Naombeni msaada wa kuchangiwa Bima ya Afya (NHIF) ili kuokoa maisha yangu

Ni mwanaume ana miaka 41 tu masikini...Sijui kama ana mke na watoro..ila ninachofahamu ana mama hasiye na uwezo, ambaye anapitia mateso makali ya kuona mtoto wake anaumia lakini hawezi msaidia.. kama mama chukua tu dk 1, fikiria hali hiyo na hapo hapo ona nuru ikianganza kutoka kwa Miss Natafuta
Unanifaa sana wewe
 
Ahadi/ na utekelezaji wake
1. Nyani ngabu 220,000/= AMETUMA
2. Palsa. 100,000/= AMETUMA
3. Amu. 100,000/= AMETUMA
4. Anonymous1. 10,000/= AMETUMA
5. Anonymous2. 1,000/= AMETUMA

Alinda. 300,000/=
Chupaku
Nguruvi3.
Sabosabo
Mwifwa
Mwisho2016
Sosthenes
G anonymous3

Asanteni wote
Mbarikiwe sana wakuu, hakika mmetoa kwa moyo maana hapa jukwaani hatufahamiani hata kwa sura zetu labda wachache sana
 
Ni mwanaume ana miaka 41 tu masikini...Sijui kama ana mke na watoro..ila ninachofahamu ana mama hasiye na uwezo, ambaye anapitia mateso makali ya kuona mtoto wake anaumia lakini hawezi msaidia.. kama mama chukua tu dk 1, fikiria hali hiyo na hapo hapo ona nuru ikianganza kutoka kwa Miss Natafuta
Sina mtoto hata so siwezi hata kufikiria but I do understand my dear.nitajitahidi
 
Kwa mchango wowote wasiliana nami kwa +255679047446 (Tigo) / +255767157788 (Voda) au siku za Jumatatu na Alhamisi fika Muhimbili, Kitengo cha figo (jengo la watoto) ulizia ofisi za ustawi (social work) hapo ofisini ulizia mgonjwa 'John Manyama'

Habari wana jamvi wa JF,
Naitwa John. Nina miaka 41. Ni mgonjwa wa figo (Chronic Kidney Disease) ninaye fanyiwa usafishaji wa damu (Dialysis) kwenye hospitali ya taifa Muhimbili kwa takribani mwaka 1 na miezi 6 sasa.

Mwanzo gharama za usafishaji na dawa nilizimudu kutokana na akiba yangu niliyo ilimbikiza kutokana na shughuli za usimamizi wa ujenzi wa nyumba na miundombinu. Pia jamaa na marafiki nao michango yao ilihusika sana japo kwa sasa nimebaki peke yangu.

Pamoja na michango mbalimbali na akiba yangu, sikuweza kufikisha pesa (TSh 1,500,000) ya kulipia bima ya afya (NHIF).
Kilichonisukuma kuja kwenu ni kukosa namna ya kumudu gharama za usafishaji figo kwa wagonjwa wa kulipia (public) ambazo zimepanda kutoka TSh 50,000 kwenda TSh 90,000 kwa dialysis moja, wiki tatu zilizopita.

Kawaida mgonjwa wa kulipia anatakiwa afanye dialysis 2 kwa wiki. Japo awali nilipewa kiwango cha msamaha cha Sh 30,000 kwa kila dialysis lakini sikuweza kumudu kulipia zote 2 kwa wiki.

Naamini wana JF ni wasikivu na jamii ya ushirikiano. Kumbuka mgonjwa wa figo hasubiri. Akikosa matibabu wiki moja tu maisha yake yanakuwa mashakani.

Naombeni michango yenu ya bima ya afya na dialysis. Mwenyezi Mungu awabariki
.
.
.
_________November 2018 UPDATE________
Wakuu mpaka sasa mchango wa bima ya afya uliopatikana kutoka kwa members hapahapa JF ni TSh 730,000. Almost tumefikia nusu ya lengo.
Lengo ni kupata TSh 1,500,000.
Nikipata bima, itanisaidia upandikizwaji wa figo. Tayari nimepata donors wa kunipa figo hivyo nawaomba muendelee kunichangia ili tufikie lengo.
.
Pia watakaopenda kunichangia pesa ya kusafisha damu (TSh 30,000 kwa session) nitashukuru. Session ziko 2 kwa wiki. Unaweza kuchangia hata 1 kadri ya uwezo wako.
Gharama ya kusafisha damu (dialysis) sasa nimepunguziwa kutoka TSh 90,000 mpaka 30,000 kwa session.
.
Jamii moja huzungumza lugha moja
Asanteni
Pole sana mkuu..
 
Back
Top Bottom