Naombeni ushauri kuhusu hawara yangu

Jan 17, 2017
86
95
Jamani mimi nina mke tena mzuri wa tabia na watoto, namheshimu kwa sababu ananipenda na kunijali. Kama mada ilivyo, tangu mwaka jana nilikutana na dada mmoja anafanya kazi serikalini nikatokea kumtamani sana. Kama mwanaume nikakomaa nikampata akawa hawara yangu mpaka sasa.

Kuna kila dalili kuwa hanipendi lakini kwa sababu nilishamuweka moyoni nashindwa kumwacha na mara nyingi ananijibu anavyojisikia. Huwa nakasirika lakini kwa sababu kwa majibu yake lakini nikitaka kumjibu najiuliza sana, anaweza kuniacha lakini mwishowe naamua kuuchuna.

Hivi siku mbili zilizopita tulikosana hakunitafuta mpaka nilipomtafuta nikaamua kujishusha ili yaishe. Sio hilo tu, mara nyingi tu ananijifanya yeye ndio kidume mimi chini yake. Wanawake wengine wananiambia kwanini nahangaika na huyo mwanamke, (ambao wao wanamwona hana uzuri) wakati mke wangu ni mzuri? Siwaelewagi naona kumpoteza nitateseka sana moyoni.

NAOMBENI USHAURI NIFANYE NINI ILI NIMCHUKULIE POA? NAUMIA SANA HATA LEO TUMENUNIANA NAE
 
Jamani mimi nina mke tena mzuri wa tabia na watoto, namheshimu kwa sababu ananipenda na kunijali. Kama mada ilivyo, tangu mwaka jana nilikutana na dada mmoja anafanya kazi serikalini nikatokea kumtamani sana. Kama mwanaume nikakomaa nikampata akawa hawala yangu mpaka sasa. Kuna kila dalili kuwa hanipendi lakini kwa sababu nilishamuweka moyoni nashindwa kumwacha na mara nyingi ananijibu anavyojisikia. Huwa nakasirika lakini kwa sababu kwa majibu yake lakini nikitaka kumjibu najiuliza sana, anaweza kuniacha... lakini mwishowe naamua kuuchuna. Hivi siku mbili zilizopita tulikosana hakunitafuta mpaka nilipomtafuta nikaamua kujishusha ili yaishe. Sio hilo tu, mara nyingi tu ananijifanya yeye ndio kidume mimi chini yake. Wanawake wengine wananiambia kwa nini nahangaika na huyo mwanamke, (ambao wao wanamwona hana uzuri) wakati mke wangu ni mzuri? Siwaelewagi naona kumpoteza ntateseka sana moyoni.
NAOMBENI USHAURI NIFANYE NINI ILI NIMCHUKULIE POA? NAUMIA SANA HATA LEO TUMENUNIANA NAE
Hawala= hawara
Pole kwa mateso ya Misri, umekuwa mtumwa, zoba na kinyamkera.
Ana nini kumzidi mkeo?
Unadharauliwa unang'ang'ania!
Acha ujinga wewe rudi kwa mkeo unaleta aibu
 
Maamuzi unayo, alafu unatuomba ushauri, tutakushauri nini zaidi ya kukwambia achana nae.
 
wacha ufuska bwana..tosheka na mkeo...hawa wanawake ni wengi ajabu..tena warembo kupindukia...yafaa uwe mtu wa kuridhika na maamuzi ulioyafanya ya kumfanya huyo aliye ndani mkeo...wengine achia walio single wachague..wewe tayari ushakuwa family man..na kama dini inaruhusu kuoa zaidi ya mwanamke mmoja basi fanya hivyo..
 
Ndugu umeshikwa akili sio bure, Mungu kakubaliki umefikia level ya kuwa na mke mzuri na watoto halafu bado unalia lia na kuwa mtumwa kwa hawara??? Nuksi nyingine mnazitafuta wenyewe. Muombe sana Mungu wako.
 
Pole asee
Jaribu kumshirikisha na mkeo

Ila seriously mkuu jaribu kumtoa moyoni the same way ulivyomuweka moyoni. . .yani jitahidi kilichokuvutia kipindi unamuona kiuliwe na dalili unazoziona hupendwi nae mixer majibu yake ya hovyo

Ukishaziua sasa mfikirie mkeo mzuri na watoto wako nyumbani ,hapo upendo unaweza kurudi

NOTE
Kama hawara yako alitumia mbinu kama limbwata,kojo naomba nikupe pole maana sijui njia za kujitoa katika hayo mavitu
 
Back
Top Bottom