Huo ndo msimamo unatakiwa,unaweza kuchoma nauli,ukachomeshwa mahindi na mtu usimwone.kama anania ya kukusaidia angeweza bila hata ya hizo complicationSitaweza kufika ndugu kwa maana sina uhakika wa kukutana na wewe kwa maana hata mawasiliano hutaki kutoa na ulisema utanipeleka ubungo ukate tiketi na sasa umebadilika tena.
Mkuu unaonekana huna nia thabiti.huwezi kumwambia mtu aje mahali ambapo hakuna appoitment y uhakika.namba yako hutaki kutoa atakuamini vp.? hata kama utatuma mtu lakini dhamani yake ni wewe.kwahiyo namba yako ni muhimu awe nayo.
Pole sana dada, ntakusaidia hata kidogo.
Naombeni mnisaidie nauli tu ya kurudi kwetu Same na mwanangu wa miezi 8 na hata mnisaidie na sh.elfu hamsini tu nikaanzie biashara ya mahindi pale Same mjini.Mume ni mtu wa Kigoma. Namba yangu ya simu ni 0712 319 836
Natafuta chumba kibaha maili moja,chumba kiwe kisafi na jiko liwepo maji yawepo kwenye hiyo nyumba.Nalipa elfu 60000 kwa mwezi nitalipa miezi minne.Mwenye nacho anitafute 0762 629138.
Pole sana dada, ntakusaidia hata kidogo.
Kuna kupindi ulikuwa unatafuta nyumba Kibaha kwa namba nyingine. Umebadilisha namba?
Nashukuru sana nimepokea sh.5000 kutoka kwa SAMBOKO wa JF.Mungu akubariki sana.
Naona elfu 21 imepatikana...Hapo buku 20 nauli mpaka same, elfu moja utanunua juice na keki ya mtoto kwenye bus...Ndio maisha dada ukawasalimie Same...Usisahau kutuaga ukianza safari.
Nashukuru sana nimepokea sh.5000 kutoka kwa SAMBOKO wa JF.Mungu akubariki sana.
Huo ndo msimamo unatakiwa,unaweza kuchoma nauli,ukachomeshwa mahindi na mtu usimwone.kama anania ya kukusaidia angeweza bila hata ya hizo complication
Habarini za jioni ndugu zangu,
Mimi ni dada nakaa Tabata Mangumi nilikuwa najishughulisha na biashara ndogondogo kwa kuendesha maisha pamoja na mme wangu wa ndoa aliekuwa anafanya biashara ya dagaa kutoa Kigoma kuja Dar kwa masikitiko makubwa miezi 6 imepita tangu mume wangu aende kuchukua dagaa Kigoma hajarudi mpaka leo na nikipiga simu anakata na kwa sasa simu haipatikani kabisaa
Ila kuna tetesi kwamba kaoa huko na biashara anafikisha Tabora na kurudi Kigoma.Vyombo vyangu vya ndani vimechukuliwa kwa sababu nilishindwa kulipa mkopo midogomidogo,kwahiyo kwa sasa sina kodi na sina pesa hata ya chakula ila kwetu ni Same mkoa wa Kilimanjaro.
Naombeni mnisaidie nauli tu ya kurudi kwetu Same na mwanangu wa miezi 8 na hata mnisaidie na sh.elfu hamsini tu nikaanzie biashara ya mahindi pale Same mjini.Mume ni mtu wa Kigoma.
Namba yangu ya simu ni 0712 319 836
Asanteni
Dada pole sana. Ukifika ubungo utaniambia nikufungashie mkate.. Maana mi nauza mikate pale ubungo stand
Namshukuru ndugu mwana JF Mangwelele amenitumia elfu 16 000 mda si mrefu.Mungu akubariki.
Nimeshapita Chalinze naelekea Same,Kilimanjaro.Namshukuru Mangwelele kwa 16000,namshuku Samboko kwa 5000 na Patience kwa 3500 na Kiepe Yai pokea shukrani zangu kwa kuhimiza japo hukutoa pesa ila umeonyesha moyo na kutumia mda wako kwa kuhimiza.Shukrani zangu za pekee ziwaendee JF kwa kuniruhusu kutumia Jukwaa lao kuombea msaada,nashukuru kwa walioniombea kwa Mungu nashukuru vilevile kwa wale waliokejeli na maneno machafu, tunaambiwa tushukuru katika kila jambo.Wale walioniahidi kunisadia kunipa chochote nitawashukuru mkifanya hivyo kwa maana naweza kununulia mahindi gunia moja kisha nikaanza kuuza rejarereja.Mbarikiwe NYOOOTE!
Kuna rafiki yangu flani alitaka kuja dar kuanza maisha akawa ananiambia nimuulizie nyumba za nje ya mji ndipo nikaamua nimtangazie kwa namba yake ya simu hata hivyo aliamua kwenda Tanga kuanza maisha na hata hiyo namba aliicha kutumia.