Naombeni ushauri: Rafiki yangu amehamia kwangu na mabegi

Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe

Hujuia neno la kutumia kumwambia aondoke au unataka ushauri wa nini?
 
kumbe una uzoefu tayari Sasa unaomba ushauri wa nini, Fanya kama ulivyofanya kumtoa rafiki yako wa kwanza.
 
unajua huyu anapiga mishe gan?? kama na yeye anabangaiza mzigo umeongezeka? mnamsaidia kutafta kula? aliehamia kwa mwenzie alitakiwa atoe taarifa tu kwamba nakuja kwako kujihifadh nimezinguana na anko ili huyu ajue ana mgeni atakaye kaa muda

Nategemea rafiki yangu anielewe zaidi ya ndugu yangu wa damu! Rafiki yangu Kama ni rafiki wa kweli anatakiwa kusimama na Mimi kabla hata sijamuomba!

Ama nini maana ya urafiki? Unless ni Unafiki.
 
Huyo ni mpuuzi fukuza .Alitakiwa akuambie kabla sio kuhamia ghafla na mabegi .
 
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe
Mpokee rafiki yako kwa mikono miwili, mkirimu, awe huru kabisa hapo kwako. Ajione yupo nyumbani kabisa.

Maisha ya ujana huwa hayachelewewi kupita, ni kama Moshi.

Tumia fursa hiyo kuonesha utu wako wa hali ya juu. Kaa nae ki hekima. Mwenyezi Mungu aliyemfikisha hapo kwako ndiye mwenye kujuwa yaliyojificha. Usitafute maovu wala mabaya, tafuta mema na uzidishe wema kwake kila siku.

Ni mambo ya kupita tu hayo.

Kila utachokifanya kwake sasa hivi kitaishi nae milele.
 
Huyo ni mpuuzi fukuza .Alitakiwa akuambie kabla sio kuhamia ghafla na mabegi .
Hapana, sikubalini na wewe. Atahama tu, taratibu, huyo hapo anajiengesha kwa yaliyomkuta alipotokea, na huyo rafiki yake hata asimuulize, yeye ampokee kwa mikono miwili.
 
Kuna mwanangu nilimstiri hivo hivo tukatoboa wote we keep it real sisi so wana, wa kukunja mashauzi kibao nikiwa na buku nampa mwanangu jero nikununua range namsusia pajero
Song: rafiki wa kweli
Artist: langa
Sijui unaishije na, mwanao ila mimi wanangu torati sheria
 
Hapana, sikubalini na wewe. Atahama tu, taratibu, huyo hapo anajiengesha kwa yaliyomkuta alipotokea, na huyo rafiki yake hata asimuulize, yeye ampokee kwa mikono miwili.
Ukweli umenipiga kwa logic .ila baada ya muda walau wiki mbili amuulize
 
Hana haja ya kumuuliza, wema na ukarim utamfanya mwenyewe afunguke. Amsaidie kwa hali na mali. Baada ya siku tatu aanze kumpangia majukumu kama mwenyeji tu.

Asimfukuze, asimsimange wala asimnyanyapae. Ahakikishe anakula na kuvaa vizuri na yupo comfortable kabisa kwa furaha na bashasha.

Maisha ni safari fupi sana lakini mambo yake ni marefu sana.

Ukitaka kufurahia maisha, ishi kwa kuhudumia wengine wanapokuhitaji, usiishi kwa kujihudumia mwenyewe.

"Today it's me, tomorrow you".
 
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili, nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza.

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi. Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe
Ukiacha kulala hapo, atakugharimu nini? Kama ni chakula mpe yeye jukumu la chakula, mshirikiane umeme na maji.
Kama ameingilia faragha yako, mpe muda, ukifika ni lazima aondoke (usiwe kama Samia na dpw). La kama huwezi kukaa naye kabisa, muondoshe haraka kabla hajajenga mazoea.
 
Watanzania wengi tunakwama kwasababu ya aibu na kutokusema ukweli,mwambie ukweli aondoke akapange,kumfukuza kijana mwenye akili timamu na viungo vyote si dhambi na wala hutopata dhambi.

Sasa na yeye bila aibu hako ka chumba ka moja mtaishije?,Kama kakosana/kafukuzwa na mjomba wake ambaye ni tumbo moja na mama yake unadhani huyo mtu utamuweza wewe?

Anyway "KAZI YA BWEGE NI KUUMIA"

dah "KAZI YA BWEGE NI KUUMIA"
 
Wanaume wa Dar mna tabu.. urafiki wenu ni wa mashaka siku zote. Achilia mbali mabegi huku kijijini kwetu hata angekuja na familia nzima tunawapokea fresh tu
 
Acha roho mbaya mbebe hata mwezi mmoja tu
Kwanini vijana wa sikuizi tuna roho mbaya Watanzania waleo wamekuwa na roho mbaya kutokana na Serikali ya CCM kuwasababishia maisha magumu, mbona wazee wetu wallikuwa hawa fikuzi wageni wakija kuishi majumbani kwao, Nyumbani kwetu watu walikuwa wanakuja kuishi tena ni jirano zake Baba yetu uko kijijin kwao lakini mzee wetu alikuwa ana wapokea na Mzee wetu alikuwa choka mbaya. Kwaiyo huyu mlalamikaji aishi tu na huyo rafiki yake kwa moyo wote.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama ni rafiki yako huyo. Kama ni kweli rafiki basi urafiki wenu ni wa mashaka sana. Rafiki huwa mnashare feelings, mnagawana andazi moja, mnalala. Hilo suala kama kweli ni marafiki Wala usingekuja kuomba ushauri huku.
 
Maisha ni fumbo hakuna aijuae kesho wala baadae yake. Hamna hata mmoja anayependa shida na matatizo. Kiasi cha yeye kuwaacha wote na kukufata wewe maanayake kakuamini. Wote tupo kwenye kutafuta, mafanikio ya mtu yapo mikononi mwa mtu, huwezijua labda mafanikio yako yako mikononi mwake. Kingine kilamtu ana kheri na shari zake. Huwezijua labda uwepo wake ukakufungulia milango ya baraka.

Muweke chini, ongea nae vizuri mpange mipango nini cha kufanya ili kujikwamua kimaisha. Kikubwa ni kuombea dua tu na kuishi bila kinyongo. Huo ndio urafiki, kuna nyakati urafiki unakua zaidi ya undugu.
 
Back
Top Bottom