Naombeni ushauri wa jinsi ya kumfikishia ujumbe Mke Wangu bila kuumiza moyo wake

Mkiambiwa mkae nao ndani kabla ya kuji commit hamtaki! Mnaleta ulokole haya sasa pambana na hali yako. Demu hakaguliwi kwa kuja kulala kwako weekend na kuodoka au kukutana lodge tu.

Mteke, ishi nae ndani kwa miezi kadhaa kabla hujamuoa (Volunteer Program). It works kama demu anajitegemea mshawishi ukae nae sehemu moja utamjua madhaifu yake yote kabla hata hujalipa mahali.

Wanawake wa sikuhizi ni hovyo sana hasa hawa wa 2000's
Huu ni uhuni. Kwahiyo ukiona hakufai unamwacha unadandia mwingine, sivyo? Utadandia wangapi? Na uliyemwoa alishadandiwa na wangapi? Ungependa kuoa volunteer sugu? Kwa mpango huu wa kwako utasabaisha kuwepo wanawake wachakavu wengi ambao kila mtu anajaribia zana hapo kwake, na wanaume wachakavu ambao wameshachovya kila mahali. Ndipo mnapata ndoa zilizokwisha kuchakaa tangu hata hazijaanza. Mitumba sugu. Hii kamwe siyo sifa njema.
 
Siku mtoe Out au tengeneza mazingira mazuri ya ww na yeye tu.

Then mwambie tucheze mchezo, alaf anza ww kumwambia , leo unaomba akuambie kitu kimoja tu anachopenda toka kwako na kimoja ambacho hapendi.

Sasa ikija zamu yako, ndio useme hiko chake na jinsi gan hukipendi na kukukosesha Mahaba.

Atanuna ila niamini atabadilika sana na hii inasaidia sana.

Huwez acha mke kisa kunuka mdogo mzee,
Midomo yote ikinuka kuna suluhisho
 
Mkiambiwa mkae nao ndani kabla ya kuji commit hamtaki! Mnaleta ulokole haya sasa pambana na hali yako. Demu hakaguliwi kwa kuja kulala kwako weekend na kuodoka au kukutana lodge tu.

Mteke, ishi nae ndani kwa miezi kadhaa kabla hujamuoa (Volunteer Program). It works kama demu anajitegemea mshawishi ukae nae sehemu moja utamjua madhaifu yake yote kabla hata hujalipa mahali.

Wanawake wa sikuhizi ni hovyo sana hasa hawa wa 2000's

Hata ukikaa nae na ukajua hili,
Utamuacha?.

Ni kitu kidogo kinachoweza kurekebishika.

Ni namna ya kumwambia jinsi gan kinakera.
Iwe umekaa nae ndan au umeoa bila kukaa nae ndan.
Ni kitu kidogo sana kurekebisha hiki.
 
Nina ndoa changa inayokaribia mwaka, nampenda sana mke wangu kiasi cha kutowaza kuachana ila tatizo ni suala la usafi wake ndio linalonikosesha amani na nimeshajitahidi kumrekebisha ila habadiliki.

Tangu nimemuoa yupo vizuri sana kwenye suala zima la usafi wa mazingira ya nyumba. Akiamka atafanya usafi wa nyumba nzima,atafagia,atapiga deki kila kona,atajaza maji,atapika nk. Kuhusu mambo ya usafi kwa ujumla yuko vizuri maana hata kufua huwa anafua Mara mbili kwa wiki na akianza kufua huwa habakishi hata leso chafu ndani mpaka wakati mwingine huwa namuomba apumzike hizo kazi zake.

Tatizo alilonalo ni kuhusu usafi wa mwili wake,yaani hajali kabisa kuhusu mwili wake utadhani atautumia peke yake. Sio ajabu kwake kuamka asubuhi akafanya pilika zake mpaka jioni bila kupiga mswaki na wala hajali kwamba kinywa chake kinatoa harufu. Anaweza kuingia bafuni kuoga akatoka bila kupiga mswaki na wala asijali.

Amekuwa akitoa harufu sana mdomoni kiasi cha kunikosesha raha hata kwenye tendo la ndoa na Mara nyingi huwa namchukua wote kwenda bafuni tupige mswaki pamoja huku namtania na kucheka japo inaniuma. Pamoja na mazoea yote ninayomfanyia ya kwenda nae kupiga mswaki asubuhi na kabla hatujalala bado hajazoea kabisa na nikisema nikaushe basi hatopiga mswaki siku hiyo.

Hapo sijaongelea uvivu wake wa kuoga kiasi kwamba akioga asubuhi basi hataki kuoga tena mpaka asubuhi unayofuata,yaani suala la kuoga Mara ya pili huwa linaleta ugomvi sana maana nikimlazimisha sana huwa ananuna na mtalala hamuongei siku hiyo huku akidai kuwa baridi ni kali hivyo hataki kuoga tena.

Kinywa chake kinatoa harufu mpaka nikahisi labda dawa za meno hazimsaidii nikawa namnunulia mouth washer afanye kusukutua mdomoni lakini alitumia Mara chache tu anadai zinamuumiza mdomo na akazitupa na kila nikinunua mpya haikai ndani anaficha wapi sijui.

Roho inaniuma Sana maana naweza nikatoka kazini nikiwa na mahaba full charge lakini akinisogelea tu ili tuongee kimahaba basi harufu inaniharibu akili yangu na kujikuta sitamani tena romance. Nikipiga nae mswaki anajisugua meno kidogo ananawa madai kamaliza,ukimuambia jisugue na ulimi hataki na atanuna usiku mzima.

Nakosa Raha ya mapenzi na mpaka nimeanza kuchepuka japo nampenda sana. Jinsi ya kumwambia live siwezi lakini kila njia ninayotumia kumrekebisha inagonga ukuta maana waweza ukamnunulia mswaki mpya ukaukuta bafuni hata wiki nzima hajaufungua kuutumia wakati mswaki anaoutumia ushachakaa.

Najiuliza Ni Nani nikamuambie tatizo lake sipati jibu na yeye ni mtu ambaye ukimshitakia hata kwa mama ake basi atalia wiki nzima mpaka nyumba naiona chungu. Nishaurini wanajamii maana nimedumu nae muda mrefu kwenye uchumba sikuwahi kuijua tabia yake hii,Leo hii nimemuoa ndo ananipa mateso haya.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Huyoooo ni chaguo lakoooooo
 
AhAhah naomba tu siku nyingine r usije sema kuwa baada ya mdomo kunuka sas Ni papuchi yakee inanukaa
 
Nitajitahidi Kwan hili maana kila nikiwaza jinsi ya kumwambia hivyo huwa nachoka,sitaki kumuumiza kihisia kabisa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Yes! Mwambie ukweli maana hakuna atakayemwambia ukweli zaidi yako. Na ukiendelea kuchepuka siku akigundua atakuja kukulaumu kuwa umepungukiwa nini kwake?

Mwambie ukweli hata kama atachukia utamwambia kuwa ni wajibu wako kumrekebisha uonapo mapungufu kwake
 
Mkuu mpeleke kwa Dentist!Huyo Dentist mpange na umwambie kero kuhusu mkeo halafu umpeleke!!HUYO DENTIST UMLISHE MANENO KUWA UKIFIKA NA MKEO KWA AJILI YA UCHUNGUZI BAADA YA UCHUNGUZI AMWAMBIE KUWA YUPO MBIONI KUOZA MENO YOTE HIVYO AMPE RATIBA YA KUPIGA MSWAKI KUTWA MARA TATU KWA MWAKA MMOJA BILA KUACHA!!!AKIFUATA MAELEKEZO HAYO ATAZOEA NA HATOACHA KUPIGA MSWAKI TENA!!!
 
Ulipozingua ni hapo uliposema umeanza kuchepuka. Eti mtu unampenda halafu unachepuka kwa sababu ya mswaki tu? Huyo uliyechepuka naye anapiga mswaki wa malaika? Nikwambie usichokijua, na hii ni kwa uzoefu nina ndoa ya miaka 24. Mke wa mwenzio siku zote hana kasoro, lakini wa kwako kasoro utaiona tena kubwa sana. Na sababu ni rahisi tu, ni issue ya time and distance. Kadri kitu kinavyozidi kuwa karibu yako (distance) na unavyokaa nacho muda mrefu (time) ndivyo unavyogundua details nyingi, na watu hutumia details kufanya judgement. The fewer the details, the softer the judgement.
Mkeo umekaa nae karibu ndipo ukaona hiyo issue ya kunuka mdomo, si ajabu wengine walio mbali naye hawajaiona hiyo ndio maana hata wewe hukuiona wakati wa uchumba! Na ana mengine mazuri yanayoonekana kwa mbali, na kwa hayo wengine wanamtamani kama wewe ulivyomtamani ukamchumbia na kumuoa. Na huyo uliyechepuka naye ukipata naye muda na ukaribu wa kutosha utagundua kasoro zake pia. Na wewe una kasoro zako mkeo anazivumilia. Kwa hakika hiyo habari ya kunuka mdomo siyo justification ya kuchepuka, kamwe siyo.
Kaa na mwenzio, anzisheni mada za kuboresha uhusiano wenu. Anzeni kujadili kwanza yale yanayowafurahisha, mwambie mwenzio mambo unayofurahia kwake, apate morale ya kuendelea nayo kwa ufanisi zaidi. Naye akuambie ya kwako. Kisha mzungumze ya kuboresha, na siyo yote kwa siku moja, kama ni mengi yanakatisha tamaa. Orodhesha yote kichwani mwako halafu anza na yale mepesi, usilete yote, leta moja tu, jepesi ili liwe rahisi kutekelezwa, na likisharekebika toa pongezi na onesha tofauti, mwenzio atafurahi. Kisha baada ya muda ibua jingine, na kadri linavyofanyiwa kazi uwe unapongeza kila hatua. Naye mpe nafasi hiyohiyo ya kukurekebisha, fanyeni hivyo mtafurahia maisha.
Na usidhani kuwa mambo ya kurekebishana yataisha. Sisi tuna miaka 24 na bado tunayo ya kurekebishana, na tunafurahia kila tunapofanikiwa kurekebisha jambo moja. Kumbuka nyote ni wanadamu siyo mawe, kwa hiyo hamtabakia static. Mtarekebishana mambo fulani, lakini kwa kuwa bado mnakua na mazingira yanawabadilikia kila siku, yataibuka mambo mapya, changamoto mpya, nazo zinaweza kuleta tabia mpya kwa pande zote mbili, ambazo tabia hizo bado zitahitaji kusemewa na kurekebishwa. Usidhani ukifanikiwa kumpigisha mswaki ndio umemaliza ya kurekebisha, yatakuja mengine. Utamaliza aliyotoka nayo kwa wazazi wake, yatakuja mengine atakayopatia kwako hapo. Nawe vivyohivyo.
Zingatia: 1. kuchepuka siyo suluhisho, huyo mchepuko ukija kumjua kwa undani utagundua naye siyo kamili. 2. Rekebishaneni kwa upendo na kwa nia ya kudumisha ndoa yenu.
Asante sana mkuu, umeongea mengi yenye hekima hata mm nmejifunza kitu.. Asante sana kaka.
 
Nina ndoa changa inayokaribia mwaka, nampenda sana mke wangu kiasi cha kutowaza kuachana ila tatizo ni suala la usafi wake ndio linalonikosesha amani na nimeshajitahidi kumrekebisha ila habadiliki.

Tangu nimemuoa yupo vizuri sana kwenye suala zima la usafi wa mazingira ya nyumba. Akiamka atafanya usafi wa nyumba nzima,atafagia,atapiga deki kila kona,atajaza maji,atapika nk. Kuhusu mambo ya usafi kwa ujumla yuko vizuri maana hata kufua huwa anafua Mara mbili kwa wiki na akianza kufua huwa habakishi hata leso chafu ndani mpaka wakati mwingine huwa namuomba apumzike hizo kazi zake.

Tatizo alilonalo ni kuhusu usafi wa mwili wake,yaani hajali kabisa kuhusu mwili wake utadhani atautumia peke yake. Sio ajabu kwake kuamka asubuhi akafanya pilika zake mpaka jioni bila kupiga mswaki na wala hajali kwamba kinywa chake kinatoa harufu. Anaweza kuingia bafuni kuoga akatoka bila kupiga mswaki na wala asijali.

Amekuwa akitoa harufu sana mdomoni kiasi cha kunikosesha raha hata kwenye tendo la ndoa na Mara nyingi huwa namchukua wote kwenda bafuni tupige mswaki pamoja huku namtania na kucheka japo inaniuma. Pamoja na mazoea yote ninayomfanyia ya kwenda nae kupiga mswaki asubuhi na kabla hatujalala bado hajazoea kabisa na nikisema nikaushe basi hatopiga mswaki siku hiyo.

Hapo sijaongelea uvivu wake wa kuoga kiasi kwamba akioga asubuhi basi hataki kuoga tena mpaka asubuhi unayofuata,yaani suala la kuoga Mara ya pili huwa linaleta ugomvi sana maana nikimlazimisha sana huwa ananuna na mtalala hamuongei siku hiyo huku akidai kuwa baridi ni kali hivyo hataki kuoga tena.

Kinywa chake kinatoa harufu mpaka nikahisi labda dawa za meno hazimsaidii nikawa namnunulia mouth washer afanye kusukutua mdomoni lakini alitumia Mara chache tu anadai zinamuumiza mdomo na akazitupa na kila nikinunua mpya haikai ndani anaficha wapi sijui.

Roho inaniuma Sana maana naweza nikatoka kazini nikiwa na mahaba full charge lakini akinisogelea tu ili tuongee kimahaba basi harufu inaniharibu akili yangu na kujikuta sitamani tena romance. Nikipiga nae mswaki anajisugua meno kidogo ananawa madai kamaliza,ukimuambia jisugue na ulimi hataki na atanuna usiku mzima.

Nakosa Raha ya mapenzi na mpaka nimeanza kuchepuka japo nampenda sana. Jinsi ya kumwambia live siwezi lakini kila njia ninayotumia kumrekebisha inagonga ukuta maana waweza ukamnunulia mswaki mpya ukaukuta bafuni hata wiki nzima hajaufungua kuutumia wakati mswaki anaoutumia ushachakaa.

Najiuliza Ni Nani nikamuambie tatizo lake sipati jibu na yeye ni mtu ambaye ukimshitakia hata kwa mama ake basi atalia wiki nzima mpaka nyumba naiona chungu. Nishaurini wanajamii maana nimedumu nae muda mrefu kwenye uchumba sikuwahi kuijua tabia yake hii,Leo hii nimemuoa ndo ananipa mateso haya.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Chunga sana
IMG-20200628-WA0005.jpg
 
Nimeandika nikafuta ngoja wangine waje kukushauri.
Hawa ndo wababa wa familia tulionao kipindi hiki, aisee
 
Hata ukikaa nae na ukajua hili,
Utamuacha?.

Ni kitu kidogo kinachoweza kurekebishika.

Ni namna ya kumwambia jinsi gan kinakera.
Iwe umekaa nae ndan au umeoa bila kukaa nae ndan.
Ni kitu kidogo sana kurekebisha hiki.
Kama dogo uzi wa nini?
 
Huu ni uhuni. Kwahiyo ukiona hakufai unamwacha unadandia mwingine, sivyo? Utadandia wangapi? Na uliyemwoa alishadandiwa na wangapi? Ungependa kuoa volunteer sugu? Kwa mpango huu wa kwako utasabaisha kuwepo wanawake wachakavu wengi ambao kila mtu anajaribia zana hapo kwake, na wanaume wachakavu ambao wameshachovya kila mahali. Ndipo mnapata ndoa zilizokwisha kuchakaa tangu hata hazijaanza. Mitumba sugu. Hii kamwe siyo sifa njema.
Unaangalia unaloliweza kulivumilia unalibeba. Kama huwezi ni ngumu!
 
Back
Top Bottom