Naombeni ushauri kuhusu hawara yangu

Naombeni ushauri kuhusu hawara yangu

Ewe mwana mpotevu. Rudi nyumbani kwako, mke na wanao wamekusubiria!!!!
Kwa Uzi wako huu yawezekana home huachi hata matumizi ila huyo kimada wako Salary inateketea.
 
Aliwazalo mjinga ndilo humfika, hongera shemeji endelea kumuendekeza hawala ila ipo siku litakufika akili itakufunguka
 
Jamani mimi nina mke tena mzuri wa tabia na watoto, namheshimu kwa sababu ananipenda na kunijali. Kama mada ilivyo, tangu mwaka jana nilikutana na dada mmoja anafanya kazi serikalini nikatokea kumtamani sana. Kama mwanaume nikakomaa nikampata akawa hawala yangu mpaka sasa. Kuna kila dalili kuwa hanipendi lakini kwa sababu nilishamuweka moyoni nashindwa kumwacha na mara nyingi ananijibu anavyojisikia. Huwa nakasirika lakini kwa sababu kwa majibu yake lakini nikitaka kumjibu najiuliza sana, anaweza kuniacha... lakini mwishowe naamua kuuchuna. Hivi siku mbili zilizopita tulikosana hakunitafuta mpaka nilipomtafuta nikaamua kujishusha ili yaishe. Sio hilo tu, mara nyingi tu ananijifanya yeye ndio kidume mimi chini yake. Wanawake wengine wananiambia kwa nini nahangaika na huyo mwanamke, (ambao wao wanamwona hana uzuri) wakati mke wangu ni mzuri? Siwaelewagi naona kumpoteza ntateseka sana moyoni.
NAOMBENI USHAURI NIFANYE NINI ILI NIMCHUKULIE POA? NAUMIA SANA HATA LEO TUMENUNIANA NAE
Utakuta huyo HAWARA sura kama SAFARI BUTI . Bado unajipendekeza KULA KONA FASTER HAKUFAI
 
Pole sana, hayo ni matokeo ya uzinzi. Umeshikwa masikio kiongozi.
 
Umelishwa limbwata mkuu ipo siku utamuacha mkeo utahamia kwake mazima siku akili yako ikikurudia na ww utaanza kujishangaa nilipenda nn hapa
 
Jamani mimi nina mke tena mzuri wa tabia na watoto, namheshimu kwa sababu ananipenda na kunijali. Kama mada ilivyo, tangu mwaka jana nilikutana na dada mmoja anafanya kazi serikalini nikatokea kumtamani sana. Kama mwanaume nikakomaa nikampata akawa hawara yangu mpaka sasa.

Kuna kila dalili kuwa hanipendi lakini kwa sababu nilishamuweka moyoni nashindwa kumwacha na mara nyingi ananijibu anavyojisikia. Huwa nakasirika lakini kwa sababu kwa majibu yake lakini nikitaka kumjibu najiuliza sana, anaweza kuniacha lakini mwishowe naamua kuuchuna.

Hivi siku mbili zilizopita tulikosana hakunitafuta mpaka nilipomtafuta nikaamua kujishusha ili yaishe. Sio hilo tu, mara nyingi tu ananijifanya yeye ndio kidume mimi chini yake. Wanawake wengine wananiambia kwanini nahangaika na huyo mwanamke, (ambao wao wanamwona hana uzuri) wakati mke wangu ni mzuri? Siwaelewagi naona kumpoteza nitateseka sana moyoni.

NAOMBENI USHAURI NIFANYE NINI ILI NIMCHUKULIE POA? NAUMIA SANA HATA LEO TUMENUNIANA NAE
Atakuwa kakufanyia mambo
 
Tamaa zako mbaya zimekuponza...Acha kuugua mapenzi piga chini...Baki njia kuu
 
Mrudie mkeo na ubaki nae pekee, unachofanya mungu hapendi, utapata adhabu duniani na akhera.
 
Aliwazalo mjinga ndilo humfika, hongera shemeji endelea kumuendekeza hawala ila ipo siku litakufika akili itakufunguka
asante kwa ushauri mzuri, ila nikijaribu kumwacha naumia moyoni,,, namrudia. Nimejaribu mara nyingi tu nashindwa
 
Mkeo nimshauri cha kufanya usimpende huyo mwanamke. (utani)
 
Ebwanaeee pole kwanza mzee mwenzangu. Ushauri wangu ni huu. Mchukue mkeo toka naye mazingira ya nyumbani mwende mkalale hotelini. Then mweleze ukweli na mpigie magoti kumwomba msamaha na umwambie hurudii tena. Nakuhakikishia utarudi kunipa majibu
 
Back
Top Bottom