Naombeni muongozo wa kupima DNA

Naombeni muongozo wa kupima DNA

Kwa ushauri wangu, nenda Nairobi, Kenya. Watafute Lancert Lab wakupe huduma.
Bongo nioso.
Hakuna cha Nairobi wala wala wapi mwamke agome mtoto kupimwa DNA

Kila kitu hapa hapa Tanzania hakuna cha Nairobi wala wapi
 
Kwa ushauri wangu, nenda Nairobi, Kenya. Watafute Lancert Lab wakupe huduma.
Bongo nioso.
Wakenya mnajitia wajanja hakuna cha Nairobi wala nini kila kitu hapahapa huko Nairobi mkapimane wakenya kwa wakenya mtu wetu haji huko
 
Wanakuja kukupa muongozo ila sikushauri kabisa utakuja kukutana na madude usielewe nn kimetokea. Ila kama unajiweza nenda kapime ila kama unajua maisha yako bila huyo mke utateseka jiachie tu fanya mambo yako.
Siyo mke ndugu ni mpita njia tu wala hana future naye na mtoto now ni 7yrs old.
 
But kadri ya uelewa wangu hapa Tanzania sheria haziruhusu mtu binafsi kwa mapenzi yake kupima dna. Maombi ya kupima dna huwasilishwa kwa mkemia mkuu na taasisi kama vile mahakama, jeshi la polisi, ofisi ya ustawi wa jamii nk
Mbona sheria ni ngumu kiasi hiki.
 
TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA VINASABA

Taratibu za kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba

Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009. Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na

Maafisa ustawi wa jamii, Mawakili, Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro, Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai, Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba, Wakuu wa Wilaya,Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria

3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki .

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
Utaratibu mgumu sana
 
Kitanda hakizai haramu piga chini hilo wazo ila kama mamaake anazingua mkazie
Mama yake mbwa kabisa.

Mtoto huyu awali alikuwa na Baba 3 ambao wote kipindi cha mimba waliambiwa ni wahusika.

Baadaye wote wakafahamu kila mmoja akazingua now ni miaka 7 sasa huyu mwanamke kangangania mwanaume 1 akidai ndiyo mhusika.

Hapo hatakama ni wewe utakubaliaje.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Nov 2023 lenye kichwa Cha habari"Serikali yatoa Mwongozo wanaotaka kupima DNA"

Utaratibu ni kuwa na barua kutoka either 1)Ustawi wa Jamii 2)Mwanasheria au 3) mahakama then utaipeleka ofisi ya mkemia.

Utapewa Control number ulipie 300,000.Then mambo mengine yatafuata.
Shkrani
 
Mkuu DNA za hospital za kibongo naskia zinawa-favor wanawake sana ukienda elewa tu jibu ni kwamba mtoto ni wako... Hutopata jibu lingine.
Hata mimi nimesikia jambo hilo, kuwa hakuna ukweli
 
Ulipochomeka dude lako live hilo katikati ya mapaja hukujua kuwa waweza tia mimba mtu au kumpa au kupata ukimwi mjinga wewe?

Unakuja kutusumbua Jamii Forums na ubwege wako
Kila mtu hufikiri kilingana na uwezo wake kielimu, na kiuchumi, hivo masikini muda wote hujaa hasira na chuki kwa kila jambo.

Asante kwa mchango wako.
 
Wanakuja kukupa muongozo ila sikushauri kabisa utakuja kukutana na madude usielewe nn kimetokea. Ila kama unajiweza nenda kapime ila kama unajua maisha yako bila huyo mke utateseka jiachie tu fanya mambo yako.
Mateso ni ya mda tu akapime
 
Back
Top Bottom