Naombeni ushauri: Rafiki yangu amehamia kwangu na mabegi

Superleta

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
466
538
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili, nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza.

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi. Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe
 
Watanzania wengi tunakwama kwasababu ya aibu na kutokusema ukweli,mwambie ukweli aondoke akapange,kumfukuza kijana mwenye akili timamu na viungo vyote si dhambi na wala hutopata dhambi.

Sasa na yeye bila aibu hako ka chumba ka moja mtaishije?,Kama kakosana/kafukuzwa na mjomba wake ambaye ni tumbo moja na mama yake unadhani huyo mtu utamuweza wewe?

Anyway "KAZI YA BWEGE NI KUUMIA"
 
Mkuu usimfukuze huwezi jua ni yapi yaliyomsibu mpaka akafikia hatua ya kuondoka kwa mjomba wake kaa nae ujue shida ni nini na unamsaidiaje kama rafiki wa kweli.

Ikibidi mwambie kama mambo yake hayasomeki arudi nyumbani akajitafute ikiwa ana nyumbani kwao.
Stori yake inaweza kuwa kama ya INSIDER MAN .

Weka akiba ya wema maana haujui ni lini wema wako utakusaidia
 
Mvumilie mkuu. Ila inabidi mpange utaratibu wa kuishi hapo ghetto. Mchangie matumizi kama kodi, chakula n.k

Huwezi kujua leo na kesho huyo mwamba anaweza akatoboa kabla yako na akawa msaada kwako. Mvumilie in the mean time akiji-sort.

Ila ukiona anakuwa mzigo kwako yani sio mtu wa kupambania kombe mda wote yupo tu na simu JF mara Insta au anakuletea wanawake ghetto fukuza au hama muache.

Otherwise mvumilie huwezi kujua maana majaribu kama hayo yaweza kuja na neema.
 
Maisha ni safari ndefu sana na kwenye safari hiyo hakuna anayejua mbele kuna nini au kitatokea nini..... hivyo yatupasa kuwa makini na matendo yetu dhidi ya wanadamu wenzetu kwa kuwa maisha ni kitendawili....

Nyinyi bado angali vijana wadogo...bado mnatafuta mihimili ya kimaisha....katika hali kama hizo kuegemeana ni mambo ya kawaida kwa hata yeye mwenyewe hapendezwi na hali hiyo.......

Yakupasa kutumia hekima na busara juu ya jambo hili badala ya hasira.....

Hili ni jambo la kawaida lakini limekuwa kubwa kwa kuwa wewe umelipokea vibaya.......

Jiulize kwanza wewe mpaka kufikia hapo hujawahi kufanyiwa msaada wowote.....???

Ndugu zangu tujitahidi kuwa na stara kidogo tunapo shughulika na wanadamu wenzetu kwani kati yetu hakuna aliye salama katika hali zozote zinazowakumba wanadamu wenzetu.........
 
Kitu ninachojivunia ni kua mkweli, zungumza ukweli ajue ukiona hakuelewi ongea kwa vitendo ingiza manzi ako hapo tena unamwambia mwanake wangu anakuja atalala hapa tafta pa kulala mapema unaendaje sehem kukaa bila kutoa taarifa
 
Maisha ni safari ndefu sana na kwenye safari hiyo hakuna anayejua mbele kuna nini au kitatokea nini..... hivyo yatupasa kuwa makini na matendo yetu dhidi ya wanadamu wenzetu kwa kuwa maisha ni kitendawili....

Nyinyi bado angali vijana wadogo...bado mnatafuta mihimili ya kimaisha....katika hali kama hizo kuegemeana ni mambo ya kawaida kwa hata yeye mwenyewe hapendezwi na hali hiyo.......

Yakupasa kutumia hekima na busara juu ya jambo hili badala ya hasira.....

Hili ni jambo la kawaida lakini limekuwa kubwa kwa kuwa wewe umelipokea vibaya.......

Jiulize kwanza wewe mpaka kufikia hapo hujawahi kufanyiwa msaada wowote.....???

Ndugu zangu tujitahidi kuwa na stara kidogo tunapo shughulika na wanadamu wenzetu kwani kati yetu hakuna aliye salama katika hali zozote zinazowakumba wanadamu wenzetu.........
Shida sio kufanya stara, aliemfata mwenzie alipaswa kumwambia nakuja na mabegi yangu kwa ako nimezinguana naye sio kumvamia mwenzie sasa hivi maisha ni magum nyie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom