Naombeni ushauri: Rafiki yangu amehamia kwangu na mabegi

Mvumilie mkuu. Ila inabidi mpange utaratibu wa kuishi hapo ghetto. Mchangie matumizi kama kodi, chakula n.k

Huwezi kujua leo na kesho huyo mwamba anaweza akatoboa kabla yako na akawa msaada kwako. Mvumilie in the mean time akiji-sort.

Ila ukiona anakuwa mzigo kwako yani sio mtu wa kupambania kombe mda wote yupo tu na simu JF mara Insta au anakuletea wanawake ghetto fukuza au hama muache.

Otherwise mvumilie huwezi kujua maana majaribu kama hayo yaweza kuja na neema.
Asitegemee fadhila kwamba mwamba akitoboa basi anaweza kumpiga tafu baadae hilo sahau.. washkaji wengi ni masnich wkt wakiwa na shida vichwa vinakuwa chini akitoboa mabega yanakuwa juu na kusahau waliowasaidia....

Uamuzi ni wako akidha asepe au abaki.
 
Mtu unaweza muona rafiki yako kumbe siyo, anajua huna mishe lakini ataamka kanuna bila sababu
 
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema?Mimi kuishi na watu sidhani kama nitaweza, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana nashindwa kuwa huru kabisa natamani nimtoe hapa hata kesho asubuhi

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu
Umesema ni rafiki yako! Then nashauri ongea nae mueleze ukweli kwamba huna nafasi.
 
Maisha ni fumbo kubwa sana hakuna ajuaye kesho yake na kamww kwwnye maisha usimdharau mtu kila jambo hutokea kwa sababu ..... ngoja nikupe ushuhuda wangu wa kweli kipindi na kuja dar nlifikia kwa mshkaji wangu flani maeneo ya keko sikuwa na kazi inshort sikiwa na mbele wala nyuma mshkaji alinivumilia kwa mda kuna wakati tililala njaa ngoja ni fupishe maisha yaliendelea kibishi ... nikajaga kupata kazi mahali tangu sikuile mambo yakawa tofauti .... alikuja kufukuzwa kazi kodi nikawa na lipia mmi ....... nikaja kumunganisha kwwnye kampuni mjoa ya kichina Leo kila mtu ana maisha yake na tuna wasiliana ........ KATI YETU HAKUNA AJUAYE KESHO .....LEO UTA MKAZIA LAKINI KESHI NDO ATAKAYE KUSAIDIA ...
 
Kuna mawili .
1. Usimfukuze akae hata mwezi
2. Muulize mipango yake hadi lini atasepa au nini kinaendelea .
3. Muulize kuhusu huyo mjomba wake
4. Kwa maisha haya huwezi jinsia moja kuishi pamoja huna raha yaani .
5. Maisha yakutegemeana ni mbaya sana.
6. Nani mwenye ufunguo na ameenda wapi na ni either ni usiku au mchana, na hayupo karibu unapiga simu hadi unazima . Sipendagi ni kero sana
 
Usimfukuze, mshirikishe kwenye mishe za kutafuta hela ili mtafute wote. Siku atakapotengamaa kiuchumi atatafuta chumba chake. Hii ndio maana halisi ya UPENDO na MAISHA
 
Mkuu usikurupuke kumfukuza au hata kumwonesha vitendo vya wazi kuwa hupendi uwepo wake, jipe muda endelea na mishe zako tu kwani ye sio mtoto mdogo useme utamwachia nani.
 
Mhifadhi mwenzio ndiyo urafiki wenyewe. Kama una bangaiza, mbangaize pamoja, huwezi kujua nani ataanza kutoboa kwenye maisha. Be kind, kwakufanya hivyo, unajifungulia milango ya baraka. Hawa ndugu hawa ambao siyo wazazi wetu halisi waangalie hivyo hivyo wanatambuaga vijana kama hawa once wakifanikiwa, lakini hawapo tayari kuwa sehemu ya kufanikisha.

Mpe mwenzako support, share the little, sharing is caring.

Mungu awasaidie na kuwafungilia milango yake ya baraka
Mtoa post nafikiri ushauli huu unakufaa huwezi jua kesho yako au yake Mungu ni mwema kwa waja wake.
 
Pole umenikumbusha mbali.
Nilimkaribisha rafiki yangu kwangu,aliomba akae wiki mbili tu ila alikaa zaidi ya miezi mitatu.
Changamoto kubwa ilikua aina ya maisha yetu ni tofauti kabisa,
Nikaamua kuondoka na kumuachia chumba.
Ni vyema uongee nae kwanza,muelewane pamoja na urafiki ila atambue apo ni kwako.
Ukikaa nae ndipo utamjua ni mti wa aina gani.
 
Bila hakuna asiyekataa kuwa hali ni ngumu kwa kuwa sote tunapitia magumu maishani mwetu......lakini nyakati ngumu kwenye maisha yetu zisitufanye tuondokane na ubinadamu wetu na utu wetu kwani hata wewe unaweza kujikuta upo kwenye hali unayoiona kwa mwenzako........

Mimi na wewe hatufahamu kero alizokuwa anakumbana nazo huko alikotoka mpaka zikamsukuma kufanya maamuzi hayo.....bila shaka ameghafirika kama ambavyo binadamu wengine hughafirika wanapopitia magumu.....

Jambo la muhimu ni kukaa naye Kwa utulivu na kuzungumza naye na sio kumtimua huo ni unyama......

Haya maisha hayaeleweki kuna leo na kesho.......
sijakataa lakini angetumia ustaarab
 
Mm wala sio mnafiki,toka nimeanza kuishi gheto nimeishi na washkaji kibao mpaka nimekuja kuoa na wengine mpaka leo mazaga yako kama zipo kwangu,sijawahi kuishi pekee yangu gheto toka nimeanza kujitegemea
ukweli wangu ningemuuliza ana mpango wa kukaa muda gan halaf kuna ule urafiki unajua huyu mwana huwez mtupa kuna wale wa ku pass by aje anikere sasa mimi nasemea huyu wapili wa kupita,aje anikere bure? kwa nn tuje kukerana kama anakaa wiki wiki mbili its okay shida iwe ni gea ya kuingilia azidishe miez ubaya aanze kua sio wa kujiongeza ukirudi unakuta na boxer zako zimevaliwa
 
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi kuishi na watu sidhani kama nitaweza, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana nashindwa kuwa huru kabisa natamani nimtoe hapa hata kesho asubuhi

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

Mtafutie chumba cha Giza ni elfu 30, lipia miezi mitatu. Nunulia Godoro na shuka kule tandale. Nunua unga na dagaa, sufuria na sahani. Na jiko la Mkaa la elfu tatu.
Jumla 300k mpe elfu 50.
Kisha mwambie kila la kheri
 
Kulikuwa na maana gani ya kutumia neno rafiki yangu,at the same time unalalamika acha ubinafsi-sasa kama MTU ni rafiki yako unashindwaje kumpa hifadhi.
 
Mtafutie chumba cha Giza ni elfu 30, lipia miezi mitatu. Nunulia Godoro na shuka kule tandale. Nunua unga na dagaa, sufuria na sahani. Na jiko la Mkaa la elfu tatu.
Jumla 300k mpe elfu 50.
Kisha mwambie kila la kheri
unahisi huyu mtoa mada anazo hizo hela?? kumbe watu wa jf ni matajiri hivi
 
Wewe mwenyewe hauna kazi umesema umemaliza chuo, halafu hali ya mwenzako unaisema kuwa naye yeye ni jobless....

Mkuu urafiki wenu wa chuo ulikuwa wa namna gani tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom