about him, proceed wth yr own matters. Hakuna ndoa hapo wala mapenzi, utaishia kutesekatuuuuu
 
Mwanaume anaweza kuwa na wanawake 7 ila akawa anampenda mmoja tu,wewe tulia mshindi atatangazwa kanisani au msikitini..kama yuko na huyo mwanamke kwa miaka 9 basi siyo chaguo lake ila ni tamaa tu so zali lipo kwako sikilizia tu utammiliki
 
Hawezi hata kunitumia pesa ya matumizi hadi tugombane. Na pesa kubwa anayotuma ni 15000 hiyo ni kubwa sana.kuna dalili huonekana mapema kabisa ila upofu wa mapenzi hututia giza..!

Pili hao watu kuachana ni ndoto wana concrete background, usijipe stress mapema hivyo anza kujinasua taratibu
 
We binti, acha kupoteza muda wako. Huyo jamaa anaonekana ana shida sana. Kijana wa umri huo kutokuwa na msimamo, kwa kweli ni shida. Anakutamkia ndoa sababu anajua we una shida ya kutamkiwa hivyo. Kweli kwa umri wako unapoteza muda kugombea mwanaume wa mtu?

Akikuzoea atakumwaga na atarudi alipotoka. Wanaume akili zao... hiyo inayomfanya amponde kwako, afanye kila njia ubaki kwake ni tamaa. Siku utakuja. Atakuweka kipaumbele hadi utajiona malkia. Lakini ile curiosity ikiisha, atakucompare wewe na yule.

Akifanya hivyo ndio ujiulize bond yako wewe na yule ipi ni kubwa? Je kama alikuja akamponda yeye kwako atashindwa nini kurudi kukuponda? Nenda katengeneze maisha yako. Hayo unayoyawahi hayana faida yoyote kwako. Ndoa zipo. Kama iliandikwa ni yako hata iweje itakuwa hivyo. Ila kama si yako jisumbue na kupoteza muda wako.
 
Akufukuzaye hakwambii toka utaona matendo, na usisubir mpaka utupiwe nguo nje jiongezee,

Tulipewa akili kuchanganua zuri na baya, hivyo tumia akili usiongezwe na hisia za ngono,

Maamuzi utafanya wewe lakini hapo huna chako.
We binti, acha kupoteza muda wako. Huyo jamaa anaonekana ana shida sana. Kijana wa umri huo kutokuwa na msimamo, kwa kweli ni shida. Anakutamkia ndoa sababu anajua we una shida ya kutamkiwa hivyo. Kweli kwa umri wako unapoteza muda kugombea mwanaume wa mtu? Akikuzoea atakumwaga na atarudi alipotoka. Wanaume akili zao... hiyo inayomfanya amponde kwako, afanye kila njia ubaki kwake ni tamaa. Siku utakuja. Atakuweka kipaumbele hadi utajiona malkia. Lakini ile curiosity ikiisha, atakucompare wewe na yule. Akifanya hivyo ndio ujiulize bond yako wewe na yule ipi ni kubwa? Je kama alikuja akamponda yeye kwako atashindwa nini kurudi kukuponda? Nenda katengeneze maisha yako. Hayo unayoyawahi hayana faida yoyote kwako. Ndoa zipo. Kama iliandikwa ni yako hata iweje itakuwa hivyo. Ila kama si yako jisumbue na kupoteza muda wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom