Naombeni msaada wa kuchangiwa Bima ya Afya (NHIF) ili kuokoa maisha yangu

Bestates Tanzania

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
401
593
Kwa mchango wowote wasiliana nami kwa +255679047446 (Tigo) / +255767157788 (Voda) au siku za Jumatatu na Alhamisi fika Muhimbili, Kitengo cha figo (jengo la watoto) ulizia ofisi za ustawi (social work) hapo ofisini ulizia mgonjwa 'John Manyama'

Habari wana jamvi wa JF,
Naitwa John. Nina miaka 41. Ni mgonjwa wa figo (Chronic Kidney Disease) ninaye fanyiwa usafishaji wa damu (Dialysis) kwenye hospitali ya taifa Muhimbili kwa takribani mwaka 1 na miezi 6 sasa.

Mwanzo gharama za usafishaji na dawa nilizimudu kutokana na akiba yangu niliyo ilimbikiza kutokana na shughuli za usimamizi wa ujenzi wa nyumba na miundombinu. Pia jamaa na marafiki nao michango yao ilihusika sana japo kwa sasa nimebaki peke yangu.

Pamoja na michango mbalimbali na akiba yangu, sikuweza kufikisha pesa (TSh 1,500,000) ya kulipia bima ya afya (NHIF).
Kilichonisukuma kuja kwenu ni kukosa namna ya kumudu gharama za usafishaji figo kwa wagonjwa wa kulipia (public) ambazo zimepanda kutoka TSh 50,000 kwenda TSh 90,000 kwa dialysis moja, wiki tatu zilizopita.

Kawaida mgonjwa wa kulipia anatakiwa afanye dialysis 2 kwa wiki. Japo awali nilipewa kiwango cha msamaha cha Sh 30,000 kwa kila dialysis lakini sikuweza kumudu kulipia zote 2 kwa wiki.

Naamini wana JF ni wasikivu na jamii ya ushirikiano. Kumbuka mgonjwa wa figo hasubiri. Akikosa matibabu wiki moja tu maisha yake yanakuwa mashakani.

Naombeni michango yenu ya bima ya afya na dialysis. Mwenyezi Mungu awabariki
.
.
.
_________November 2018 UPDATE________
Wakuu mpaka sasa mchango wa bima ya afya uliopatikana kutoka kwa members hapahapa JF ni TSh 730,000. Almost tumefikia nusu ya lengo.
Lengo ni kupata TSh 1,500,000.
Nikipata bima, itanisaidia upandikizwaji wa figo. Tayari nimepata donors wa kunipa figo hivyo nawaomba muendelee kunichangia ili tufikie lengo.
.
Pia watakaopenda kunichangia pesa ya kusafisha damu (TSh 30,000 kwa session) nitashukuru. Session ziko 2 kwa wiki. Unaweza kuchangia hata 1 kadri ya uwezo wako.
Gharama ya kusafisha damu (dialysis) sasa nimepunguziwa kutoka TSh 90,000 mpaka 30,000 kwa session.
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja
Asanteni
.
.
.
______NOVEMBER 28 2018 UPDATE______
Wakuu leo nimetoka kulipia bima ya afya (NHIF) iliyotokana na michango yenu.
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote mlio fanikisha zoezi hili. Mpo wengi na wengine hawakupeda kutajwa hapa lakini wote kwa umoja wenu nasema asante.
.
Kwa sasa nasubiri kadi ya bima itoke. Itachukua siku 21 za kazi kutoka.
Kadi ikitoka itanisaidia kwenye matibabu yote ikiwemo vipimo kwa ajili ya transplant na madawa baada ya trasplant (ikiwa ntapandikizwa) isipokuwa haitaweza kunihudumia upande wa kusafisha damu (dialysis) pamoja na dawa za ku-boost damu mpaka baada ya mwaka mmoja ntakapo renew.
Hivyo kwa sasa ntaendelea kulipia dialysis mpaka pale ntakapo pandikizwa figo au baada ya mwaka ntakapo renew bima
.
Natumai tutazidi kushirikiana na kupeana updates.
Naomba mwenyezi Mungu atuongoze na kutubariki wakati tukiendelea kutimiza majukumu yetu.
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja
.
.
.
_________JANUARY 2019 UPDATE__________
Wakuu, heri ya mwaka mpya. Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi ya uhai na kufanya historia ya maisha yangu kuingia mwaka 2019.
.
Nimewaletea taarifa kuwa ile kadi ya bima ya afya niliyo kuwa nikiisubiri kwa ule muda wa siku 21, sasa iko mikononi mwangu, nina maana nimesha ichukua toka mfuko wa bima wa taifa (NHIF)
.
Nawashukuru sana kwa kazi kubwa mlio ifanya.
Mwanzo ilionekana ni kitu kama hakiwezekani hivi, kumbe inawezekana.
Niliwaamini ndo maana nilileta ombi langu kwenu. Kuna mitandao mingi ya kijamii lakini mi niliona Jamii Forum ndo ina watu wenye ukweli kwa maana kwamba mtu akisema ndiyo inakuwa ndiyo kweli, akisema hapana inakuwa hapana kweli.
Mitandao mingine imetawaliwa na maroboti. Roboti linaweza ku-like au ku-comment post yako, ukasema ni mtu kumbe ni roboti.
.
Narudia kuwashukuru kwa hapa tulipofikia.
Jambo la nyongeza, napenda kukumbushia kwa wale watakao wiwa kunichangia pesa ya kusafisha damu (dialysis) kwa mwaka huu 2019 wakati nikisubiri bima ikomae, nawakaribisha.
Hili nililieleza kwenye update ya November 28 2018, unaweza kupitia ukasoma.
.
Mwenye mchango anaweza pitishia kwenye namba hizi:
0767157788 (M-Pesa) au 0679047446 (Tigo Pesa) Jina litakalo tokeza ni John Makanga
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja.
 
Madocta walisema ugonjwa ulisababishwa na nini?
Inaonekana nilikuwa na presha ambayo mimi mwenyewe sikuitambua. Sikuwahi kupima presha toka nimezaliwa mpaka hapo nimekuja kuumwa figo.
Sikufikiria swala la presha ya kupanda sababu nilijua inakuwa kwa watu wenye uzito mkubwa au wanene. Mimi toka mdogo mpaka sasa ni mwembamba na uzito wangu haukuwahi kuzidi kilo 57.
Kichochezi cha ugonjwa kilikuwa dawa za malaria. Nilikutwa na malaria, nikapewa dawa za mseto. Nilipomaliza dozi tu tatizo likaanzia hapo
 
Aisee pole sana mkuu
 
Kwa mchango wowote wasiliana nami kwa +255679047446 au siku za Jumatatu na Alhamisi fika Muhimbili, Kitengo cha figo (jengo la watoto) ulizia ofisi za ustawi (social work) hapo ofisini ulizia mgonjwa 'John Manyama'

Habari wana jamvi wa JF,
Naitwa John. Nina miaka 41. Ni mgonjwa wa figo (Chronic Kidney Disease) ninaye fanyiwa usafishaji wa damu (Dialysis) kwenye hospitali ya taifa Muhimbili kwa takribani mwaka 1 na miezi 6 sasa.
Mwanzo gharama za usafishaji na dawa nilizimudu kutokana na akiba yangu niliyo ilimbikiza kutokana na shughuli za usimamizi wa ujenzi wa nyumba na miundombinu. Pia jamaa na marafiki nao michango yao ilihusika sana japo kwa sasa nimebaki peke yangu.
Pamoja na michango mbalimbali na akiba yangu, sikuweza kufikisha pesa (TSh 1,500,000) ya kulipia bima ya afya (NHIF).
Kilichonisukuma kuja kwenu ni kukosa namna ya kumudu gharama za usafishaji figo kwa wagonjwa wa kulipia (public) ambazo zimepanda kutoka TSh 50,000 kwenda TSh 90,000 kwa dialysis moja, wiki tatu zilizopita.
Kawaida mgonjwa wa kulipia anatakiwa afanye dialysis 2 kwa wiki. Japo awali nilipewa kiwango cha msamaha cha Sh 30,000 kwa kila dialysis lakini sikuweza kumudu kulipia zote 2 kwa wiki.
Naamini wana JF ni wasikivu na jamii ya ushirikiano. Kumbuka mgonjwa wa figo hasubiri. Akikosa matibabu wiki moja tu maisha yake yanakuwa mashakani.
Naombeni michango yenu ya bima ya afya na dialysis. Mwenyezi Mungu awabariki
 
Ila pamoja na hayo ungeweka walau picha za vyeti ili kuleta uhalisia wa kile ambacho tunapaswa kukuchangia maana hali ya udanganyifu inazidi kupanda kila kukicha. Mungu akubariki sana
Natumia faili ambalo linabaki Muhimbili. Nilizonazo binafsi ni risiti za malipo ya wodini, vipimo, madawa na dialysis. Ukihitaji, nakutumia
 
Back
Top Bottom