Naombeni ushauri: Rafiki yangu amehamia kwangu na mabegi

Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi kuishi na watu sidhani kama nitaweza, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana nashindwa kuwa huru kabisa natamani nimtoe hapa hata kesho asubuhi

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe
Pole sana mkuu! Ushauri wa haraka usikurupuke maana hata yeye sidhani kama atakuwa na furaha kukaa kwako kwa muda mrefu. Cha kufanya mpe muda wa siku tatu kwanza baada ya hapo ukae nae na kuzungumza ujue ana mipango gani.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Mtafutie chumba cha Giza ni elfu 30, lipia miezi mitatu. Nunulia Godoro na shuka kule tandale. Nunua unga na dagaa, sufuria na sahani. Na jiko la Mkaa la elfu tatu.
Jumla 300k mpe elfu 50.
Kisha mwambie kila la kheri
Hizo hela za kumpangia natoa wapi mimi mwenyew ndo najitafuta?
 
Sasa ataishi vipi naye kama hana hizo Pesa.
Hapo watagombana tuu.

Urafiki wa ukubwani mara nyingi niwa mashaka. Ingawaje sio wote.
kuna watu wamenivamia hapo juu nimeambiwa ninaroho mbaya wakat nimeshauri sawia mtoa mada anaonekana ni mtu wa kujitatftia riziki kwa kipato ambacho kinamtosheleza yeye ndio maana kuja kwa jamaa amepata stress hajui wataishije kama mzigo umeongezeka na kama wangekua wana walioshibana kwashida na raha yasingetokea yan uje na kuondoka then boom kagombana na anko anahamia na mabegi like real?? akimfia humo ndani itakuaje watu wanapenda kupokea mizigo
 
Hizo hela za kumpangia natoa wapi mimi mwenyew ndo najitafuta?
make sure unajua kilichomtoa kwa mjomba wake, usikae naye kizembe huyo ni binadam watu tunatembea na kifo akikufia humo ndani had uje ujulikane huna hatia my nigga umesota sana
 
kuna watu wamenivamia hapo juu nimeambiwa ninaroho mbaya wakat nimeshauri sawia mtoa mada anaonekana ni mtu wa kujitatftia riziki kwa kipato ambacho kinamtosheleza yeye ndio maana kuja kwa jamaa amepata stress hajui wataishije kama mzigo umeongezeka na kama wangekua wana walioshibana kwashida na raha yasingetokea yan uje na kuondoka then boom kagombana na anko anahamia na mabegi like real?? akimfia humo ndani itakuaje watu wanapenda kupokea mizigo

Sio kwamba angeomba akasuluhishwe na Mjomba wake ili aendelee kukaa Kwa Mjomba labda ingekuwa sahihi.
Au pengine anataka Uhuru ambao haujaifikia, yaani Wakati wake haujafika.

Hapo kama mshikaji Hana Pesa hakuna jinsi itabidi amchane makavu kuwa hapa mambo bilabila. Na hataweza kuishi naye.

Amwambie kuwa kama wamegombana na mjombaake yupo tayari kwenda kuwapatanisha
 
make sure unajua kilichomtoa kwa mjomba wake, usikae naye kizembe huyo ni binadam watu tunatembea na kifo akikufia humo ndani had uje ujulikane huna hatia my nigga umesota sana

Hospitalini Daktari ndio hutoa chanzo cha kifo. Hilo wala lisimtishe ikiwa ni Rafiki au classmates mwenzake.
 
Sio kwamba angeomba akasuluhishwe na Mjomba wake ili aendelee kukaa Kwa Mjomba labda ingekuwa sahihi.
Au pengine anataka Uhuru ambao haujaifikia, yaani Wakati wake haujafika.

Hapo kama mshikaji Hana Pesa hakuna jinsi itabidi amchane makavu kuwa hapa mambo bilabila. Na hataweza kuishi naye.

Amwambie kuwa kama wamegombana na mjombaake yupo tayari kwenda kuwapatanisha
kati ya watu wote tuliochangia wewe umeza kikubwa sana uko sahihi amsaidie kumuombea msamaha dizain kama kuja na kuondoka kwake kwa mtoa mada ameyapenda hayo maisha sasa n kama kapata mlango wa kutokea
 
Huo wema unaoufanya hapo Mungu atakulipa maradufu. Ila kuwa makini na washkaji ambao hawawezi kukwambia situation mpka aje mazima. Maana yake hakuamini na anakuona wewe siyo mwana. Yaani wewe ni kimeo. Hana inshu na wewe kama alishindwa kukutaarifu kuja kwake hapo mazima basi jiandae kwa vitukio vya kustukiza.
 
Niliwai ishi najamaa/class mate wachuo ambaye hakuwa mwana kabisa tena hakutoa taarifa kuwa anakuja nilimpokea mwana nilikuwa na life lakuunga haswa. Kabla hajaja nilikuwa nimetoka kufukuzwa kazi afu mwana kaniungia bila taarifa nilimpokea kusema kweli sikuwa pungukiwa kitu baada ya mwezi nikapata mishe na yeye nikamtafutia mishe baada ya mwaka na nusu tukaachana
Japo sio mwana kivile mpaka leo nilitoa msaada ambao sitegemei malipo tona kwake
Yes, this is what I said. Kama anakuja bila kukuelezea situation maana wewe si rafiki wewe ni college mate. Rafiki au mwana utajua inshu zake na wewe ndo utatoa options. Na hili lako. Litamkuta. Atende wema Mungu atamlipia ila huyo jamaa ana mashaka
 
Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili,nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza

Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi

Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko

Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta

Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?

Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona

Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu

MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe
Umewezaje kuleta hii mada hapa una uhakika yeye hayupo jf kweri,maana akiona huu ujumbe wako atakuchukia maisha yake yote.
 
Kwanza huko ni kukosa ustaarabu unahamiaje nyumbani kwa mtu kama unaingia pangoni yani....kuna watu ustaarabu hawana ila watakachoona ni roho mbaya kwa mtu.

Kwanini asiseme mapema kuwa mambo hayajakaa fresh aje akae kwa muda wakati anacheki ramani, huyo ni mtu wa ovyo.
 
sema wewe
 
Kabisa na hakunitaarifu kabisa
 
Umewezaje kuleta hii mada hapa una uhakika yeye hayupo jf kweri,maana akiona huu ujumbe wako atakuchukia maisha yake yote.
Mimi sijali kwa sasa maana nachotafuta ni ushauri hajafanya uungwana kbs
 
Back
Top Bottom