Naombeni ushauri kaka na dada zangu

Azimio la kazi

Senior Member
Jun 7, 2023
138
451
Wakuu nipeni ushauri mdogo wenu.

Nipo kwenye mahusiano na huyu binti kimsingi tulianza mahusiano kipindi nipo mwaka wa kwanza chuoni (hivi sasa nipo mwaka wa pili), lakini yeye tayari hivi sasa kamaliza masomo na yupo nyumbani (amesoma Diploma ya clinical medicine).

Lengo la mahusiano yetu ni badae tuanzishe familia kwa pamoja ( kufunga ndoa)

Umri wake ni mkubwa kwangu ananizidi miaka miwili Mimi ni wa 2001

Ni zaidi ya mara manne sasa huyu binti ananambia kuna wanaume ambao wanamu-approach kwa ajili ya kumuoa, hata rafiki zake wa kike mara nyingi huniambia kuwa huyu binti anawindwa na wanaume wengi tena ambao wapo seriously na wenye maisha yao.

Ofcourse hata mimi naweza ku confirm hicho kitu maana she is beautiful pia ana akili na ufahamu mzuri, she is completely wife material.

Jana usiku amenitumia screenshot za chats za jamaa ambaye ni engineer jamaa anamwambia kabisa anataka kumuoa mwakani na yupo seriously.

Ugumu unakuja hapa, mimi bado nipo chuo tena maisha yangu ni kawaida sana, na nyumbani kwetu hali si nzuri hata kidogo, kiufupi bado na safari ndefu sana ya kujitafuta kimaisha.

Naona kabisa huyu binti nitamchelesha kwenye maisha anayotaka, na yeye anajua hali yangu hiyo, natamani kumwambia akubali hao wanaomchumbia lakini sijui atapokea vipi, maana tunapendana , na mimi napotazama safari ya maisha yangu bado naona ukungu na giza kubwa sana.

Sitaki kumzibia riziki huyu binti, najua ananipenda na mimi pia na mpenda sana.

Hapa nipo njia panda, sijui nifanye maamuzi gani kwa manufaa ya Kila.
 
Kama uliwahi kupiga, mwambie ukweli wewe huna maisha bado una jitafuta sana. Kama ana kupenda kweli akuvumilie, kama hawezi kukuvumilia aolewe tu wewe huna neno. Japo una mpenda kweli ila kuendelea kubaki nae na yeye kuna mijitu yenye maisha yao ina mfuata una ona ni kumzibia ridhiki basi aolewe tu.
 
Mwanamke anaekupenda ababaishw Na hao wanao mtongoza,mwanamke KUTONGOZWA kawaida,umr wako bado mdogo SOMA kwanza ACHANA Na kichwa cha chini tumia cha juu kufikiria Na s hisia.huyo mwanamke atakusumbua sana Muda utaongea usije ukaleta uzi kuwa umetendwa vibaya.

MWISHO MWENYE MAAMUZ NI WEW
 
Una jirani ,rafiki au ndugu.au unaishi kama
Rango
IMG_0137.jpg
 
Miaka 22 mwaka wa pili unang'ang'ana na binti aliyemaliza chuo?

Hata kama mngekuwa mmemaliza wote, bado ungekuacha na aolewe na mtu mwenye maisha.

Wewe zingatia masomo huyo siyo size yako.

Huyo Injinia atakuwa kazaliwa miaka ya 80 au tisini, yaani watu hawa wana maisha tayari na tunapendwa haswa.

Sasa wewe mwanangu wa 2001, subiri wasichana waliozaliwa 2010 ambao sasa hivi wana miaka 13, ambapo 2033 watakuwa na 23 years na wewe ukiwa na 32 na maisha juu.

Kupanga ni kuchagua. Mwanaume anapanda chati kadiri umri unavyokwenda.
 
Back
Top Bottom