Naombeni ushauri wa jinsi ya kumfikishia ujumbe Mke Wangu bila kuumiza moyo wake

Siku ambazo unashinda nyumbani mjengee mazingira ya kuoga nae hata mara tatu au nne kea siku, hakikisha kila mnapooga mnabadilisha nguo. Mnunulie body spray,perfumes, lotions na simple makeups na kila anapopaka muonyeshe kufurahia na kumsifia, msisitize kusuka nywele zake na kuzweka katika hali ya usafi kila mara,sio lazima asuke za gharama kubwa, hata twenfe kikioni zikiwa safi zinavutia. gharamia vitu vidogo vidogo vitakavyomfanya abadilike, toka nae sehemu mbali mbali ajionee wanawak wengine wanavyojijali nae atatamani

Msigie kila anapokua msafi, Mfano akioga vizuri akipaka perfume mwambie amependeza na unavutiwa na harufu yake na unatamani ukae karibu nae wakati wote kwa jinsi anavyinukia, ukifanya hivyo lazima atajua kwamba unapenda awe msafi n aanukie vizuri nae atabadilika

To note
Ni ngumu sana kumfundisha mke usafi maana wanawake asili yetu ni usafi sasa huyo ambae hajali hata mwili wake unahitaji saikolojia ya hali ya juu ila uwe na subira atabadilika tu

Nina ndoa changa inayokaribia mwaka, nampenda sana mke wangu kiasi cha kutowaza kuachana ila tatizo ni suala la usafi wake ndio linalonikosesha amani na nimeshajitahidi kumrekebisha ila habadiliki.

Tangu nimemuoa yupo vizuri sana kwenye suala zima la usafi wa mazingira ya nyumba. Akiamka atafanya usafi wa nyumba nzima,atafagia,atapiga deki kila kona,atajaza maji,atapika nk. Kuhusu mambo ya usafi kwa ujumla yuko vizuri maana hata kufua huwa anafua Mara mbili kwa wiki na akianza kufua huwa habakishi hata leso chafu ndani mpaka wakati mwingine huwa namuomba apumzike hizo kazi zake.

Tatizo alilonalo ni kuhusu usafi wa mwili wake,yaani hajali kabisa kuhusu mwili wake utadhani atautumia peke yake. Sio ajabu kwake kuamka asubuhi akafanya pilika zake mpaka jioni bila kupiga mswaki na wala hajali kwamba kinywa chake kinatoa harufu. Anaweza kuingia bafuni kuoga akatoka bila kupiga mswaki na wala asijali.

Amekuwa akitoa harufu sana mdomoni kiasi cha kunikosesha raha hata kwenye tendo la ndoa na Mara nyingi huwa namchukua wote kwenda bafuni tupige mswaki pamoja huku namtania na kucheka japo inaniuma. Pamoja na mazoea yote ninayomfanyia ya kwenda nae kupiga mswaki asubuhi na kabla hatujalala bado hajazoea kabisa na nikisema nikaushe basi hatopiga mswaki siku hiyo.

Hapo sijaongelea uvivu wake wa kuoga kiasi kwamba akioga asubuhi basi hataki kuoga tena mpaka asubuhi unayofuata,yaani suala la kuoga Mara ya pili huwa linaleta ugomvi sana maana nikimlazimisha sana huwa ananuna na mtalala hamuongei siku hiyo huku akidai kuwa baridi ni kali hivyo hataki kuoga tena.

Kinywa chake kinatoa harufu mpaka nikahisi labda dawa za meno hazimsaidii nikawa namnunulia mouth washer afanye kusukutua mdomoni lakini alitumia Mara chache tu anadai zinamuumiza mdomo na akazitupa na kila nikinunua mpya haikai ndani anaficha wapi sijui.

Roho inaniuma Sana maana naweza nikatoka kazini nikiwa na mahaba full charge lakini akinisogelea tu ili tuongee kimahaba basi harufu inaniharibu akili yangu na kujikuta sitamani tena romance. Nikipiga nae mswaki anajisugua meno kidogo ananawa madai kamaliza,ukimuambia jisugue na ulimi hataki na atanuna usiku mzima.

Nakosa Raha ya mapenzi na mpaka nimeanza kuchepuka japo nampenda sana. Jinsi ya kumwambia live siwezi lakini kila njia ninayotumia kumrekebisha inagonga ukuta maana waweza ukamnunulia mswaki mpya ukaukuta bafuni hata wiki nzima hajaufungua kuutumia wakati mswaki anaoutumia ushachakaa.

Najiuliza Ni Nani nikamuambie tatizo lake sipati jibu na yeye ni mtu ambaye ukimshitakia hata kwa mama ake basi atalia wiki nzima mpaka nyumba naiona chungu. Nishaurini wanajamii maana nimedumu nae muda mrefu kwenye uchumba sikuwahi kuijua tabia yake hii,Leo hii nimemuoa ndo ananipa mateso haya.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Siku ambazo unashinda nyumbani mjengee mazingira ya kuoga nae hata mara tatu au nne kea siku, hakikisha kila mnapooga mnabadilisha nguo. Mnunulie body spray,perfumes, lotions na simple makeups na kila anapopaka muonyeshe kufurahia na kumsifia, msisitize kusuka nywele zake na kuzweka katika hali ya usafi kila mara,sio lazima asuke za gharama kubwa, hata twenfe kikioni zikiwa safi zinavutia. gharamia vitu vidogo vidogo vitakavyomfanya abadilike, toka nae sehemu mbali mbali ajionee wanawak wengine wanavyojijali nae atatamani

Msigie kila anapokua msafi, Mfano akioga vizuri akipaka perfume mwambie amependeza na unavutiwa na harufu yake na unatamani ukae karibu nae wakati wote kwa jinsi anavyinukia, ukifanya hivyo lazima atajua kwamba unapenda awe msafi n aanukie vizuri nae atabadilika

To note
Ni ngumu sana kumfundisha mke usafi maana wanawake asili yetu ni usafi sasa huyo ambae hajali hata mwili wake unahitaji saikolojia ya hali ya juu ila uwe na subira atabadilika tu
Umeniambia kitu kikubwa sana, Asante

👏👏
 
Mkiambiwa mkae nao ndani kabla ya kuji commit hamtaki! Mnaleta ulokole haya sasa pambana na hali yako. Demu hakaguliwi kwa kuja kulala kwako weekend na kuodoka au kukutana lodge tu.

Mteke, ishi nae ndani kwa miezi kadhaa kabla hujamuoa (Volunteer Program). It works kama demu anajitegemea mshawishi ukae nae sehemu moja utamjua madhaifu yake yote kabla hata hujalipa mahali.

Wanawake wa sikuhizi ni hovyo sana hasa hawa wa 2000's

Ulokole unawaponza wengi sana.! Na mimi nishasema sioi mwanamke bila kumfanyia yafuatayo;
1. Kumpiga mashine nijue kitumbua chake kikoje, kitamua au ndio kuogelea Bwawani mtera.
2. Kukaa naye ghetto hata isipokuwa muda mrefu ila nitakuwa namtaka aje ghetto nara kwa mara nione usafi wake n uwajibikaji wake kwenye majukumu yake kama Mama wa familia.
3. Ni lazima nijaribu kumjaribu kuonesha kama kumcheat nione anamtuzamo gani..! Kama ni wale wa kufanya maamuzi kwa kusikia bila kuona basi huyo hanifai.
4. Lazima nione mtizamo wake juu ya masuala ya kijinsia, yeye kama atakuwa na zile akili za ufemenist ule wa kusema hawezi nipikia au kunifulia nguooo basi huyo kwaheri
 
Siku ambazo unashinda nyumbani mjengee mazingira ya kuoga nae hata mara tatu au nne kea siku, hakikisha kila mnapooga mnabadilisha nguo. Mnunulie body spray,perfumes, lotions na simple makeups na kila anapopaka muonyeshe kufurahia na kumsifia, msisitize kusuka nywele zake na kuzweka katika hali ya usafi kila mara,sio lazima asuke za gharama kubwa, hata twenfe kikioni zikiwa safi zinavutia. gharamia vitu vidogo vidogo vitakavyomfanya abadilike, toka nae sehemu mbali mbali ajionee wanawak wengine wanavyojijali nae atatamani

Msigie kila anapokua msafi, Mfano akioga vizuri akipaka perfume mwambie amependeza na unavutiwa na harufu yake na unatamani ukae karibu nae wakati wote kwa jinsi anavyinukia, ukifanya hivyo lazima atajua kwamba unapenda awe msafi n aanukie vizuri nae atabadilika

To note
Ni ngumu sana kumfundisha mke usafi maana wanawake asili yetu ni usafi sasa huyo ambae hajali hata mwili wake unahitaji saikolojia ya hali ya juu ila uwe na subira atabadilika tu
Ameeleza yote
 
Nnachoshindwa kuelewa kaka kwenye uchumba ilikuaje? mana the way umeandika ni kama vile ulitafutiwa na hukupata nafasi ya kumjua then mkakutana kanisanai yeye ndani ya shela na wewe ndani ya suti mkafunga ndoa. Hayo uliyoyaandika ni marahisi sana kuyagundua kipindi cha urafiki mpaka kufikia uchumba esp. swala la kunuka mdomo na uvivu wa kuoga.
 
Kuna kitu kama kinaniambia hata kutawadha mkeo pia huwa hatawadhi...
 
Mwambie ukweli mkuu,

Ni kweli ukweli unauma a unajenga sana kwa atakayeuzingatia
Huna haja ya kumficha huyo ni mkeo
Let her know the truth kua anakukera anaposhindwa kua msafi,
 
Back
Top Bottom