Kuna mini kabang ya tigo 3500 tu, unapewa dk 75 sms 2000 na mb 500
Ukiunganisha anakuwa hana sababu nyingine.
mkuu hawa beki 3 ni changamoto kwa kweli ukisema umlimit ndo utaumia kabisa hata mtoto anaweza akaugua gafla akashindwa kukupa taarifa chamsingi nunua sim ya mezani alafu unaunganisha laini moja tu ya kwako akipiga sehem nyingine sim haiendi hapo utakua umemkomesha
1000 kwa wiki??? inatumikaje???
Nawasalimu wana MMU.
Jamani tuna hawa wadada wanatusaidia kukaa na nyumba zetu.
Kama tujuavyo maisha ya siku hizi bila simu inakuwa patashika kidogo.
Huwa mdada akija kama hana simu huwa nampa simu ambayo nimeinunua kwa ajili ya nyumbani ili niweze kuwasiliana naye naye awasiliane nami ambapo sipo nyumbani.
Na kama inatokea mdada kaja na simu yake basi simlazimishi atumie ile yangu, huwa natumia tu ile namba yake kwa mawasiliano.
Kinachotokea mpaka naomba mwongozo hapa ni kwamba; Huwa nampa sh. 1000 kila wiki kwa ajili ya simu, ili akipata dharura basi aweze kunitaarifu. Mara nyingi mimi huwa napiga simu nyumbani mara kwa mara kwa hiyo inatokea mara nyingi tu ndani ya wiki hajanipigia wala kutuma sms hata moja, na yaweza kuwa hivyo hata mwezi mzima.
Kinachonichosha, siku ikitokea kapata dharura wala hapigi, nikiuliza naambiwa simu haina hela.
Wenzangu pia mnakumbwa na hili tatizo?
Nifanyeje sasa ili hili tatizo liishe?
sababu wakati mwingine ni jambo la maana kabisa linatokea lakini hawezi kuniambia kisa hela kwenye simu kamaliza zoote kupigia watu wake, sasa maana yoooteee ya mimi kumpa hela ya simu inakuwa haipo.
Nimepata mdada mpya sasa nataka nianze naye tangu mwanzo sheria ya hela yangu ya simu iweje........
Hayo yooooote uliyoaorodhesha hapo ni mambo ambayo ni ya msingi kwa binadamu yoyote yule kuyapata na hutakiwi kuyahesabu kabisa kwa mtu ambae anakulelea wanao,kukufulia,kukusafishia nyumba yako n.k
Mshahara unaompa hautoshi kukamilisha mahitaji yake yote ikiwemo na vicha kwaajili ya kuwasiliana na wazazi,ndugu na jamaa zake,sio kwakuwa yeye ni msaidizi wako basi asiwasiliane nao,lakini cha ajabu zaidi ni wewe kuona mtu kupewa sh 1000 kwaajili ya vocha wiki nzima kuwa ni sawa
Sijui unaonaje kuwa ni sawa hata kama unamhudumia yote hayo uliyoyasema
Ni kwanini ukimfanyia ndugu yako huyahesabu lakini kwa msaidizi wako unayahesabu?
Au ndugu yako ni binadamu kuliko msaidizi wako wa kazi?
Usimpe hela weka tu utaratibu wa kupiga kila siku mara mbili au tatu..au weka hela simu ya nyumbani sio yake
If only everyone else had the same perception about house-helps like you then the world would have been a better place!!! Do not underestimate the power of someone who cooks for you, cleans up after you, look after your kids when you are out making money, literally gets the house running in your absence. Tuwapende na kuwaheshimu hawa mabinti jamani, treat them like they were your own family, akikosea mkanye like you would do your own siblings, hizi shida ndogo ndogo za kila siku utazisikia kwa jirani tu!
natamani hii pia ionwe na BAK na Eiyerhakuna mtu anayetaka kuwanyanyasa hawa beki 3 hata kidogo--sote tunaishi nao kiundugu na kirafiki. tunachojaribu kuongelea hapa ni JINSI GANI YA KUWA-SHAPE ILI WAWE NA MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI ZA WAAJIRI WAO--hii ndiyo point and there's no one claiming to look baby sitters down his/her nose!!!
mfundishe huduma ya tafadhali nipigie...mpe mazoezi ya kufanya hivyo angalau mara moja kwa siku....
ukimuunganishia hv ndio ataacha kazi zote atakaa kupiga cm cku nzima! wewe beki 3 huwajui vzr eeh?
Mie huwa sijitii headache na maid hata siku moja. Kwa suala hili uliloleta hapa, nakushauri ununue mobile fone ya mezani. Nenda voda hapo wanakupa lisimu la mkonge, ukiwa nyumbani unawaka halijafutwa vumbi. Hicho kimobile ndo kwanza unampigia yuko mtaa wa tatu na anakujibu niko home, hali shwari!
but anyways, kukaa na msichana ukimfanya comfortable utafaidi wewe. Mpigie wewe, tena mruhusu akutumie msg ya tafadhali nipigie kama ana shida yoyote. Tena jumapili kaa na wanao, muache dada akabarizi kwa maboifrendi. jirani wa kakangu alikuwa mkali hapo UDSM, hgal haruhusiwi kupiga picha hata na mwanae wala wanae hawaruhusiwi kwenda kwa jirani. Siku mwanae alikuwa anaharisha, kina dada wakakaa kimya tu na sie tuko home tunaangalia tv tu. By the time mama mtoto anarudi saa moja usiku, anakamata mwanae kwenda hospitali, mtoto anafariki!
mtoto anaweza kuungua ama kuumia mbele yako na usiweze kumlinda. Relax
Rafiki yangu BAK, hakuna sehemu nimesema sitaki aongee na ndugu zake..... aongee nao tu any time, sina shida na hilo.
Sijui naeleweka hapa au la; huyu mtu nampa 1000 kwa wiki kwa ajili ya kunipigia endapo dharura itatokea nyumbani, ni kiasi cha kutoa taarifa tu. Siku hizi bongo simu ni very cheap kupiga, yaani mimi hata sms naonaga uvivu kutuma. napiga kwenye mtandao wowote, muda wowote, ni cheap sana. huyu mdada anaweza kaa mwezi mzima asinipigie simu ya dharura, inawezekana hata miezi mi3 au mi4, kila siku huwa anapokea tu simu zangu. lakini sasa ikija tokea kumetokea dharura na anahitaji kuwasiliana nami anasema hana airtime, unadhani hiyo ni fair?
Kuhusu wababa kusaidia kuangalia wadada endapo mama hayupo hilo halina mjadala, wababa wote wanafanya hilo. Ila naweza kukushangaa sana rafiki mkeo yupo sitting room wewe upo busy kumwelekeza dada jinsi ya kufanya kazi pale nyumbani, utakuwa unafanya kazi si yako.
Have a good day as well:smile-big::smile-big:
simu la MKONGE? hahaha! mkuu umenichekesha sana! hata mi nalitamani.
Bahati mbaya hata ujui mada ipi ya kutoa povu ila kwa kuwa umejua kusema neno hilo basi unalitumia hata mahali ambapo halina haja,mfano wako ulioutoa mbona haulingani na mada iliyopo?elewa somo kwanza kabla ya kutema povu. hakuna mtu aliyemzuia kuwasiliana ila aweke fedha zake, asitumie vibaya mali ya mwajiri.
imagine umemtumia mwanao karo halafu amechukua amekula yote kisha akarudishwa home. unapomuuliza anakuambia alichukua pesa ya karo akachezea kamari! utamuelewa?